Serikali ya Marekani bado yafungwa. Rais Trump ashinikiza kupewa fedha za kujenga ukuta

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Rais Trump alieleza akiwa White House siwezi kusema lini serikali itafunguliwa. Naweza kusema serikali itafunguliwa pale tutakapokuwa na fedha ya ukuta au uzio chochote wanachokiita

Kufungwa kwa baadhi ya idara za serikali kuu ya Marekani hakuonekani kuwa suluhisho la karibuni litapatikana huku Rais Donald Trump akisisitiza siku ya Jumanne kuwa serikali itaendelea kufungwa mpaka madai yake ya kutaka fedha za ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico yameridhiwa.

"Siwezi kusema lini serikali itafunguliwa. Naweza kusema itafunguliwa pale tutakapokuwa na fedha ya ukuta, uzio chochote wanachokiita" Trump alisema kwenye ofisi yake huko White House baada ya kuzungumza na wanajeshi wa Marekani kwa njia ya video walio kwenye mataifa ya nje.

Rais Trump alidai kuwa maelfu ya wafanyakazi wa serikali ambao wako nyumbani kutokana na serikali kuu kufungwa pia wanataka ukuta ujengwe licha ya ukosefu wa ushahidi wa kuunga mkono madai yake.

Jumatatu Trump alisema wademocrat lazima wamalize tatizo hili wakati viongozi wa Democrat katika bunge wamemlaumu Trump kwa kuitumbukiza nchi katika vurugu.

Chanzo: VOA Swahili
 
Mbona Magu anachota tu, si na yeye achote!
 
Trump na magu ni manabii wa mataifa haya mawili karne hii ya 21.

Inasemekana ni ndugu hawa,trump baada ya kumaliza darasa la saba huko chato alipata wafadhiri akaondoka na kwenda kusoma marekani,akiwa huko alianza mikakati yake ya biashara na maisha,kisha siasa-mpaka alipotusua urais,bado wanawasiliana kwa simu kupeana mikakati mbali mbali.
 
Mbona Magu anachota tu, si na yeye achote!
Huko Marekani mwenye maamuzi ya mwisho
katika matumizi ya mapato ya taifa si Rais Trump...
Ni wananchi kupitia wawakilishi wao.

Hapa Tanzania mwenye maamuzi ya mwisho
katika matumizi ya mapato ya taifa ni Raisi Magufuli...
Si wananchi kupitia wawakilishi wao.
 
NO, NOT AT ALL. NA TANZANIA NI WANANCHI, MADARAKA YA WANANCHI YAMEPORWA NA DIKITEITA
 
Back
Top Bottom