Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Wanaume hutoka nje kwa sababu ambazo zinatofautiana na zile za wanawake. Wanaume hutoka nje kwa sababu ambazo zinaonekana wazi kwamba hazina mashiko, angalau kwa nje.
Kama ilivyo kwa wanawake, sababu za kutoka nje kwa wanaume ni nyingi pia, lakini nitazitaja baadhi ambazo ndizo zenye kujitokeza sana kwenye mazingira yetu hapa nchini.
Kama ilivyo kwa wanawake, sababu za kutoka nje kwa wanaume ni nyingi pia, lakini nitazitaja baadhi ambazo ndizo zenye kujitokeza sana kwenye mazingira yetu hapa nchini.
- Kuridhisha mwili- Kimaumbuile, inaelezwa kwamba, mwanaume hahusishi tendo la ndoa na kumpenda mtu. Kwa mwanaume kupenda ni jambo moja na tendo la ndoa ni jambo lingine, tofauti na wanawake ambao huunganisha kupenda na tendo la ndoa. Kwa mfano, yale mazingira ambayo Waingereza huyaita one night stand. Mwanaume anakwenda semina , anajikuta ameshawishika kwa mwanamke mwingine, wanakutana kimwili na biashara inaishia hapo hapo. Hakuna kupenda, kuna kutamani na kuonja.
- Kupenda kubadilisha mboga- hapo ndipo ile nadharia ya kwamba mwanaume hawezi kula mboga moja inapochipukia . wanawake walio wengi na hata wanaume pia huamini kwamba , mwanaume hawezi kuendelea kufanya mapenzi na mtu mmoja. Dhana hii haina ukweli , lakini kwa kiasi fulani ina ukweli kutegemea malezi na mazingira aliyokulia mtu na anamoishi na watu anaofuatana nao. Kuna idadi ya kutosha sana ya wanaume ambao wanaona kubadili wanawake ni jambo lisiloweza kuepukika.
- Udadisi kwa wanawake fulani-Wanaume wanatabia ya kujiuliza maswali kuhusu aina fulani ya wanawake. Sio tu suala la tamaa, bali ni kutaka kujua zaidi kuhusu umbile fulani, kuhusu mwanamke wa aina fulani alivyo kitandani. Kwa kiasi fulani wanwake nao wana tatizo hili, lakini sio kubwa kama la wanaume.
- Kupunguza hisia za kutojiamini-Mtu ambaye hajiamini anaweza kujaribu kujificha au kutafuta kujipandisha, kupitia pombe, fedha, magari ya kifahari na vitu vingine vya kifahari. Lakini pia anaweza kujihusisha na ngono za hovyo, katika kujaribu kutafuta nafuu
- Kuna maradhi ya kupenda ngono kupita kiasi-kama ilivyo kwa matatizo mengine ya kimwili na ya kihisia, kuna yale ambayo ni sugu. Kuna wanaume na wanawake ambao hutoka nje ya ndoa zao kwa sababu hawawezi kudhibiti hisia zao za kupenda ngono. Haifahamiki usugu huu wa kupenda ngono kupita kiasi husababishwa na nini, lakini ukweli ni kwamba wapo watu wenye usugu huu. Hapa ndipo unakuta mwanaume kamaliza jirani zake, wasichana wa kazi, ndugu wa mke na mwanamke yeyote atakayemkalia vibaya.
- Kutoridhishwa ndani-Kama nilivyosema awali, mwanaume huchukulia kufanya mapenzi kama kitu kimoja na kupenda kama kitu kingine. Anapojikuta haridhishwi na mkewe, huamua kwenda kutafuta ridhiko nje, anaweza kuwa bado anampenda mkewe, lakini mwili wake haujaridhishwa na kwa sababu kupenda kwa upande wake hakuna maana sawa na tendo la ndoa, hutafuta mwili mwingine.