Asbuhi kulikua na kipindi cha Jambo, ni kipindi cha salamu, zikienda Sambamba na burudani ya mziki, salumu zilikua zinatumwa kwa posta Card.
Mchana: mchana mwema, jioni: Jioni njema. Pia kulikua na kipingi cha mkoa kwa mkoa, kipindi kilichokua kikihusisha maelezo, Tamaduni za wenyeji wa mkoa husika.
Kulikua na Kipindi cha Misakato, Ombi lako, ni vipindi vya burudani ya mziki, kipindi cha zilipendwa ni miziki ya zamani, zaidi hii ambayo hivi sasa tunaita zilipendwa.
Kipindi hicho iliitwa RTD, ikimaanisha RADIO TANZANIA DAR ES ALAAM.
Kipindi hiyo Radio ilikua moja ikiwa na idhaa tatu,
1. Idhaa ya Taifa
2. Idhaa ya Biashara, kama sikosei matangazo yake yalikua yakianza alasiri kwa siku za kazi, siku mapunzi mchana.
3. Idhaa ya nje, hii matangazo yake yalikua yakienda kwa kiingereza.
Magazeti wakati huo, yalikua Matatu, Uhuru gazeti la kila siku, ispokua juma pili, sina uhakika.
Mfanyakazi, lilikua linatoka Juma tano na Juma mosi, pia kulikua na Mzalendo ambalo hutoka juma pili tu.
Magazeti haya yalikua yakichapwa na shirika la shirika la uchapishaji la serikali wakati huo KIUTA.
Hutuba ya rais Nyerere kipindi hicho ikianza, kama kuna mtoto anakohoa, huambiwa akae mbali.
Ila kulikua na maigizo kipindi hicho, iliitwa mchezo wa radio, kipindi cha mahoka, Pwagu na Pwaguzi. Kipindi hicho Taifa lilikua moja, inchi ilikua ya Kizalendo kwelikweli, mtaani huwezi kaa na mtu asiejulikana anuani yake kama hivi sasa, huko vijijini kulima, ilikua lazima kucheza karata, bao, kukaa vijiweni, kunywa pombe asbuhi, mnakamatwa,
Vijiji vilimaliki mashamba yao ya kijiji, yaliitwa Mfumaki,
Maduka ya vijiji maduka yalikua machache sana kipindi hicho.