Inasikitisha kwamba wengi wetu tunasahau historia haraka hivi, na inakuwa rahisi kwetu kuwa influenced na vyombo vya magharibi.
Issue ya zimbabwe ni ya kihistoria. Wengi wetu tumesahau kwamba zimbabwe ilikuwa ni kama symbol ya independence movements za africa miaka ya 60-80. Pamoja na kwamba, zimbabwe ilipata uhuru kabla ya south africa na namibia, lakini ilionekana kwamba ilikuwa turning point, na matumani yakawa makubwa kwamba nchi zilizobaki zingefanikiwa soon.
Hatua serikali ya Mugabe ilizochukua katika suala la ardhi, in a perfect world, ilitakiwa kuchukua baada tu ya uhuru, lakini kumbuka, huku south africa ikiwa bado chini ya makaburu, z'bwe haikuwa kwenye position, kisiasa, kijeshi au kiuchumi, ya kufanya hivyo. Hapa simtetei kwa nini imechukua this long kufanya maamuzi haya, kuna uwezekano kwamba alijisahau au kama wengine wanavyosema, amechukua hatua hizi ili kupata political support ndani ya nchi (ingawa nakataa kuamini sababu hizi zote mbili), lakini ukweli ndiyo huo kwamba ni hatua iliyotakiwa kuchukua, hawa wazungu wanaolalamika wamenyang'anywa ardhi wawalaumu wazee wao kwa 'kuwaleta' afrika! Matatizo ya zimbabwe ya kiuchumi yanatokana na sanctions (illegal sanctions) kuliko sera ya ardhi. Definetly, sera ya ardhi, especially jinsi ilivyokuwa aggressive ingeleta mtitisiko wa mazao kwa kipindi kifupi, lakini statistics zinaonyesha z'bwe walikuwa kwa miaka mingi na surplus kila mwaka kwenye mazao, kiasi kwamba hiyo isingeathiri supply, at least siyo kwa rate iliyotokea. Ndiyo maana nasema illegal sanctions ndiyo zimechangia hizo inflation na matatizo mengine.
Ningependa tujikumbushe kwamba, pamoja na kwamba africa, technically tumeamua kumove on baada ya ukoloni, kwa maana ya kwamba hatujadai fidia au kutaka msamaha kutoka kwa watawala wetu wa zamani, hii haizuii some measures kuchukuliwa kurekebisha baadhi ya mambo. Nyerere alijaribu kureverse baadhi ya mambo, kama unakumbuka moja ya dai kubwa la Mwalimu kuhusu ujamaa, ni kwamba, africa kabla ya ukoloni tulikuwa wajamaa, yeye alichokuwa anajaribu kufanya ni kuturudisha jinsi tulivyokuwa tunaishi, lakini kwa kuwa mimi na wewe hatukuwa na kumbukumbu zozote ya jinsi tulivyokuwa tunaishi miaka 80-90 kabla, tukampinga. Zaidi, kilichomuangusha zaidi, ni kwamba nchi za magharibi na zenyewe hazikushirikiana naye.
Lumumba na yeye alikuwa anaonekana anaelekea huko huko. Nani asiyejua role ya marekani na ubelgiji katika kumuondoa, na hadi kumuua Lumumba? Hivi mnadhani Kabila kama raisi aliyechaguliwa kidemokrasia, hana haki, na hata wajibu, wa kuaddress events zote zilizotokea baada ya uhuru, especially foreign involvement? Matter of fact, Laurent Kabila alikuwa ni pro-lumumba.
Vipi kuhusu Nkrumah? Naye pia alikuwa anajaribu kuaddress effects za ukoloni na advocate measures za kuturudisha tulipokuwa, ikiwemo african union. Kilichomtokea ni kile kile wanachojaribu kumfanyia Mugabe, ingawa Mugabe amehakikisha 'wana-mtandao' ndani ya nchi na majirani wapo naye! Kama umesoma kilichomtokea Mzee Kwame, ni kwamba waliangusha bei ya cocoa, matokeo yake uchumi ukaanguka, na zaidi ya hapo kulikuwa na direct involvement ya cia katika operation nzima iliyomuondoa. Je tumove on bila kuaddress hizi issues?
Vipi hukusu angola? Kuna evidence nyingi zinazoonyesha marekani walimsupport savimbi na unita, against a legitimate govt ya angola, je hiyo haikuwa terrorism on the part of the cia and other usa agencies? Je dos astos hana haki, au hata wajibu wa kuuliza maswali hukusu kilichotokea angola kwa karibu miaka 30 ikiwemo vifo vya maefu ya watu, maelfu kuwa vilema wa maisha, eneo kubwa la ardhi kuwa unusable kwa sababu ya landmines etc.
Tukirudi kuhusu zimbabwe, measures alizochukua Mugabe ni long overdue. Sidhani kama utaratibu uliokuwa initiated na britain, wa kuipa serikali ya z'bwe pesa ili iwalipe white farmers ni sahihi, actually nadhani ni mbovu, na for once, tuone kwamba kuna actions viongozi wetu wanachukua in the best interest ya nchi zetu, siyo tunalaumu tu. Kuna wanaosema, mashamba walionyang'anywa wazungu wamepewa wafuasi wa Mugabe, basi kama Mugabe ana wafuasi wengi kiasi hicho, idea kwamba nchi nzima ya z'bwe ipo against Mugabe inatokea wapi?
Huko South Africa, wameanza kubadilisha majina ya mitaa, ambayo inaonekana ina majina ya kibaguzi au kikaburu na kureplace na majina ya kiasili, nilikuwa naongea na mwanataaluma mmoja wa mambo ya historia, nikamuhakikishia south africa ikiwa kwenye position ya kufanya maamuzi kama ya z'bwe itafanya, it maybe 10 years, 20 years, lakini na wenyewe watajaribu kureverse effects za ukoloni na ukaburu, ikiwemo issue ya ardhi. Kuna wanaosema Mandela sold out, kuna wanaosema alichoka kupigana akaamua kusettle for whatever karubu alichoweka mezani, lakini kama unafikiri the fight is over, fikiria tena. The fight for the independence of africa is far from over!