Zijue sababu za wanaume hutoka nje ya ndoa zao…….

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
Wanaume hutoka nje kwa sababu ambazo zinatofautiana na zile za wanawake. Wanaume hutoka nje kwa sababu ambazo zinaonekana wazi kwamba hazina mashiko, angalau kwa nje.
Kama ilivyo kwa wanawake, sababu za kutoka nje kwa wanaume ni nyingi pia, lakini nitazitaja baadhi ambazo ndizo zenye kujitokeza sana kwenye mazingira yetu hapa nchini.
  1. Kuridhisha mwili- Kimaumbuile, inaelezwa kwamba, mwanaume hahusishi tendo la ndoa na kumpenda mtu. Kwa mwanaume kupenda ni jambo moja na tendo la ndoa ni jambo lingine, tofauti na wanawake ambao huunganisha kupenda na tendo la ndoa. Kwa mfano, yale mazingira ambayo Waingereza huyaita one night stand. Mwanaume anakwenda semina , anajikuta ameshawishika kwa mwanamke mwingine, wanakutana kimwili na biashara inaishia hapo hapo. Hakuna kupenda, kuna kutamani na kuonja.
  2. Kupenda kubadilisha mboga- hapo ndipo ile nadharia ya kwamba mwanaume hawezi ‘kula mboga moja’ inapochipukia . wanawake walio wengi na hata wanaume pia huamini kwamba , mwanaume hawezi kuendelea kufanya mapenzi na mtu mmoja. Dhana hii haina ukweli , lakini kwa kiasi fulani ina ukweli kutegemea malezi na mazingira aliyokulia mtu na anamoishi na watu anaofuatana nao. Kuna idadi ya kutosha sana ya wanaume ambao wanaona kubadili wanawake ni jambo lisiloweza kuepukika.
  3. Udadisi kwa wanawake fulani-Wanaume wanatabia ya kujiuliza maswali kuhusu aina fulani ya wanawake. Sio tu suala la tamaa, bali ni kutaka kujua zaidi kuhusu umbile fulani, kuhusu mwanamke wa aina fulani alivyo kitandani. Kwa kiasi fulani wanwake nao wana tatizo hili, lakini sio kubwa kama la wanaume.
  4. Kupunguza hisia za kutojiamini-Mtu ambaye hajiamini anaweza kujaribu kujificha au kutafuta kujipandisha, kupitia pombe, fedha, magari ya kifahari na vitu vingine vya kifahari. Lakini pia anaweza kujihusisha na ngono za hovyo, katika kujaribu kutafuta nafuu
  5. Kuna maradhi ya kupenda ngono kupita kiasi-kama ilivyo kwa matatizo mengine ya kimwili na ya kihisia, kuna yale ambayo ni sugu. Kuna wanaume na wanawake ambao hutoka nje ya ndoa zao kwa sababu hawawezi kudhibiti hisia zao za kupenda ngono. Haifahamiki usugu huu wa kupenda ngono kupita kiasi husababishwa na nini, lakini ukweli ni kwamba wapo watu wenye usugu huu. Hapa ndipo unakuta mwanaume kamaliza jirani zake, wasichana wa kazi, ndugu wa mke na mwanamke yeyote atakayemkalia vibaya.
  6. Kutoridhishwa ndani-Kama nilivyosema awali, mwanaume huchukulia kufanya mapenzi kama kitu kimoja na kupenda kama kitu kingine. Anapojikuta haridhishwi na mkewe, huamua kwenda kutafuta ridhiko nje, anaweza kuwa bado anampenda mkewe, lakini mwili wake haujaridhishwa na kwa sababu kupenda kwa upande wake hakuna maana sawa na tendo la ndoa, hutafuta mwili mwingine.
 
sawaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

so ndo jstifications za kuendelea na MIPANGO YA KANDO?

Hilo ni angalizo, ambalo litawasaidia wanawake kuwajua waume zao kwa urahisi......... ukiona mumeo ni mzinzi,basi jua kwamba kuna moja ya sababu nilizozitaja hapo inahusika...........................
 
Nadharia zako zinafanana na ambazo nimewahi kuzisoma kwenye magezi ya marehemu baba yangu,haya ni magazet ya JITAMBUE...ni kweli umewahi kuyapitia?
 
Sababu zako ni za kweli, zina logic. Ila swala hapo ni kujizuia maana hizo zote tukiziendekeza hatutafika mbali.
 
Nadharia zako zinafanana na ambazo nimewahi kuzisoma kwenye magezi ya marehemu baba yangu,haya ni magazet ya JITAMBUE...ni kweli umewahi kuyapitia?

Ni kweli, kwani nami nilikuwa mmoja wa waandishi waandamizi wa gazeti hilo...........kwa huwa baba yako ameshauacha mwili, sina budi kuendeleza kile tulichokuwa tukikifanya.......... habari hii waweza kuipata pia katika kitabu cha Mapenzi kuchipua na kunyauka, hapa nimejaribu kuandika kwa muhtasari sana, lakini katika kitabu hicho, sababu hizo zimeelezewa kwa kirefu zaidi..........
 
Nadharia zako zinafanana na ambazo nimewahi kuzisoma kwenye magezi ya marehemu baba yangu,haya ni magazet ya JITAMBUE...ni kweli umewahi kuyapitia?
Usinambie Munga aliacha mtoto mkubwa hivi
 
Usinambie Munga aliacha mtoto mkubwa hivi

Usishangae kaka....kuna watoto wa dada zake, kaka zake na labda wajomba zake na shangazi zake............ Pia hata wale waliokuwa wanafunzi wake hupenda kujitambulisha kama watoto wa Munga Tehenan.............. Tuko wengi sana mpaka huko mikoani........
 
Usishangae kaka....kuna watoto wa dada zake, kaka zake na labda wajomba zake na shangazi zake............ Pia hata wale waliokuwa wanafunzi wake hupenda kujitambulisha kama watoto wa Munga Tehenan.............. Tuko wengi sana mpaka huko mikoani........

Ni kweli mkuu, hata mimi ni mmoja wa wanafunzi wake na hupenda kujitambulisha kama mwanae pia...........vipi Bwana Mtambuzi mbona hatuonani bana.......Je weekend hii utakuwepo pale kwa Dr. John?
 
Mkuu lakini hiyo number 6 si iko both ways au?:confused3:

Ngoja niinukuu hapa..........
"6. Kutoridhishwa ndani-Kama nilivyosema awali, mwanaume huchukulia kufanya mapenzi kama kitu kimoja na kupenda kama kitu kingine. Anapojikuta haridhishwi na mkewe, huamua kwenda kutafuta ridhiko nje, anaweza kuwa bado anampenda mkewe, lakini mwili wake haujaridhishwa na kwa sababu kupenda kwa upande wake hakuna maana sawa na tendo la ndoa, hutafuta mwili mwingine."

Hii namba sita, nitawatetea wanawake.... mara nyingi wanawake huwavumilia waume zao ukilinganisha na wanaume, kama nilivyobainisha hapo namba 1. kwamba wanaume kwao tendo la ndoa ni kitu kingine na upendo ni kitu kingine, tofauti na wanawake ambao kwao upendo na tendo la ndoa huenda sambamba. Kama itatokea mwanamke akatoka nje kutokana na udhaifu wa mumewe, basi ujue hapo hakuna upendo. lakini kama anampenda mumewe kwa dhati kabisa, kamwe hataweza kutoka nje ya ndoa.
 
Ni kweli mkuu, hata mimi ni mmoja wa wanafunzi wake na hupenda kujitambulisha kama mwanae pia...........vipi Bwana Mtambuzi mbona hatuonani bana.......Je weekend hii utakuwepo pale kwa Dr. John?

Nitakuwa nje ya mji..........Natarajia kwenda Pemba Mnazi huko Kimbiji............
 
Hizo zote hapo ni kazi za shetani tu.
Yesu ni dawa ya yote.
 
wanaume kwao tendo la ndoa ni kitu kingine na upendo ni kitu kingine, tofauti na wanawake ambao kwao upendo na tendo la ndoa huenda sambamba. Kama itatokea mwanamke akatoka nje kutokana na udhaifu wa mumewe, basi ujue hapo hakuna upendo. lakini kama anampenda mumewe kwa dhati kabisa, kamwe hataweza kutoka nje ya ndoa.
Inadhaniwa na watu wengi kwamba ni lazima mwanamke awe na hisia za kimapenzi kwa mwanaume afanye tendo la ndoa naye, lakini sijawahi kupata kipimo chochote kinachothibithisha hii stereotype ina ukweli. Bali nimeshawahi kusoma wanawake wakikiri hawafanyi tendo hilo na watu ambao wana mapenzi kwao tu. Unless wanawake hao wote ni waongo, inamaanisha uwezo wa kutofautisha mahaba na tamaa sio wanaume tu walio nao. Basi, nafikiri inawezekana kabisa mwanamke kutoka nje ya ndoa kwa sababu haridhishwi kitandani wakati anampenda mume wake, ingawa inaonekana wanaume hutoka nje kwa sababu hilo sana kuliko wanawake.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom