Zile kauli za "Maendeleo Tanzania hayana chama" majukwaani, nahisi ni unafiki na danganya toto tu!

Greataziz

Senior Member
Feb 8, 2018
124
99
*Kaandika Dotto Bulendu, mhadhiri chuo kikuu Saut Mwanza*..

Unafungua vyombo vya habari,unaenda mtandaoni unakutana na kauli zifuatazo kutoka kwa viongozi.

1."Kama mnataka msiendelee kubomolewa mchagueni mgombea wetu"unaanza kujiuliza kwa hiyo mkichagua mpinzani,mnapigwa bomoa bomoa?.

2."Unakutana na kauli nyingine,mimi kwenye mkoa wangu diwani wa upinzani siwezi hata kupokea simu yake na hata kumuona sitaki kabisa na wewe mkuu wa wilaya nitakaye kuona unaongea na diwani wa upinzani jiandae kujieleza",unajiuliza ndiyo tumefika huku?

3."Wewe kama ni mtumishi wa umma na unapingana na chama tawala,jiandae kuondoka" unajiuliza mpaka watumishi wa umma nao?

4."Sisi kule bungeni huwa kuna vikao vya vyama,sisi kikao chetu huwa kinaongozwa na waziri mkuu,huko huwa tunagawana kwanza sisi halafu tunaenda bungeni kupitisha ukiwa upinzani hutapata mgao wa miradi ya maendeleo" unajiuliza hii ndiyo maana ya bunge?

Naomba haya iwe ni kutekeza kwa ulimi na si kuwa ndiyo dhamira ya siasa za sasa!.

Hapa ndipo huwa nafikia hatua nasema,wacha nijifunze zaidi hiki kinachoitwa sayansi ya siasa!.Ndiyo hiki wanachosoma watu chuo kikuu mpaka ngazi ya udaktari?
 
kuna huyu

RC Mnyeti: Siwezi kutoa msaada kwa diwani wa CHADEMA , Labda Ahamie CCM Ndo Ntamsikiliza

07:25
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amewataka madiwani wa vyama vya upinzani kujiunga na CCM ili waweze kushirikiana naye kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama tawala.

Amesema yupo tayari kupokea simu ya diwani wa CCM hata akipigiwa usiku wa manane, ili kumpa msaada lakini si diwani kutoka vyama vya upinzani.

Akizungumza jana Februari 11, 2018 katika mkutano wa hadhara kata ya Haydom wilayani Mbulu, Mnyeti amesema ni vyema madiwani wa Chadema wakajiunga na CCM.

Amesema diwani wa Chadema ni ngumu kufanikisha maendeleo ya wananchi kwa madai kuwa, hakuna ambaye atamsikiliza akiwasilisha hoja zake katika vikao vya halmashauri husika.

"Hata hapa Haydom najua ni ngome ya Chadema hata mwenyekiti wa kijiji namuona ana damu ya CCM, sasa ondokeni huko mje huku tutekeleze ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020 kwa kuleta maendeleo," amesema Mnyeti.

Awali, mkazi wa kata ya Hayderer, John Tluway aliuliza swali kwa mkuu huyo wa mkoa akitaka kujua sababu za mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga kutofika kwenye kata hiyo inayoongozwa na Chadema.

Akijibu swali hilo, Mnyeti amempongeza Mofuga kwa kutokufika kwenye kata hiyo inayoongozwa na Chadema kwa maelezo kuwa diwani wa kata hiyo anapaswa kujiunga na CCM ili kufanikisha maendeleo.

"Mkuu wa wilaya ninakupongeza kwa wewe kutofika kwenye kata hiyo kwani ningepata taarifa umefika mara ya kwanza, mara ya pili na mara ya tatu ningekuwa na mashaka na wewe lakini hongera sana kwa kutokwenda," amesema Mnyeti.

Pia, amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kutekeleza na kufanikisha kwa vitendo ilani ya CCM hata kama hawana kadi ya chama hicho kwani ndicho ambacho kipo madarakani.

"Mtekeleze hayo kwa nia safi, hiyo ni sawa na imani kwani hata kanisani huwezi kusikia padri akimsifu Muhammad na pia kule msikitini imamu huwa hamsifu Yesu," amesema Mnyeti.

Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mbulu, Nasaeli Sulle alimhakikishia Mnyeti kuwa wananchi wa Haydom wamejitambua kuwa walifanya makosa na kuchagua Chadema ila sasa wapo tayari kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM
 
Tutaendelea kuwa masikini milele tukiwa na viongozi kama hawa wajinga wanaowaza ukabila na uchama
 
Uzi fikirishi sana huu. Swali ni, Je, Tutaendelea kuburuzwa hivi hivi nchini kwetu mpaka lini?? Ukiangalia kuwa hatutakaa tuliondoe hili dude kwa kura za kwenye box. Tutaishi kwa kudra za Mungu hadi lini?? Ati watu wananiambia; Iko siku tu! Kwani leo ni half day?? Najiona mpumbavuuu kuliko alivyoniona Benjamin
 
tutaendcelea kuwa masikini mpaka kufa tukiongozwa na ccm hasa wawe na itikadi kama za awamu hii kiongozi anapewa dhamana ya kuongoza wananchi halafu anashika kipaza sauti anaongea mambo ya kipumbavu kama haya.......... nadhani kuna mtu anawatuma waseme haya kwani hao wana chadema ni wasomali ama watanzania kwani hii nchi ni mali ya ccm?
 
kwakweli ifike mahali tuamue moja kama ni mbwai ni mbwai kiongozi anasimama anasema ujinga huu mnampopoa mawe papo hapo watakoma
 
*Kaandika Dotto Bulendu, mhadhiri chuo kikuu Saut Mwanza*..

Unafungua vyombo vya habari,unaenda mtandaoni unakutana na kauli zifuatazo kutoka kwa viongozi.

1."Kama mnataka msiendelee kubomolewa mchagueni mgombea wetu"unaanza kujiuliza kwa hiyo mkichagua mpinzani,mnapigwa bomoa bomoa?.

2."Unakutana na kauli nyingine,mimi kwenye mkoa wangu diwani wa upinzani siwezi hata kupokea simu yake na hata kumuona sitaki kabisa na wewe mkuu wa wilaya nitakaye kuona unaongea na diwani wa upinzani jiandae kujieleza",unajiuliza ndiyo tumefika huku?

3."Wewe kama ni mtumishi wa umma na unapingana na chama tawala,jiandae kuondoka" unajiuliza mpaka watumishi wa umma nao?

4."Sisi kule bungeni huwa kuna vikao vya vyama,sisi kikao chetu huwa kinaongozwa na waziri mkuu,huko huwa tunagawana kwanza sisi halafu tunaenda bungeni kupitisha ukiwa upinzani hutapata mgao wa miradi ya maendeleo" unajiuliza hii ndiyo maana ya bunge?

Naomba haya iwe ni kutekeza kwa ulimi na si kuwa ndiyo dhamira ya siasa za sasa!.

Hapa ndipo huwa nafikia hatua nasema,wacha nijifunze zaidi hiki kinachoitwa sayansi ya siasa!.Ndiyo hiki wanachosoma watu chuo kikuu mpaka ngazi ya udaktari?
Chadema inawapa headache sana ccm, yaani watakufa kwa presha.

Kadiri wanavyozidi kupanua chudi dhidi ya chadema ndivyo wananchi wanazidi kuitamani chadema.
 
tutaendcelea kuwa masikini mpaka kufa tukiongozwa na ccm hasa wawe na itikadi kama za awamu hii kiongozi anapewa dhamana ya kuongoza wananchi halafu anashika kipaza sauti anaongea mambo ya kipumbavu kama haya.......... nadhani kuna mtu anawatuma waseme haya kwani hao wana chadema ni wasomali ama watanzania kwani hii nchi ni mali ya ccm?
Ccm wamepaniki hasa kila wanapoona upinzani unazidi kushamiri licha ya kutumia gharama lubwa hadi ya kumwaga damy bila mafanikio.
 
Uzi fikirishi sana huu. Swali ni, Je, Tutaendelea kuburuzwa hivi hivi nchini kwetu mpaka lini?? Ukiangalia kuwa hatutakaa tuliondoe hili dude kwa kura za kwenye box. Tutaishi kwa kudra za Mungu hadi lini?? Ati watu wananiambia; Iko siku tu! Kwani leo ni half day?? Najiona mpumbavuuu kuliko alivyoniona Benjamin
Mimi natamani hata leo tulianzishe umoja ni nguvu peke Yangu sitaweza lets stand For This upumbavu
 
tutaendcelea kuwa masikini mpaka kufa tukiongozwa na ccm hasa wawe na itikadi kama za awamu hii kiongozi anapewa dhamana ya kuongoza wananchi halafu anashika kipaza sauti anaongea mambo ya kipumbavu kama haya.......... nadhani kuna mtu anawatuma waseme haya kwani hao wana chadema ni wasomali ama watanzania kwani hii nchi ni mali ya ccm?
Ndio Hapo sasa baadhi wakuu wa mikoa wanajigeuza miungu watu kwamba hawatakufa wao hii nchi ni mali yao
 
Back
Top Bottom