Mpinzire
JF-Expert Member
- Jan 18, 2013
- 7,229
- 12,954
Kwa muda sasa kumekuwa na kashikashi kati ya Rais Trump na viongozi wa chama cha Democratic juu ya kutaka kujenga Ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico, Democratic ni wazi hawataki ukuta ujengwe zaidi ya kumtaka rais Trump azidishe tu ulinzi huko border huku Trump bado akishinikiza lazima ukuta ujengwe kiasi kupelekea ata shughuli za Serikali kusimama kwa muda sasa katika Wizara 8..
Swali langu la msingi hapa linalonifanya nishindwe kuelewa kizungumkuti hiki..!
1. Je, Democratic wanafaidika moja kwa moja na udhaifu uliyopo huko boda..?
2. Zipi hasara ambazo Marekani kama taifa itazipata endapo ukuta utajengwa..?
3. Nini kitatokea kama hali ikiendelea kuwa hivi?
Wafuatiliaji wa habari za Kimataifa naomba mnijuze?