Wataalamu wa Uchumi hii ni kweli kuhusu Deni la Taifa?

Yenga08

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
464
891
"Deni la Serikali kufikia June 30,2022 lilikuwa Tsh. Trilioni 71.31 ikilinganishwa na Tsh. Trilioni 64.52 lililoripotiwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kuna ongezeko la Trilioni 6.79 sawa na 10.5%, ambapo kipimo cha deni la Serikali kinachotumia pato la Taifa kinaonesha Deni hili ni himilivu”

Akiongea kuhusu deni hilo la Taifa baada ya CAG kumaliza kusoma Ripoti hiyo, Rais Samia amesema yafuatayo ——— > “Mwenendo wa Deni la Serikali tunakopa ndio, tunakopa kwa maendeleo lakini tunakopa kwa akili, tusipokopa hatutofanya maendeleo lakini lazima tukope mikopo yenye unafuu tufanye maendeleo”

“Tuko vizuri, mikopo ndio maendeleo tutaendelea kukopa lakini tuko makini kwamba lazima tuwe chini ya viwango tulivyowekewa” ——— Rais Samia.
 
Wanakopa pesa zenyewe wananunua matreni ya zamani, pesa za miradi wanadouble hii nchi mpk nije kuwa Rais imeshoza sana.
 
Hapo Samia aliamua kumjibu CAG, lakini sijaona popote kama taarifa ya CAG ilikuwa na swali kwa Samia mpaka akaamua kumjibu.

Sijui ni maendeleo gani wanayofanya huko serikalini kwa mikopo, ikiwa ameacha wezi watuibie mabilioni na hawafanyi chochote.

Hii inaonesha wazi kuna sauti ndani ya Samia inamwambia kukopa kila siku sio vizuri, ndio maana anakosa amani kujibu hata pale ambapo hajaulizwa.
 
Mfanya biashara yoyote mwenye akili timamu, hakopi pesa ya kuchezea/kuchezewa na mtu yeyote, ama ndugu na ama mzazi wake kabisa, atalala naye mbele, kwa sababu anajua, kitu kidogo tu, anaanguka na biashara inaanguka.

Kukopa sio vibaya! Shida ni, unasimamiaje hiyo mikopo kuhakikisha hata ile thumuni haipotei?

Tufikiri kwa pamoja! Mikopo iliyokopwa 2021/2022 inawiana na miradi kule ilikoelekezwa?

Ninauhakika kwamba! Ni 49%tu yamikopo yote ndio hufika kwenye eneo la tukio na kufanya kazi!

51% zinaishia kwa mafisadi na ndiyo hayo yanayomzomea JPM kwamba hakufaa kuongoza kwa sababu ukweli hakuruhusu mbwa kulamba asali.
 
Back
Top Bottom