Zingatia haya ukiwa ukweni

Jitu la kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,446
Reaction score
7,990
Ukienda kusalimia ukweni muda wa wiki moja kuna tabia ambayo shemeji zako wanazo wanaamka saa 11 alfajiri halafu wanasogoea karibu na mlango wa chumba ulicholala wanagonganisha majembe, hii ni ishara ya wewe uamke uwende nao shambani kulima.

Usiwe mzembe amka nenda nao shambani kapige jembe kweli kweli ili warudi kusimulia kwa wakwe zako na itakuwa heshima kwa mkeo Pia hakikisha unapunguza matumizi ya simu.

Uwapo ukweni usipende sana kukaa karibu na wazazi wa mkeo we nenda ndani kaa au eneo maalumu lilotengwa kwa ajili ya kupumzikia ucheze na watoto michezo itakakayowafanya wakupende huku ukiwapa na vihela vya kununua pipi mara kwa mara.

Usiende jikoni kumuuliza mkeo kama amechelewesha chakula we tulia mchatishe kwa simu atakupa utaratibu na mambo yatakuwa sawa pia hakikisha unakuwa wa kwanza kushiba hii itakusaidia sana kukuamini.
 
Mkuu......really???

Kama mimi isije ikatokea huo mchezo wa kugongesha majembe mlango wa chumba nilicholala maana itawabidi wakaitishe kikao cha ukoo wao wanijadili,yaani hapo ndo watakuwa wameniamsha nifanye kile nilichomlipia mahari dada yao.

By the way, unakaaje ukweni wiki daraja linalounganisha vitongoji na mjini limekatika au?
 
Ukienda kusalimia ukweni muda wa wiki moja kuna tabia ambayo shemeji zako wanazo wanaamka saa 11 alfajiri halafu wanasogoea karibu na mlango wa chumba ulicholala wanagonganisha majembe, hii ni ishara ya wewe uamke uwende nao shambani kulima...
Niwe wa kwanza kushiba wakati sijashiba, sijakuelewa lengo lako hasa.
 
Ukienda kusalimia ukweni muda wa wiki moja kuna tabia ambayo shemeji zako wanazo wanaamka saa 11 alfajiri halafu wanasogoea karibu na mlango wa chumba ulicholala wanagonganisha majembe, hii ni ishara ya wewe uamke uwende nao shambani kulima.

Kwa sie ambao ukweni kwetu ni mjini na sio vijijini, kuna ishara zipi?
 
Niliwah kumpelekea moto ukweni na dada mtu akainasa audio
 
Cha kufia njaaa nini [emoji1787]
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…