Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,380
- 39,333
Nimepata barua ifuatayo toka kwa mkazi mmoja wa Tarime, Imani iliyooneshwa kwangu naamini ni imani na heshima kwa forum hii ambapo pamekuwa ni kimbilio la watu wengi wakiamini kuna "vichwa" ambavyo vinaweza kujadili mustakabali wa Taifa letu kwa uhuru na maono bora zaidi kuliko mahali pengine popote. Naileta kama ilivyo:
My Take:
- Kama tulikuwa na waandishi wamekuwa embedded hadi Comoro ipo haya ya ziara nyingine (nakumbuka ziara moja waandishi hawa wakatiwa lupango) ya kundi la waandishi, wana diplomasia kutembelea Tarime kuona kile ambacho serikali ya Rais Kikwete haitaki dunia ione.
- Hadi hivi sasa watu waliouawa Tarime idadi yao ni kubwa zaidi kuliko waliouawa Zimbabwe katika migogoro yao ya ardhi inayoendelea siku za hivi karibuni. Hivyo kabla hatujafikiria kupeleka vikosi vyetu Zimbabwe ipo haja ya vikosi hivyo kwenda na kupiga kambi Tarime kwanza.
- Kwa vile inaonekana kuna tatizo katika kutatua migogoro yetu wenyewe ipo haja ya Rais Kikwete kuomba msaada toka nje ili waje watusaidie Tarime, kwani haiwezekani miaka nenda rudi wananchi wa Tarime waishi katika mazingira ya wasiwasi. Ikibidi kuwa na kituo cha polisi kila mtaa na iwe hivyo, lakini wananchi wa Tarime na wao wanastahili kuishi katika nchi ya "amani, umoja na mshikamano".
- Wabunge wetu waunde msafara hata wa dharura kutembelea na kukutana na wananchi wa Tarime ili kujua kinachoendelea na hatimaye washirikishwe katika kutafuta usuluhishi wa pande hizo zinazogongana. Kwa hili wanaweza kupata msaada wa wataalamu wa sayansi jamii ambao wameshafanya tafiti nyingi tu za matatizo ya Tarime.
Dear Mwanakijiji,
Nimechukua hatua ya kukuandikia kwa kuwa ninajua mchango wako katika kusaidia wanyonge wa nchi hii, nimeona kazi unazofanya bila malipo na impact yake pia. Kwa kuwa nina imani na wewe najua hata hili ukitaka kulifatilia na kulianzishia mada ili solution ipatikane inawezekana.
Ndugu yangu kuna vita inaendelea huko tarime kati ya wanchari na warenchoka, najua utakuwa umeshawahi kusikia juu ya migogoro hii inayojitokeza huko mara kwa mara. Kinachoniuma ni kwamba serikali imekaa kimya kabisa utadhani hawajui kinachoendelea. Je ni kweli kwamba wameshindwa ku control hiyo situation? Mbona Comoro majeshi yameenda and now we are talking about Zimbabwe while our own people are killing each others like animals? Nyumba zinachomwa, mashamba yanachomwa, njaa inaingia, watu hawalimi wanaishi kwa wasiwasi, vijana wanaisha wanabaki wazee na watoto, je hata lini serikali itaenda kusaidia. Mimi Navyoandika kauwawa cousin yangu na baba yangu mdogo, lakini ni wengi walioathirika.
Mimi sijui tatizo hasa ni nini, inasemekana ni ardhi or may be there is more than that, je ni kweli serikali imeshindwa kujua chanzo na kutafuta solution? Au ndo tunasubiri ifike kama ile ya watusi na wahutu?
Please naomba tafute information kutoka kwa watu husika may be DC Wa Tarime au viongozi wowote maana hata mimi hapa nilipo sina information nyingi zaidi ya kuletewa taarifa Fulani kauwawa kwenye vita, it hurts, nasikia hata vitoto vidogo vimeanza kujifunza kutengeneza mikuki na upinde, can youi imagine fropm that early age wanaanza kujaa chuki na kisasi, ni taifa gani tunalojenga? Ukipata more information anzisha n mada ili ijadiliwe usikie maoni ya watu wengine to get a solution may be kuna watu wanajua zaidi ya mimi JF. Ila hata Chacha Wangwe anaweza kutoa information. Please help, ndugu zetu wanaisha huko na serikali yetu imeamua kufumba macho.
Thanks in advance brother.