Zimbabwe au Tarime...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,998
Nimepata barua ifuatayo toka kwa mkazi mmoja wa Tarime, Imani iliyooneshwa kwangu naamini ni imani na heshima kwa forum hii ambapo pamekuwa ni kimbilio la watu wengi wakiamini kuna "vichwa" ambavyo vinaweza kujadili mustakabali wa Taifa letu kwa uhuru na maono bora zaidi kuliko mahali pengine popote. Naileta kama ilivyo:


My Take:

- Kama tulikuwa na waandishi wamekuwa embedded hadi Comoro ipo haya ya ziara nyingine (nakumbuka ziara moja waandishi hawa wakatiwa lupango) ya kundi la waandishi, wana diplomasia kutembelea Tarime kuona kile ambacho serikali ya Rais Kikwete haitaki dunia ione.

- Hadi hivi sasa watu waliouawa Tarime idadi yao ni kubwa zaidi kuliko waliouawa Zimbabwe katika migogoro yao ya ardhi inayoendelea siku za hivi karibuni. Hivyo kabla hatujafikiria kupeleka vikosi vyetu Zimbabwe ipo haja ya vikosi hivyo kwenda na kupiga kambi Tarime kwanza.

- Kwa vile inaonekana kuna tatizo katika kutatua migogoro yetu wenyewe ipo haja ya Rais Kikwete kuomba msaada toka nje ili waje watusaidie Tarime, kwani haiwezekani miaka nenda rudi wananchi wa Tarime waishi katika mazingira ya wasiwasi. Ikibidi kuwa na kituo cha polisi kila mtaa na iwe hivyo, lakini wananchi wa Tarime na wao wanastahili kuishi katika nchi ya "amani, umoja na mshikamano".

- Wabunge wetu waunde msafara hata wa dharura kutembelea na kukutana na wananchi wa Tarime ili kujua kinachoendelea na hatimaye washirikishwe katika kutafuta usuluhishi wa pande hizo zinazogongana. Kwa hili wanaweza kupata msaada wa wataalamu wa sayansi jamii ambao wameshafanya tafiti nyingi tu za matatizo ya Tarime.
 
Nakubaliana nawe kwani mimi binafsi nimewahi kufika eneo hili ila kulikuwa hakuna mapigano kipindi hicho.

Wananchi hawa wanaishi kata ya Mwema ,na kikubwa kati yao ni serikali kuwatenga ,kwani awali walikuwa wanataka kujenga shule ya Sekondari na Mtendaji wa Kata akawaambia kuwa kwa vile wamechagua diwani wa CUF,basi hatawaruhusu na hili lilisababisha mapigano ya mwezi February hii ilitokana na mtendaji huyu kutoka ukoo mmojawapo.

Ngoja nitawapa simu ya huyu Diwani ili muweze kumhoji na pia ntawapatia baadhi ya contacts za independent persons.
 

Kuna reports kuwa Tarime kuna uwezekano wa kuwa na deposit kubwa sana ya madini kuliko ilivyosema mwanzoni. Haya mapigano na kutoelewana kati ya jamii za wakurya na vile yanavyoachwa tu ni dalili mbaya sana... yangu macho tu.

Serikali inaweza kudhani kuwa inamkomesha Wangwe au madiwani wa upinzani lakini implication zake ni kubwa sana.
 
Mwanakijiji,

..tarime,kigoma,ngara, kuna matatizo makubwa ya usalama.

..lakini usije ukashangaa wabunge wa maeneo hayo wakaomba majeshi yapelekwe Zimbabwe na siyo kwenye majimbo yao.

..WATANZANIA NDIVYO TULIVYO!!
 
Kama kawaida wale akina Kolimba wanafanya nini? Tarime kweli muda mwingi huwa siyo salama.

Kwa sasa hivi mtu anayetoa wazo la kupeleka majeshi Zimbabwe kwa tanzania yetu ambayo hata wananchi wanalala njaa(hata ujumbe huo umeonyesha), hawana uwezo wa kunua mafuta, hawana amani mfano mzuri ni zanzibar ambako watu wengine walikuwa wamepoteza hata matumaini ya kuishi nk. Mimi mtu huyo namshangaa na kumuona kuwa amekosa busara.
 

Mkulu Kakindomaster,

Niliitisha mtu aresign effective immediately baada ya kufikia conclusion hii - frustration kuhusu kile kinachoendelea.
 
Mkulu Kakindomaster,

Niliitisha mtu aresign effective immediately baada ya kufikia conclusion hii - frustration kuhusu kile kinachoendelea.

Nafikiri tulisha sema RAIS wetu anafaa kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje, kwa sababu ameifanya hii kazi muda mrefu amejikuta anaipenda kuliko kazi nyingine yoyote.

Mimi nashindwa kujua kabisa kwa nini anatoa umuhimu wa mambo ya nje kuliko wananchi tuliomchagua!
 
Kwani Tanzania tuna waandishi wa habari wa aina gani? Mbona habari kama hii haipewi kipaumbele kabisa? Wameshindwa kwenda kupiga kambi na kuleta full information na video recording? Au wanapenda tu kuandika habari za kusadfisha mafisadi ili wapate pesa ya kula? Njaa isifanye msaliti kazi zenu, fatilieni hii ishu jamani, hawa watu wanahitaji msaada, mnaponyamaza serikali pia inajidai haijui.
 
Sasa Mwanakijiji, what is the next step, inaonekana imani kubwa imeonyeshwa kwa jamvi hili, J tutaendelea kupiga zogo tu au kuna uwezekano wa kupata maelezo hata kutoka kwa kamanda wa polisi wa mkoa huo.
 

Niweka hii habari hapa kwa kina siku za nyuma watu wakaipuuza na hatimaye wakaipeleka kwenye udaku!

PM
 
Can you please MKJJ contact Chacha immedieately and urge him to table this in the ongoing bunge session? I mean this is really scary!

Sorry kwa kukubesha majukumu, lakini sasa ndio hivyo tena ukubwa jalala ndugu yangu!!
 
He tabled it wakati wa kuchangia hoja ya Waziri Mkuu but no body took it seriously! Can some put it here the hansard of that day? Tuone walisemaje?

PM
 
kwa muandishi mmoja mmoja tarime hawawezi kwenda. kwa sababu kunahitaji ulinzi mkubwa kweli kweli. ukipita mitaa watu hawakujui unaweza kukatwa panga kirahisi sana.
wafanyakazi wa serikali walioko tarime karibu wote wanatembea na bastola.

hali ni mbaya mno tarime, na kweli kunahitajika nguvu za jeshi kurejesha amani. lakini viongozi wetu hawajali kwa sababu hii ni siri ya tanzania, nguvu za magharibi hazijui hili na wao wanaishi kwa kujionyeshea kwa magharibi tu.

baada ya masaa kadhaa tusubirini salva atasema tusiongelee hali ya tarime kwa sababu tunaweza kukosa fedha za wahisani.
grrrrrrrrrr
 
Sasa hivi eti hawajui kinachoendelea kule ila wakati wa kuomba kura watafika sijui wataenda kuwapa story gani walah, na sijui nao watawapigia kura? inatisha hii. LuNYUNGU, kandi wabhaki mwana wasu saidia jirani zako kuriport haya
 
Leo mbunge wa Rorya Prof.Sarangi ameitaka serikali kupeleka Jeshi kule JWTZ kwani hali ya usalama ni mbaya sana mpaka Rorya .

Amesema kuwa kama serikali haitapeleka jeshi kuhakikisha kuwa wananchi wa maeneo ya jirani hawawaibii basi wao kama wana Rorya wapo tayari kuifuata mifugo yao huko Kenya japo hakuitaja moja kwa moja alisema nchi jirani.

Hii ni hali ya hatari sana , nimemtafuta sana Diwani wa kata ya Mwema ila mpaka sasa hapatikani kwenye simu na nimetumia contact zangu zote nimeshindwa kumpata.

Nimetuma ujumbe huko kuwa namtafuta na najua kuwa kama ataweza kuupata ujumbe wangu basi ataweza kuwasiliana nami then ntawapa feedback.

Nawatakia kheri...
 
Nahitaji contacts zozote kule kutoka Tarime kwenyewe... I could do a special report on "Tarime - The Bloodshed and the Conspiracy of Silence" , Tarime - Umwagikaji Damu na Njama ya Ukimya.
 



Wakulaumiwa wako wengi. Tumeona pia na watu kama Zitto nao wameunga mkono hizo adventures za JK. Shame on them.
 
Petu Hapa... this is for you.. ndiyo mara ya kwanza nililiangalia suala la Tarime kwa ukaribu zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…