Zimbabwe: The turmoil, reconciliation, and the future!



In August, President Robert Mugabe's neighbours declined to criticise
Zimbabwe's human rights record.




Tutabanana hapa hapa mimi siendi popote labda mni- DITO.

Ni Uzalendo wa hali ya Juu! Wakati hapa tunalia mafisadi wanauza nchi nje-Mugabe awafukuza mafisadi wa ardhi na anarudisha ardhi kwa Mwananchi wake-Je Tanzania tuna uwezo huo...hata kwa fikra?
 


CREDIT: AP

A Zimbabwean beggar poses with wads of Z$200,000 notes in the capital, Harare, where on the black market Z$200,000 is worth one US cent.

You need a container load to go shopping ........
 
Wakati ni ukweli tabia ya Ufisadi ni ya wenye uchu wa kuhodhi.
Ni Ukweli Wazimbabwe hawakuwa wanahodhi mashamba.
Ni Ukweli Waingereza walihodhi mashamba na Wazimbabwe.

Tuache unduminakuwili! Zimbabwe inahitaji ushirikiano wa kila namna kutoka kwa Waafrika wote!
Tukishindwa kusimama kidete na Waafrika wenzetu, Wazimbabwe-nani atafanya hivyo?

Sasa tunalia hela zetu zirudishwe kutoka kwa mafisadi-mafisadi ndio nani?
 
..hivi Mugabe akiwapiga bao wapinzani wake nini kitatokea?

..namkubali Simba Makoni kuliko Tsivangirai, lakini sina uhakika kama ana-support ya kutosha kumshinda Mzee Mugabe.
 
Zimbabwe bans Western observers


Mugabe haambiliki na haoni huruma jinsi raia wake wanavyopata tabu katika maisha ya kila siku. Ipo siku atalipa madhambi yake.
 
Kikwete na Bush washamaliza mazungumzo kuhusu Zimbabwe..kama hamuelewi Kikwete alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa AU kwa shinikizo la marekani.Na hi ni kwasababu ya makubaliano kati ya Blair na Bush kabla ya kuingia madarakani kuwa na yeye atawasaidia Uingereza kupambana na dikteta wa zimbabwe Mugabe,kama vile UK walipomsaidia Bush kupambana na dikteta wa iraqi Sddam Hussein.Kufanya hivyo si rahisi kama Tanzania na CCM wataendelea kumkumbatia Mugabe...kwani makaburu wa Afrika kusini hawajasahau Tanzania ilivyohusika bega kwa bega kwenye ukombozi wa Afrika Kusini.So Tz haikuweza kupuuziwa..lakini bado system ya mzungu ni ile ile "Divide and rule"Sasa Kikwete na Musharaf wa Afrika..ila asitumie nguvu yake ya support kutoka mgharibi vibaya.Kwani hata Mugabe na Saddam waliwahi kuwa vipenzi wao!MUDA HUU NI WA KIKWETE KUUTUMIA NA KUWALETEA MAENDELEO WWANANCHI KAKBLA HAYAJAGEUKA KAMA ILIVYO KWA WENGINEO!
 
Kuna Uwezekano Mkubwa Kuwa Ccm Watakula Pesa Za Bush Halafu Watamgeuka Mugabe!kikwete Ajue La Kufanya!
 
To hell wth Mugabe. Halafu kama JK bado ni kibaraka wa AS imabidi sasa amtose Mugabe la sivyo atakua amelikoroga.

Simba Makoni ni mtu mwenye msimamo anaeweza kuisogeza Zimbabwe mbele.Zimbabweans should drop out the brutal dictator Mugabe
 
Asipomtosa Mugabe Atapoteza Support Ya Magharibi!kibaki Alikubali Yaishe Kwasababu Kikwete Kama African Union Chairman Alikuwa Apeleke Majeshi Kenya Kwa Support Ya Marekani..so The Next Person Is Mugabe!
 
Blair Atafurahi Kweli Kweli..kwani Support Yake Kwa Bush Iraq Italipa!wazungu Itabidi Warudishiwe Maestate Yao huko Zimbabwe Halafu Wazawa Warudi Kwenye Vibanda na vichochoroni huko Harare na kwingineko!Simsupport Mugabe lakini wananchi wa Zimbabwe wasisahauliwe inapokuja kwenye rasilimali za nchi yao!
 

Mimi sijaelewa hapa .Blair afurahi ?
 
Mimi sijaelewa hapa .Blair afurahi?

Waliochukuliwa mashamba yao ni mabepari wengi wao ma tycoon wanaoishi huko ukerewe ambao walienda kulalamika kwa Blair kwamba haki zao za kimsingi kunyanganywa mashamba hayo makubwa zilikiukwa! Shida ya Mugabe ni kwa sababu aliwageuka mabepari hao baada ya kuona support ya wananchi wake inapungua! Hivi sasa hawaendi kwa queen tena...ni kwa prime minister na sirikali yake.

To be specific Tony Blair ambaye anaanza kufundisha chuo kikuu cha Yale na ambaye alikuwa waziri mkuu wa Ukerewe wakati huo alikuwa akitafuta kila namna ili seikali ya Mugabe itengwe kisiasa, Tanzania haikufanya hivyo...ila makubaliano ya Blair kumsupport Bush pia yalihusisha Bush kumsupport Blair! Na ndio maana jina la Mugabe nalo likaanza kupata kipaumbele kwenye hotuba za Bush huku la Saddam likiendelea kupamba moto kwa Mr Blair!

Ni wazi kuwa jukumu la Mugabe sasa kakabidhiwa Kikwete akiwa kama mtopu wa Afrika anayefagiliwa na Marekani! Kikwete alipoenda Nairobi kama mwenyekiti wa umoja wa Afrika mwenye kupewa support na nchi za magharibi ikiwemo marekani, aliwaambia kabisa kuwa analeta jeshi pamoja na ujumbe maalum kutoka kwa Bush kusupport adhma hiyo in any means necessary. Sasa tusubiri tu tuone atafanya nini kuhusu Zimbabwe!

Je atamuondoa Mugabe madarakani ama atamshinikiza uchaguzi usimamiwe na umoja wa Afrika? Ama je watambana kwa namna gani Mugabe? Tusubiri tuone. Najua alisema tetesi za kituo cha jeshi zilikuwa si za kweli kwenye kusaini makubaliano hayo..Hiyo inawezekana! Marekani waweke kituo cha jeshi cha nini wakati tayari wameshaizunguka dunia kwenye bahari na nchi kavu? Kwani hapo Kenya si kuna kituo cha jeshi? Sasa Tanzania cha nini? Hata hivyo bado hatujaelezwa Marekani wao watapata nini kwenye makubaliano hayo! Tatizo ni kwamba wananchi wa kawaida ndio wenye kuteseka huko Zimbabwe!

Usishangae Mugabe akiambiwa na yeye ashirikiane madaraka na Tsvangarai. The situation there is so desperate and the people wants to get over it..and have their lives back on the hopefull side! since the country is well blessed...people should be the first ones to consider when dealing with the well being of the beloved and beautifull people and land of Zimbabwe(former southern Rhodesia)! Sasa kama shida ni Mugabe..hivyo vikwazo si ndio vinawaumiza wananchi? Vikwazo aliwekewa Saddam..waliokuwa wakiteseka ni wananchi wa Iraqi! Na bado wanaoendelea kuteseka ni wananchi pamoja na kufa ni wao!

Vikwazo vyenye kuwaletea shida na mateso wananchi wa kawaida si vyenye kutatua matatizo bali kudidimiza maendelo na kusababisha vifo "MUNGU IBARIKI AFRIKA..NA WATU WAKE! AIEPUSHE NA TAFRANI ZA DUNIA HII AMBAYO HAINA HAKI" na pia ailetee amani na maendeleo..na kuikwamua kutoka kwenye makucha ya mabepari na mafisadi! Atusaidie tuifanye AFRIKA KUWA MOJA!Amen.
 
Wana JF,
Zim si shwari hata kidogo kwa sasa,wapinzani sasa wanaadhibiwa kwellikweli.Zipo taarifa za watu kuteswa wanaompiga mheshimiwa na wameanza kupata ukimbizi ndani ya nchi yao.

Binafsi sikuwa nimewahi kumlaumu mgabe kwa kuwa niliamini matatizo ya wazim yanatokana na hawa wazungu walifikiri wanamkomoa mgabe kumbe wanawatesa wananachi wa zim waso na hatia.Sera ya ardhi kwa ujumla ilikuwa sahihi,na uamzi wa mgabe ulitokana na uingereza kutotimiza makubaliano waliyofanya mwishoni mwa miaka ya sabini kati ya Rhodesia wakati huo na Uingereza

Kwa kuanza kuwatesa wananchi na nafikiri sasa huyu mzee sasa kapoteza mwelekeo
 




MUGABE kitu and please learn more about the ZIM CRICIS kabla ya kurukia conslusion kuwa alikosea

GOOD STARTING POINT NI HAPA:

http://en.wikipedia.org/wiki/Land_reform


ukishaelewa jinsi LAND REFORMS zinavyokenda then ingia hapa:

http://en.wikipedia.org/wiki/Land_reform#Africa


na mzungu8 yoyote yule akikiletea propaganda kuwa MUGABE ni DIKTETA and so on muuloizie kuhusu hili

http://en.wikipedia.org/wiki/Lancaster_House_Agreement




Ukishaelewe kwa nini waingereza waligoma kutekeleza LANCASTER AGREEMENT ndio urudi tujadili ...kwa nini waingereza waligoma kutekeleza hiyo LANCASTER AGREEMENT?

Otherwise tegemea watu kuja humu na ARTICLES ambazo ni anti Mugabe na kwa kuijua JF at least ni watu kama 7 hivi ndio watakuja humu kukupa analysis na si hizi propaganda

 
Ukitaka kujua kuhusu Zimbabwe ni lazima uanzie mbali na kufahamu jinsi Zimbabwe ilivyopata uhuru, jinsi R. mugabe alivyokuja kuwa waziri mkuu jinsi alivyoingia madarakani na jinsi alivyoua wananchi wa Bulawayo kwa father of the nation. Huna sababu ya kwenda Wikipedia kwenye majungu, hata wewe unaweza edit wikipedia.

Kuna Wabongo wengi sana walikaa Zimbabwe baada ya uhuru ulizia utapata majibu. Hii habari ya kulialia nyau na ushabiki wa wezi wa Credit card huwezi kupata ukweli. We are talking about 4 million people who left Zimbabwe, I mean 25% of the population. They don't have food and basic needs because of Dictactor Mugabe.
 
Zimbabwe inflation hits 165,000%




A 10 million Zimbabwe dollar note was
issued this year




Thats life in Zim today!
 


BLISTERING WOUNDS: An opposition supporter waiting for treatment for severe burns at a Harare clinic on Thursday. Civil rights groups in Zimbabwe say security forces and party thugs loyal to President Mugabe have unleashed a campaign of violence against opposition supporters after the disputed elections on March 29.

PHOTO CREDIT: REUTERS

Wengine wamesema huu ni ugomjwa wa ngozi ambao umeanza kuonekana tu baada ya uchaguzi sijui ulikuwa umejificha wapi?



tatizo ni kuwa mugabe anachukiwa na vibaraka wa wakoloni...kwa hiyo wanajitahidi kuonyesha hata picha za watu wenye magonjwa ya ngozi kisha wanamsingizia shujaa bob.
mi kwa hilo haliniingii akilini na ninaungana na wewe.



Dispossessed: Zimbabwean farm workers sit outside the house
they say was burned by police as part of an intimidation
campaign against opponents of Robert Mugabe
 
Why I am not a stooge of the West — Morgan Tsvangirai,

Zimbabwean Opposition Leader


Jk uliomba au uling'ang'ania uwe AU presidal sasa mbona hu-act like presidal wa Africa? Umekuwa bubu kuhusu Zimbabwe una kaupendeleo kwa Mugabe? Tuwavamie kama Comoro mbona hatuoni hicho kimbelembele?
 
Ni kweli kuna wengi humu nadani jf hawamfagilii Mugabe kabisa!
Mimi binafsi niko neutral..sidhani kuwa Mugabe ana nia mbaya na wananchi wake..wanambana ili afuate matakwa yao!
Ni jambo lenye kumake sense pale rais wa nchi anapoona kuna mrundikano wa nguvu kazi kwenye slams za harare na kwingineko wakati maelfu ya heka za ardhi yenye rutuba ikiwa mikononi mwa wazungu wachache!
Huyu jamaa there are some issues we see eye to eye!Jana niliona hotuba yake kupitia runinga yangu na nikaquote"akisema"ZIMBABWE IS NOT FOR SALE AND NO TO COLONIALISM"
Viongozi wetu akiwemo rais wetu ambaye ndiye mwenyekiti wa AU wana ubavu huo?
Je Mugabe angeamua kuwa fisadi na kuiuza nchi si angeweza kukaa madarakani bila usumbufu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…