Zinduna Talk Show: Leo mjengoni nipo na Platozoomn~~~!

11. Je ni tukio gani liliwahi kukufurahisha sana?

Mengi tu ila nalokumbuka kwa haraka ni kufaulu kwenye mtihani wa darasa la Saba.

12. Je unapenda kuvaa nguo za aina gani?

Za mtumba tena zinazofit mwili wangu.

13. Ukipata fursa ya kupata staftahi na King'asti, Je ungapenda kujadili jambo gani na yeye?

Kabla ya kujadili naye jambo lolote ningependa kumchungua kama ana kijungu na chuchu saa sita au saa kumi na mbili saa za kigoma! Halafu baada ya hapo ningependa tujadiliane naye kwa nini siku hizi mabinti wanapenda vibabu, halafu baada ya hapo ningemuuliza vipi Yule mzungu aliyemwachia e-mail kwa ahadi ya kumtumia tketi ya kuingia mamtoni ana mpango wa kumroga au ndio nipotezee tundi limekwenda bure?
Zaidi ya hivyo ningependa nijadiliane naye kwa nini mabinti wa JF wanajigonga sana kwa Mods!
 
Last edited by a moderator:
Ningependa kuwashukuru wasaidizi wangu waliofanikisha interview hii, fundi mitambo yupo Young Master akisaidiana na Mentor, na C6 . Anayefanikisha kurusha matangazo haya ni Bujibuji akisaidiwa na Nicas Mtei na pia Jiwe Linaloishi.

Kuna wale wanaowatuletea maji ya kunywa makoo yakikauka. Yupo cacico, snowhite, marejesho, charminglady, gfsonwin, Ciello, Kaunga, nivea, Yummy na lara 1.

King'asti
yeye ndiye Director wa kipindi hiki.

maji ya kilimanjaro yameisha huku... kuna togwa "busara" niliyoandaa kwa ajili ya platozoom je utaipenda da Zinduna????
 
Last edited by a moderator:
14. Je ni mwana JF gani unavutiwa na post zake, yaani ukiona jina lake tu kama ame-post thread unashawishika kuifungua ili kujua kilichomo?

Bila shaka nguruvi 3

15. Je ni jambo gani umewahi kulifanya kwa faida ya nchi yako na ambalo hata ukifa litabaki kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo?

Kupanda miti mitano........kama wachimvi hawataikata nina imani itasadia kizazi kijacho kwa kuwaletea mvua badala ya kutegea waganga kutoka Thailand!
 
Last edited by a moderator:
swali kwa omura omweito platozoom...
kwanini ulitahiriwa kwa ganzi? huoni kama ni kinyume cha mila na desturi???? je hukuona fahari na wewe kwenda "kibhagha"?????
 
Last edited by a moderator:
Ukipata nafasi ya kuwa PRESIDENT WA TZ KWA MUDA wa mwaka mmoja utafanyaje? je kati ya ccm na chadema wapi upendo wako umeegemea?

Nitatumia robo tatu ya bajeti kuhakikisha nalima mashamba makubwa ya mazao ya chakula na kufuta kabisa tatizo la njaa. Unafikiri hiki kizazi kwa nini ni kina akili kama za mchwa au panzi? Ni kwa sababu hakikupata chakula cha kutosha kwenye makuzi yao (kumbuka unga wa Yanga).

Mzungu akiwa na njaa ndipo akili yake inafanya kazi ya kuvumbua na kutatua matatizo lakini Mwafrika akishiba ndio akili yake inafanya kazi vizuri, lakini akiwa na njaa anakuwa mwizi, muuaji, mbea, mshari n.k.

Nayasubiri maombi yako
 
swali kwa omura omweito platozoom...
kwanini ulitahiriwa kwa ganzi? huoni kama ni kinyume cha mila na desturi???? je hukuona fahari na wewe kwenda "kibhagha"?????

Aaaah, wazazi wenyewe hawakuwa wanamaind hizo, halafu ile habari ya kutembezwa mitaani kama mwizi nilikuwa siipendi!
 
platozoom when growing up ulikuwa unapenda kula nini, ambacho ukifichiwa unaweza kufanya lolote mradi ukipate ule then roho yako itulie?
 
Last edited by a moderator:
Thwari ra nyongeza mhethiwa supika:
Sasa wewe platozuni embu twambie ushawahi kwenda kwa kalumanzila? Ulienda kumroga nani?

Nilienda kutafuta utajiri lakini masharti yakanishinda.............Yaani nitembee kilomita 5 peku nikiwa na bukta na hvi viguu vyangu...!kha
 
platoozoom je ushawahi kupigana? Ulipgana na nani? Mwaka gani? Mlipgana kwa sababu gani?

Nilipigana ilkuwa nyakati za foolish age, nilimg'oa jino (ingawa tayari lilikuwa bovu na limelegea), ugomvi wenyewe ulihusu nani zaidi. Pamoja na kunitwisha ngumi za haja lakini kwa sababu nilimtoa damu "nikatangazwa' mshindi.

Ya pili ni ugomvi wa mawe (nilikozaliwa hii ilikuwa kawaida) akanitoa ngeu ila yaliisha salama!
 
heheheheheeeeee
nahisi ulikuwa unalamba vidole na sahani............na sufuria pia wlaiendea ulambe
lol! maana kutaja tu mdomo umekucheza hahahahaaaa safi sana

Bado unapenda kula wali haragwe?


Mpka mdomo umecheza..........Wali harage halafu iwe kiporo naweza kujing'ata lipsi.
 
Back
Top Bottom