MBARALI MBEYA.
1.Fursa ya kilimo cha mpunga, hapa utapata mashamba kwa bei rahisi kwa sehemu zisizo na skimu ya kutumainiwa sana kama vile vijiji vya kuanzia ilongo kushuka chini yaani igalako, ruiwa,mwela,mahango, mpaka nako. Pia utapata sehemu za kulima kwa kumwagilia kama vile mradi wa kilimo cha umwagiliaji Kapunga-chimala.
Pia kilimo cha vitunguu maji Igawa-Mbarali, kilimo cha mahindi yanakubali sana ingawa wadau wanalima sana mpunga na kilimo cha maharage haya hukubali hasa kwenye mashamba ambayo hayalimi mponga. Pia bila kusahau kilimo cha alizeti, matikiti maji, matango na nyanya, hoho nk.
2. Ufugaji, hapa utafaidika na ukubwa wa eneo la hii wilaya na ardhi huwa inauzwa sio kwa bei kubwa sana. Hapa ufugaji wa kuku na nguruwe itakulipa sana. Ila ufugaji wa ng'ombe huwa changamoto sana hasa kipindi cha kiangazi maana mvua hukata katikati ya april na kufanya eneo kuwa kavu sana hivyo kukosa sehemu sahihi ya malisho ingawa kuna sehemu za malisho ya serikali.
3. Biashara sio mahari sahihi sana kutokana na idadi ya watu na ukubwa wa eneo maana idadi ni ndogo hivyo uwezo wa manunuzi ni mdogo. Na pia miundombinu ya barabara na afya si mizuri ,ukitoa barabara ya lami iliyopita kutoka Igawa kwenda mbeya mjini na iliyotoka Igawa kwenda Ubaruku hakuna nyingine zaidi.
Kwa watafutaji wa kutumia nguvu zaidi , nyakati za hela ni kipindi cha kuanzia November mpaka March mwishoni ndio kunakua na kazi nyingi za kuandaa mashamba ya mpunga, kupanda mpunga na kupalilia. Pia nyakati za mavuno kuanzia May- july kwa wabeba mizigo kazi zipo na wale wakushona na kuanika vipeto vya mpunga.
Kwa wazee wa fursa za biashara kipindi cha Mavuno ni kizuri maana utapata mpunga kwa bei rahisi nawe ukakonoe uuze mchele au uweke stoo uuze baadae ( zingatia hiyo biashara siyo rahisi kama mtu anavosimulia maana kupigwa kupo ukienda kizembe).
Zingatia kipindi cha maandalizi ya shamba, kupanda mpunga mpaka kupalilia wanawake wanahelea ( vichenchi kuliko wanaume zao) hiyo ni kulingana na hali ya uchumi wa wanachi wakule. Na kama unaalergy na jua hakika si sehemu salama nadhani ukitoa jua la Wang'ing'ombe-Njombe pale jua ni kama moto wa jehanam hasa miezi ya february, na june,july, August(Hatari sana) mpaka October.