Zilizochakachuliwa ni bora zaidi....

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931

Haya ya Beno Nduru ni aina nyingine ya ufisi..noti mpya zilizotolewa kwa mbwembwe nyingi na BOT kwa maelezo kuwa ni imara na zinalenga kuziondoa sokoni zile zilizokuwa zikitumika kutokana na uchakavu, zimeonyesha wazi kuwa haziwezi kudumu na upya wake zaidi ya miezi sita. Nyingi ya noti hizo zina sura iliyofubaa na zimechakaa baada ya kutumika kwa muda mfupi tu.

Taifa limepoteza tena Pesa zilizotumika kutengenezea noti hizo ambazo ni afadhali kuwa na noti iliyochakachuliwa kuliko noti chafu halali.
 
Attachments

  • IMG00502-20110330-1216.jpg
    IMG00502-20110330-1216.jpg
    94.9 KB · Views: 540
Kwa noti hizi, BOT wametuingiza kwenye choo cha kike kwa mbwembwe zisizo cha chembe ya aibu; sijawahi kuona noti zenye kiwango cha chini cha ubora kama hizi; halafu just imagine - watu walipoanza kulalamika kwamba noti zinachuja rangi, gavana Ndulu(lu) akaibuka na the funniest explanation of the century kwamba hiyo ni sehemu ya security features ya noti hizo!
 
Mkuu, Ndullu kama msanii wa maigizo katika hili. Nadhani wamepigwa changa na waliotengeneza hizi noti...ni aibu tupu noti kufubaa itadhani za mwaka juzi, kama unaona hizo security features zikilaluka hovyo hovyo na ule msitari kuchomoka mithiri ya karatasi iliyomwagiwa maji. Hapo noti haijakumbana na mikiki ya mikono kama ya makonda wa daladala...

Inasikitisha sana mambo yanayofanywa na baadhi ya watendaji wakuu wa nchi hii.
 
Serikali hii kwa vile ni ya wasanii ndio maana huyu Gavana yuko kazini; noti zao mpya hazina ubora wowote kuliko zile za zamani na wametumia hela nyingi za bure kuzitengeneza!! Ndullu anatakiwa afukuzwe kazi kwa ufisadi alioufanya.
 
Nafikiri changamoto nyingine ambayo tunayo wa-tanzania ni jinsi tunavyohifadhi hizo pesa maana utakuta mtu ameikunja note mara nane halafu ikawekwa kwa matiti...mmh...kazi kweli kweli
 
I hope wabunge wataliona hili na kulipigia kelele ili wahusika wa hizi noti uchwara wawajibishwe....wakika kimya serikali ya kishkaji yenyewe inaona poa tu.
 
Serikali hii kwa vile ni ya wasanii ndio maana huyu Gavana yuko kazini; noti zao mpya hazina ubora wowote kuliko zile za zamani na wametumia hela nyingi za bure kuzitengeneza!! Ndullu anatakiwa afukuzwe kazi kwa ufisadi alioufanya.

Mkuu Bulesi, hapo kwenye bold nani wa kumfukuza kazi Ndullu huyu huyu jk au mwingine? Thubutu yake, ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko jk kumfukuza kazi mbadhilifu.
 
Nafikiri changamoto nyingine ambayo tunayo wa-tanzania ni jinsi tunavyohifadhi hizo pesa maana utakuta mtu ameikunja note mara nane halafu ikawekwa kwa matiti...mmh...kazi kweli kweli
Hivi hakuna sheria zinazohusika na namna ya utunzaji wa pesa hizi? Usiombe kukutana na noti iliyotumika na muuza mkaa....
 
ufisadi una sura nyingi, kuchapisha noti mpya ilikuwa gear ya kutafuna deposit ya dollar zilizosalia kwenye accounts pale BOT, probably EPA account as usual.
 
Hivi hakuna sheria zinazohusika na namna ya utunzaji wa pesa hizi? Usiombe kukutana na noti iliyotumika na muuza mkaa....

kisha ikaenda buchani, ikaenda kwenye kwapa za mama ntilie kicha ukaishia kwa konda wa daladala na mwishoni ikaangukia mikononi mwako.
 
Halafu asiseme kuwa inagharimu kiasi cha shilingi 575/= kutengeneza noti ya shilingi 500/=.
 
hizo ni 'disposable' currency, ndio maana zinachakaa baada ya matumizi ya mtu mmoja tu kuzishika, ili zisikae sana kwenye mzunguko.
 
Back
Top Bottom