Zijue sababu za Benjamin Mkapa kumuunga mkono Lowassa

John Okello

JF-Expert Member
Sep 24, 2014
459
207
Ikiwa Dunia imesimama kwa mshutuko wa kumpoteza kiongozi shupavu Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Satta kilichotokea London mapema wiki hii, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amekaririwa na kituo cha lunginga CITIZEN nchini Kenya kwa njia ya simu akihojiwa maswali mbali mbali baada ya kifo cha Satta, Katika mahojiano yake siku sita OKELLO kupata tafakuri ya Zaidi ya masaa 30 hadi sasa na kudhubutu kusema Lowassa ameungwa Mkono na Mkapa kwa maslahi ya Taifa , chama na Serikali. Zijue sababu za Mkapa kumuunga mkono Lowassa katika Tafsiri ya mahojiano yake na kituo tajwa.

1. EDWARD LOWASSA ANAUZIKA KWA WANANCHI

Rais Mkapa aliangazia wasifu wa Lowassa bila shaka na kukiri ndie anaeuzika akiangalia utendaji na uchapakazi wa Lowassa na ndioa maana alinukuliwa aisema,"Chama kama chama lazima muwe na mtu anayeuzika na kukubalika katika jamii kwa utendaji wake, haiba yake, wasifu wake (ndani ya Chama na Serikali) lakini vile vile ushawishi wake.." ambae bila shaka ni Lowassa.

2. VIJANA WAJITOKEZE ILA NI WAKATI WA LOWASSA.
Hapa Mheshimiwa rais Mstaafu alionyesha kuwa chama kina kuza demokrasia pia na hivyo hazina ya vijana haipaswi kupuuzwa ila huu ni wa kati wa Lowassa na ndio maana hakusita kumtaja Lowassa pale alipo jitokeza 1995 na sasa ni wakati wake. Hivyo alisema "...Haya mambo ya umri na kadhalika sisi hatukutazama wakati huo ila si dhambi vijana KUJITOKEZA manake hata wakati wangu Rais wa sasa Mhe. Kikwete na kina Lowassa walijitokeza na LEO unaona Kikwete ndiye Rais" akimaanisha vijana wajitokeze ila Lowassa ndie Rais AJAYE.

3. AKIRI LOWASSA HAKUNA WA KUMZUIA NDANI YA CHAMA

"...nikuhakikishie hata kama mimi Benjamin Mkapa siko na Kikwete mwisho wa siku wanachama ndio watakaosema wewe hutaki ila sisi tuachie huyo huyo...Na hayo yalijitokeza mwaka 2005 watu walimtaka Mhe Kikwete sasa mimi kuwa Mwenyekiti wa Chama hakunipi Mandate ya kushindana na walio wengi na mliona alishinda kwa asilimia kubwa kweli kweli.." HIVYO ni wazi hata Rais Jakaya hayuko kwa ajili ya kumzuia Lowassa bali kutimiza Demokrasia.


4. AONYA MAKUNDI YA URAIS NDANI YA CHAMA YANAYOMCHAFUA BILA SABABU

Mheshimiwa Mkapa alirejea kauli ya Edward Lowassa February 7 ,2008 alipoonya wanasiasa kupakaziana siasa chafu hivyo nae alionya kwa kusema "Hivyo CCM Ina taratibu zake na wanajua nani anafaa manake siasa hizi...tuhuma zingine za kipuuzi kweli kweli...sasa mkiendekeza tuhuma mwishowe mnakuta mnabaki bila chama na kwenye siasa mkianza kushutumiana hakuna wa kusimama"


5. LOWASSA NI TUMAINI LA WENGI NA CHAGUO LA WENGI

Amekishauri chama kuwa Lowassa ni tumaini la wengi hivyo cha kama chama wao watawekeza kwake na ndipo alipo yanena haya "Hakuna chama duniani ambacho kinaona kabisa fulani atatusaidia halafu kimwache -hakuna. Manake huko ni kukiua Chama...Naamini ndivyo ilivyo hata mpaka sasa tafiti zimefanyika na naamini wamesikia watu wakisema wanamtaka nani…wakati wangu mimi mgombea alikuwa amesha tungiwa nyimbo na watu mbali mbali wenye mapenzi nae. Hivyo labda hata sasa yawezekana kuwa hivyo…washwahili walisema nyota njema huonekana asubuhi"

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA ,….SAFARI YA MATUMAINI KUELEKEA 2015.
 
wewe tu ndo hutaki kuiona hiyo ''collocation'' greencty. maana maneno hayo Mkapa kayatoa alipokua akihojiwa na ktuo cha televsheni cha Citizen kuhusana na kio cha rais Satta. Na kwa kweli alchosema kuhusiana na ndugu Lowassa ni kitu ambacho ni hakika. Lowassa amekua ni gumzo kwa watanzania wakimtaka agombee urais maana wanatumaini naye kwamba atawavusha kutoka katika hali ya sasa ya hali mbaya ya kiuchumi,elimu mbovu,ukosefu wa ajira,tatizo maji na afyamaana ote huo wana uzoefu naye wa mambo makbwa aliyoyafanya katika nyadhifa alizowahi kushika
 
Last edited by a moderator:
Acha porojo Baba,chaguo la Mkapa ni Magufuli.Fuatilia ni waziri gani pekee aliyekabidhiwa vitabu vya hotuba za Mkapa baada ya JK.
 
Acha porojo Baba,chaguo la Mkapa ni Magufuli.Fuatilia ni waziri gani pekee aliyekabidhiwa vitabu vya hotuba za Mkapa baada ya JK.

Wew ndio unae nena hayo ila Mkapa 2005 alipowataja askari wake Wa miamvuli Alitajwa Kikwete na Lowassa ...historia ilijirudia pia Jana
 
aloo ngoja aje chabruma mtot wa nje a.ka.a mr makondakta na lizabon, nslishasema hakuna wa kumzuia lowassa ndan ya ccm kuwa rais, nawashangaa hwa waswahil na mtot wa mkulima wanavyojiangaisha
 
Mkapa ni mkweli sana,kwa nafasi aliyonayo kama senior party man ameendelea kukubali Lowassa Kikwete Duo ile iliomshinda yeye na chaguo lake 2005,unlike wale wanasiasa wakongwe lakini wameendekeza Makundi bila kujali kelele na sauti kuu inayopazwa huku mitaani na majority ya wananchi wa kawaida.
 
Mkapa ni mkweli sana,kwa nafasi aliyonayo kama senior party man ameendelea kukubali Lowassa Kikwete Duo ile iliomshinda yeye na chaguo lake 2005,unlike wale wanasiasa wakongwe lakini wameendekeza Makundi bila kujali kelele na sauti kuu inayopazwa huku mitaani na majority ya wananchi wa kawaida.

Vyema Mkuu umenena
 
Jamani Okelo twashukuru unatuletea mambo mengi sana ya Lowasa. Plz ebu tujuze ya kweli kabisa kuhusu lowasa na richmond. Ili nasi tuangalie pande zote za shilingi. inawezekana ilikuwa propaganda au kweli.

Wakati ukifika nitakuletea ...huwa siandiki porojo so nipo katika tafiti tusubiri majibu.... karibu huku kwa wazalendo tunao dai Uhuru...
 
aloo ngoja aje chabruma mtot wa nje a.ka.a mr makondakta na lizabon, nslishasema hakuna wa kumzuia lowassa ndan ya ccm kuwa rais, nawashangaa hwa waswahil na mtot wa mkulima wanavyojiangaisha

Anasubiri bosi amuagize....Hahaha
 
Back
Top Bottom