Zitto afafanua kuhusu deni la Taifa... kila Mtanzania anadaiwa Tshs 488,000

Kama ni kweli hali ndiko inakoelekea kuna haja gani ya kuwa na serikali isiyoweza kuboresha hali ya waajiri wake (sisi wenyenchi)?! Kwa kweli kuna kila haja ya kufikia wakati wa kufanya mapinduzi, haitakuwa dhambi kama tukiwavua madaraka hawa viongozi wote wanaotupotosha na kuanza upya!
 
Wanikate kwenye PAYE yangu nimalizane nao!! Nadhani miezi miwili ntakua shamaliza deni langu hili la 488k.

Umenena lakini, deni hilo ni tofauti na PAYE... Ndo maana TRA imekusanya mapato kwa 106% na PAYE ikiwemo lakini bado unadaiwa 488k. Ha ha ha ha haaa
 
Nilichoelewa mimi hapa inamaana kuwa serikali hii imekuwa chanzo kikuu cha maisha mabovu ya Watanzania pesa hizi walizotukopea wangetupa wenyewe, kila mmoja angeweza kujikimu japo kwa milo miwili kwa siku, kuwa na tolori la machungwa ukiuza pia ingetosha
 
Siasa bana, kawachanganya wananchi na kuondoka,

Angekuwa mkweli angewaeleza pia kuwa hilo deni ndo linalipa mshahara wake na hata gari alilopanda ni sehemu ya deni hilo.
Pia aeleze kuwa hilo deni sehemu imetumika kulipa ruzuku ya chama chake ambacho kinapokea mamilioni ya shilingi kila mwezi toka serikalini.
Vinginevyo ni upotoshaji na kujaribu kuwadanganya wananchi ambao hawawezi kuelewa vizuri mambo hayo.
Duh kweli wewe ni mwanasiasa pia. Maana kama mkipangwa jukwaa moja na huyu kijana unauwezo wa kumshinda aisee! Hoja yako ni nzito, mie naikubali kabisa.
 
Back
Top Bottom