Zitambue wilaya za Tanzania na fursa zake ki biashara, ufugaji na kilimo kwa hiki kipindi...

kinundu

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
2,020
2,000
Kwanza nianze na kusema kwamba fursa Ni nyingi sana ila tatizo mitaji tuu... Ma haswa watu wasio na mitaji kama mimi hizi fursa tunaziona sanaa..

1.KYELA, MBEYA TANZANIA NA FURSA ZAKE
=ufugaji
Hii wilaya ina uhaba wa wafugaji wa kuku wa mayai, kuku wanyama na ng'ombe wa maziwa

Kyela tunategemea mayai kutoka tukuyu haswa haya mayai ya kisasa, tunategemea maziwa kutoka tukuyu kuanzia mgando hadi fresh wenye mitaji wote hii ni fursa kuwekeza

Kuku wa nyama haswa watu wa huku wanapendelea sanaa kuku wa kienyeji hvyo ukiwa mfugaji wa kuku wa kienyeji utakula sana pesa kwa maana wanunuzi wanapata shida kwa kuzunguka na matenga kusaka kuku vijijini hivyo ukiwa na mifugo yako wanunuzi wote wanakuja kwako...

= biashara
Kuna ujenzi wa barabara ya rami kutoka kyela mjini hadi matema beach.. Hivyo basi ni FURSA kwa wafanya biashara kuleta daladala zenu hoi bara bara ikikamilika...

Mtakua na root kama hizi
-Boda to ipinda
-Kyela mjini to ipinda
-ipinda to ngyekye
-ngyekye to matema beach

Kwa sahivi tunatumia Noah ambazo wanatuchaji 1500 kama Paulo NA umbali kutoka mabibo hadi kariakoo hiyo root ha kyela to ipinda mkileta costa itapendeza kwa 500 itakua shangwe..

= kilimo
Mpunga kyela unalipa sanaa ila tumekosa kuliko cha kisasa ili tupate mazao mengi mnoo kilimo chetu ni cha kutegemea mvua japo tuna mito mitatu mikubwa moto mbaka, kiwila, lufilyo na mto songwe jumlisha na ziwa nyasa

Lakini kuna maeneo kama mabunga wanalima kilimo mara mbili maana mashamba yao yanatunza unyevunyevu.. Kumbuka mpunga wa kyela unasoko NC hi nzima na ni mtamu alafu unabei kubwa..

Kokoa Nazo zipo NA zinastawi vizuri..

Wenye kipato na mitaji karibuni kyela..

Hali ya hewa ni joto sip baridi...

twambie fursa za wilaya uliopo tuje tufanye kazi kumbuka uzalendo ni kupeana deal.. Karibuni
 
stonebrige

Member
May 21, 2014
15
45
Mimi nipo shinyanga kwa sasa lakin bado sijaona fursa nilikua kahama kwa kahama naweza sema watu wa pale wanalima mpungunga wanalisha baadhi ya wilaya jiran pia kuna kilimo cha dengu maeneo ya msalala na kishapu hizo ni halmashauri jiran na kwa sababu magari mengi ya kwenda congo, rwanda kigali na burundi hivyo usafirishaji wa bidhaa kutoka nchi izo ni rahisi kupelekea mzunguko wa kibiashara kuwa mkubwa hapa kahama. Naomba kama kuna mtu wa shinyanga mjini au hata old shy anipe fursa plz
 
stonebrige

Member
May 21, 2014
15
45
Mood naomba huu uzi uwe endelevu usiutoe wala kuunganisha na mwingine

Kweli usemayo mimi nimekaa kiwira karibu na mto kiwira wanalima mananasi kwa wingi
 
kinundu

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
2,020
2,000
Mimi nipo shinyanga kwa sasa lakin bado sijaona fursa nilikua kahama kwa kahama naweza sema watu wa pale wanalima mpungunga wanalisha baadhi ya wilaya jiran pia kuna kilimo cha dengu maeneo ya msalala na kishapu hizo ni halmashauri jiran na kwa sababu magari mengi ya kwenda congo, rwanda kigali na burundi hivyo usafirishaji wa bidhaa kutoka nchi izo ni rahisi kupelekea mzunguko wa kibiashara kuwa mkubwa hapa kahama. Naomba kama kuna mtu wa shinyanga mjini au hata old shy anipe fursa plz
Huo no uzalendo mkuu... Kumbuka uzalendo ni kupeana deal
 
Zillion

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,008
2,000
Fursa nzuri mkuu, bt as long as una afya njema, mikono na miguu nadhani sio sahihi kusema mtaji ni tatizo.
 
willy ze great

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
882
1,000
Musoma mjini tumezungukwa na ziwa victoria hivo kupelekea watu wengi hasa kabila la wajita, wakwaya na jamii zake kuwa wavuvi wa samaki na dagaa, kwangu mimi naona fursa kubwa ni kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki hasa sato kwaajili ya kuuza viwandani na kupeleka masoko kama ya nyasho, kamnyonge na town mwigobero kwani bei ni nzuri hebu nambie samaki wa kilo mbili unauza mpaka 9000. Mungu anisaidie nimemalize chuo lazima niwekeze kwenye ufugaji wa samaki. karibuni msoja mjini
 
binjo

JF-Expert Member
Feb 22, 2016
2,117
2,000
Kweli usemayo mimi nimekaa kiwira karibu na mto kiwira wanalima mananasi kwa wingi

Ikuti ndani ya wandali na wanyaki

Nyanya wameanza kulima nazo kama wawili hivi.

Tikitiki maji mmoja

Vitungu bamia nyanya nyungu hoho karoti mboga za majani tangawizi vyooooote hivi na vingine havina mlimaji

Wanalima kwa mazoea

NANASI imekuja Leo

Daàah tango haukuna

Au tatizo hali ya hewa?
 
Mirautz

New Member
Dec 5, 2017
4
20
Mkuu niliwahi kuskia shinyanga Pumba ya mahindi wanauza bei cheap sana means ukisafirisha kuja kuuza maeneo km arusha italipa sana,, nipitaman kufanya iyo tho cjupata taarifa sahihi kama ni kweli ni cheap au laa,,
Kwa livoskia gunia la kg50 wanauza 8000-10000 akat kwa arusha ni 24000-25000
Mimi nipo shinyanga kwa sasa lakin bado sijaona fursa nilikua kahama kwa kahama naweza sema watu wa pale wanalima mpungunga wanalisha baadhi ya wilaya jiran pia kuna kilimo cha dengu maeneo ya msalala na kishapu hizo ni halmashauri jiran na kwa sababu magari mengi ya kwenda congo, rwanda kigali na burundi hivyo usafirishaji wa bidhaa kutoka nchi izo ni rahisi kupelekea mzunguko wa kibiashara kuwa mkubwa hapa kahama. Naomba kama kuna mtu wa shinyanga mjini au hata old shy anipe fursa plz
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom