wakuja town
JF-Expert Member
- Oct 26, 2020
- 898
- 1,342
Mimi natafuata jina la wimbo mmoja nadhan ni wenge bcbg, unaimbwa "baswahili batakingalaba titi, eliiiiii mamaaaa eliiii maamaaa
Aysee ninaujua vizuri mkuu mpaka video yake wamevaa kijeshi jeshi.nadhani ulikuwa unahamasisha mambo ya amani,tatizo jina la wimbo sasa!! Ngoja nifukue fukue nikiupata nitakujuzaMimi natafuata jina la wimbo mmoja nadhan ni wenge bcbg, unaimbwa "baswahili batakingalaba titi, eliiiiii mamaaaa eliiii maamaaa
Haaaa nitafurahi mkuuAysee ninaujua vizuri mkuu mpaka video yake wamevaa kijeshi jeshi.nadhani ulikuwa unahamasisha mambo ya amani,tatizo jina la wimbo sasa!! Ngoja nifukue fukue nikiupata nitakujuza
Marquiz du zaire - Mama Maria Nyerere
Field Marshal Nguza Chimbwiza Vicking na Maestro Ndalla Kasheba wakiongoza kundi zima la Maquiz Du Zaire kumtakia Mama Maria Nyerere maisha ya marefu na mema ya ustaafu kijijini Butiama baada ya kazi ngumu za majukumu ya kama First Lady.
Source: zamani leo
Mkuu bado nasubiriAysee ninaujua vizuri mkuu mpaka video yake wamevaa kijeshi jeshi.nadhani ulikuwa unahamasisha mambo ya amani,tatizo jina la wimbo sasa!! Ngoja nifukue fukue nikiupata nitakujuza
Mkuu Balantanda nahitaji sana wimbo mmoja wa zamani chorus yake inaimbwa hiviPia kuna Washirika Tanzania Stars Band.....
Bendi hii ilikuwa ikimilikiwa na Jumuiya ya Washirika Tanzania na iliundwa na wanamuziki wengi waliojiengua kutoka Orchestra Vijana Jazz,iliundwa mwaka 1989 na ilikuwa ikitumia mtindo wa Watunjatanjata(Watanzania tuondoe njaa Tanzania) na baadae wakajiita Njata one....
Bendi hii ilikuwa ikifanya maonesho yake katika ukumbi wa 92 Hotel pale Sinza Shekilango...Ilikuwa ni bendi kali hasa na ilikuwa ni tishio kwa bendi zilizotamba enzi zake hasa Vijana Jazz...
Bendi hii ilitamba na nyimbo kama Yaliyopita si ndwele(Nimekusamehe lakini sitokusahau),Washirika,Nelson Mandela,Julie,Penzi la ulaghai,Nimebaki nashangaa,Spare tyre,Maeliza,Gubu la wifi zako,Zuhura,Umbea,Watoto wamekuja juu,Masumanda,Kissa,Kayumba na nyingine kali....
Bendi hii iliundwa na wanamuziki wengi waliojiondo Vijana Jazz kama Hamza Kalala 'Komando',Eddy Sheggy,Mhina Panduka 'Toto Tundu',Adam Bakari 'Sauti ya Zege' bila kuwasahau Abdul Salvador 'Father Kidevu',Emma Mkelo 'Lady Champion',Robert Mabrish,Zahir Ally Zorro,Madaraka Morris 'Kiwembe' ,
Baadae mwaka 1991 baadhi ya wanamuziki wakiongozwa na Hamza Kalala na Eddy Sheggy na kwenda kuunda bendi mbili tofauti za Bantu Group Band(wana Kasimbagu Kahabuka) na MCA International(wana Munisandesa) na wengine(Eddy Sheggy na wenzake) walihamia Bima Lee Orch. wana Magnet Tingisha.....Hiii iliifanya Watunjatanjata itetereke kidogo hadi mwaka 1992 ilipompata mtaalam Zahir Ally Zorry ambaye aliifanya ikabaki imara na mtindo wa Watunjatanjata waliouboresha na kuwa Njata One wakiwa na nyimbo kama Gubu la Wifi zako,Maeliza,Zuhura na Umbea