Zipi sababu za wanaume kutelekeza ujauzito?

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Katika mahusiano kumekuwa na tabia ya wanaume kukimbia ujauzito na kutelekeza watoto pasipo sababu za msingi. Ukizingatia kuwa mwanaume ndiye aliyemshawishi mwanamke kwa kinywa chake mwenyewe kwamba washiriki tendo la ndoa.

Wanawake wamekuwa mstari wa mbele kuhimiza matumizi ya kinga huku wakifahamu fika kuwa wao ndio wanaobeba ujauzito lakini wanaume wamekuwa wakitaka kushiriki tendo la ndoa bila kinga na ujauzito unapotokea basi wanaume wanakuwa wa kwanza kukimbia majukumu ya kulea kichanga sababu inayowapelekea wanawake kuharibu ujauzito.

Wakati mwingine nimekuwa nikijiuliza pengine wanaume wamekosa uwezo wa kulea watoto lakini la hasha! Wapo wanaume matajiri wanaotelekeza ujauzito na inapelekea mtoto kuzaliwa na kuishi maisha duni ingawa baba yake anamiliki mali nyingi.

Je zipi sababu za wanaume kutelekeza ujauzito?

images.png
 
Nikipiga hesabu tu bado mda wa mimba na tarehe niliyopiga game ni tofauti

Bado unasikia za chinichini demu kicheche au umefuma message

Hapo lazima niikatae ukinisumbua naama na mkoa kabisa

Nimekwambia sina shida ya mtoto kwa sasa life liko tight ni demu wangu mi mwenyewe msela unga unga mwana kwangu pakavu tia mchuzi halafu unanitegeshea ..yaani ndio unioni tena

Hizo ndio sababu
 
Inategemea, maana wanawake wengine wanakubebea mimba na hukuplan ani anakudanganya tarehe zake then anakuja kukuambia ameconceive, na wakati mwingine pia unakuta mtoto sio wako

Mwanamke akikupenda anaweza kukupa mimba sio yako, na akikuchukia hata mimba yako atakugomea kua sio yako
 
Katika mahusiano kumekuwa na tabia ya wanaume kukimbia ujauzito na kutelekeza watoto pasipo sababu za msingi. Ukizingatia kuwa mwanaume ndiye aliyemshawishi mwanamke kwa kinywa chake mwenyewe kwamba washiriki tendo la ndoa.
Waambie hao wanawake baadhi waache tabia ya Kutegeshea Mimba ili Wamshike Mwanaume, Na wasizae kabla ya Ndoa. Wasiposikia Wataendelea kutendwa hadi Waione Dunia gunia
 
Hata mimi yamenikuta na nlimuweka wazi mapema kwamba kwa sasa siko tayari maana yeye alisema anataka kupata mtoto.

Asee! baada ya mwezi ananiambia ana ujauzito na nlilala nae siku1 tu tena nlizingatia tarehe alizonambia ametoka period na nikatumia period tracker
 
Back
Top Bottom