Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,185
- 10,664
Habarini za asubuhi wanaJF, natumaini mko wazma sana na Pole ziende kwa wagonjwa. Leo Naomba nilete uzi huu wenye mada ya magereza matano duniani yenye hatari yake kwenye uzuri wa miundombinu pamoja na uongozi wake. (Nisameheni kwa kutumia neno “hatari” nimetumia kunogesha tu yalivyo mazuri ila sio kwa maana ya kuwa kuna hatari ndani yake.
Karibu...,
Mwaka 2017 mtoto wa shangazi aliwekwa selo pale Ukonga alikula nyundo ya Miaka 2
Nilikuwa nakwenda kumpa hai ingawa Shangazi alikataa kumtolea dhamana wala hata nia ya kumtafutia mwanasheria ili dogo atoke.
Niliona mazingira ya gereza la Ukonga nikajisemea duuh Mbona Afrika utajuta kwanini umeingia kumi na nane za sheria
Katika kupita kwangu kwenye vitabu mbalimbali nikakutana na kitabu kimoja kinachambua magereza mbalimbali duniani yenye sifa mbaya na nzuri; magereza kutoka Mexico, Colombia na Marekani zina sifa mbaya ila kutoka nchi za Scandinavia huwa zina sifa njema sana.
Ingawa dhana ya uwepo wa magereza ni kwa nia ya kurekebisha tabia za wafungwa, lakini mazingira sio rafiki Kabisa katika magereza mengi. Baadhi ya magereza kuna uhalifu Mkubwa sana. Huku ndo kuna magenge yenye bifu balaa; yaani unaweza kudhani kuna watu wameenda huko kutawala.
Lakini kuna magereza ni masafi na ni zaidi ya kuishi kwenye hali ya uchafu na kufanya fujo. Mataifa ya Scandinavia pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya zina magereza ambazo Kwa Hakika hazina bughudha Kabsa.
Orodha inaweza kuwa tofauti na mawazo ya wengi ila kwa uchambuzi wangu naona ni vyema mkaongeza zaidi ikiwezekana.
1. Gereza la Bastoy , Norway
Ni gereza linalopatikana kwenye kisiwa cha Bastoy huko Oslofjord, na huweka wafungwa wasiozidi Mia moja tu. Ndani humo kuna huduma hizi; kucheza tennis, kuendesha farasi, kuvua samaki pamoja na kutalii.
Gereza hili hutumika kuwaweka wafungwa kwa muda mfupi tu na huwa na ulinzi wa wastani. Na Wakati Mwingine wafungwa husahau kama wamefungwa.
Ndani ya gereza hili kuna sehemu ndogo ya shamba ambalo wafungwa hufanya kazi ambayo sio kazi ngumu kama magereza mengine haswa barani Afrika
ikitokea umefungwa humu basi unaweza kutamani kuendelea kukaa.
Hakuna rekodi ya mtu kutoroka wala kufanya fujo ndani ya gereza hilo
. Hili ndo gereza namba moja kwa wala bata Ingawa ni mfungwa.
Muonekano wa juu wa eneo la gereza la bastoy.
2. HMP Addiewell, Scotland
Ni gereza lililotengenezwa kuwa kituo cha mafunzo. Ni gereza linalotoa masaa arobaini ndani ya wiki moja kwa ajili ya wafungwa kujifunza maarifa yenye kujenga maisha yao; huku ikiwa ni mpango wa kuwasaidia wafungwa kuwa raia Wema wako malizia nyundo zao.
Huku likiwa na wafungwa wasiozidi Mia sita, programu mbalimbali huanzishwa ili kuruhusu wafungwa kujifunza zaidi.
Kwa muonekano wa nje
Ndani ya vyumba
Ndani ya gereza hili wafungwa huweza kujifunza maarifa mbalimbali kama vile; ufundi wa umeme, magari na mambo mengi yote hii ili tu warudi kitaa wakiwa na kitu kichwani.
3. Otago Corrections Facility, New Zealand
Ni moja kati ya magereza yenye ulinzi mkali sana ni ngumu kutoroka bila mitambo ya CCTV kukuacha salama.
Mbali na hivyo, gereza hili hutoa nafasi kubwa ya wafungwa kuishi maisha mazuri, kuanzia kuwa na chumba kizuri pamoja na fursa ya kuongea ujuzi na maarifa. Kuna darasa maalumu kuhusu ukandarasi wa majengo pamoja na umeme. Pia mafunzo ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa pamoja na Upishi.
Uongozi wa magereza hii huwa na dhamira kubwa ya kutengeneza raia Wema wakitoka gereza Hapo.
4. Justice Center Leoben, Austria
Hili ni gereza maalumu kwa ajili ya wafungwa wasio na makosa ya kihalifu. Ndani humu kila mfungwa huwa na chumba chake, choo cha ndani pamoja na jiko na televisheni.
Nje kuna gym center iliyo na kila kitu, uwanja wa kucheza kikapu pamoja na sehemu ya kujiburudisha.
5. Aranjuez Prison, Spain
Ingawa magereza nyingi ndo huwa chanzo cha familia kuvunjika, basi gereza hili kutoka uhispania limekuwa ndo gereza lenye kuruhusu watoto wachanga kuishi na wazazi wao mpaka Miaka mitano kisha utolewa nje kulelewa na ndugu.
Kuna miundombinu tosha kwa wazazi kufurahia wakati na Watoto wao. Kuta za vyumba huchorwa katuni mbalimbali na huwepo na huduma zote muhimu kwa ajili ya wazazi na mtoto.
Bonus:
Champ-Dollon Prison, Switzerland
Gereza kutoka taifa la Uswisi, ambalo mwanzoni lilikutwa na sifa mbaya ya kuwa na wafungwa wengi.
Gereza lilifanyiwa marekebisho kadha wa kadha na kubadilisha muonekano wake.
Kwa sasa linaruhusu watu watatu kulala ndani ya chumba kikubwa kukiwa na bafu ndani.
Msosi wake huandaliwa na wapishi na huwa na vyakula muhimu kwa afya ya mfungwa mmoja mpaka Mwingine. Hata kwa wale wasiotumia baadhi ya vyakula upewa uzito wao.
Lengo la magereza linatofautiana sana kwa fikra za mtu na mtu.
Naomba niishie hapa kwa leo.
@Mshana Jr @Malcom_X @Madame B
Karibu...,
Mwaka 2017 mtoto wa shangazi aliwekwa selo pale Ukonga alikula nyundo ya Miaka 2
Nilikuwa nakwenda kumpa hai ingawa Shangazi alikataa kumtolea dhamana wala hata nia ya kumtafutia mwanasheria ili dogo atoke.Niliona mazingira ya gereza la Ukonga nikajisemea duuh Mbona Afrika utajuta kwanini umeingia kumi na nane za sheria

Katika kupita kwangu kwenye vitabu mbalimbali nikakutana na kitabu kimoja kinachambua magereza mbalimbali duniani yenye sifa mbaya na nzuri; magereza kutoka Mexico, Colombia na Marekani zina sifa mbaya ila kutoka nchi za Scandinavia huwa zina sifa njema sana.
Ingawa dhana ya uwepo wa magereza ni kwa nia ya kurekebisha tabia za wafungwa, lakini mazingira sio rafiki Kabisa katika magereza mengi. Baadhi ya magereza kuna uhalifu Mkubwa sana. Huku ndo kuna magenge yenye bifu balaa; yaani unaweza kudhani kuna watu wameenda huko kutawala.
Lakini kuna magereza ni masafi na ni zaidi ya kuishi kwenye hali ya uchafu na kufanya fujo. Mataifa ya Scandinavia pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya zina magereza ambazo Kwa Hakika hazina bughudha Kabsa.
Orodha inaweza kuwa tofauti na mawazo ya wengi ila kwa uchambuzi wangu naona ni vyema mkaongeza zaidi ikiwezekana.
1. Gereza la Bastoy , Norway

Ni gereza linalopatikana kwenye kisiwa cha Bastoy huko Oslofjord, na huweka wafungwa wasiozidi Mia moja tu. Ndani humo kuna huduma hizi; kucheza tennis, kuendesha farasi, kuvua samaki pamoja na kutalii.
Gereza hili hutumika kuwaweka wafungwa kwa muda mfupi tu na huwa na ulinzi wa wastani. Na Wakati Mwingine wafungwa husahau kama wamefungwa.
Ndani ya gereza hili kuna sehemu ndogo ya shamba ambalo wafungwa hufanya kazi ambayo sio kazi ngumu kama magereza mengine haswa barani Afrika
ikitokea umefungwa humu basi unaweza kutamani kuendelea kukaa.Hakuna rekodi ya mtu kutoroka wala kufanya fujo ndani ya gereza hilo
. Hili ndo gereza namba moja kwa wala bata Ingawa ni mfungwa.2. HMP Addiewell, Scotland
Ni gereza lililotengenezwa kuwa kituo cha mafunzo. Ni gereza linalotoa masaa arobaini ndani ya wiki moja kwa ajili ya wafungwa kujifunza maarifa yenye kujenga maisha yao; huku ikiwa ni mpango wa kuwasaidia wafungwa kuwa raia Wema wako malizia nyundo zao.
Huku likiwa na wafungwa wasiozidi Mia sita, programu mbalimbali huanzishwa ili kuruhusu wafungwa kujifunza zaidi.
Kwa muonekano wa nje
Ndani ya vyumba
3. Otago Corrections Facility, New Zealand
Ni moja kati ya magereza yenye ulinzi mkali sana ni ngumu kutoroka bila mitambo ya CCTV kukuacha salama.
Mbali na hivyo, gereza hili hutoa nafasi kubwa ya wafungwa kuishi maisha mazuri, kuanzia kuwa na chumba kizuri pamoja na fursa ya kuongea ujuzi na maarifa. Kuna darasa maalumu kuhusu ukandarasi wa majengo pamoja na umeme. Pia mafunzo ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa pamoja na Upishi.
4. Justice Center Leoben, Austria
Hili ni gereza maalumu kwa ajili ya wafungwa wasio na makosa ya kihalifu. Ndani humu kila mfungwa huwa na chumba chake, choo cha ndani pamoja na jiko na televisheni.
Nje kuna gym center iliyo na kila kitu, uwanja wa kucheza kikapu pamoja na sehemu ya kujiburudisha.
5. Aranjuez Prison, Spain
Ingawa magereza nyingi ndo huwa chanzo cha familia kuvunjika, basi gereza hili kutoka uhispania limekuwa ndo gereza lenye kuruhusu watoto wachanga kuishi na wazazi wao mpaka Miaka mitano kisha utolewa nje kulelewa na ndugu.
Kuna miundombinu tosha kwa wazazi kufurahia wakati na Watoto wao. Kuta za vyumba huchorwa katuni mbalimbali na huwepo na huduma zote muhimu kwa ajili ya wazazi na mtoto.
Bonus:
Champ-Dollon Prison, Switzerland
Gereza kutoka taifa la Uswisi, ambalo mwanzoni lilikutwa na sifa mbaya ya kuwa na wafungwa wengi.
Gereza lilifanyiwa marekebisho kadha wa kadha na kubadilisha muonekano wake.
Kwa sasa linaruhusu watu watatu kulala ndani ya chumba kikubwa kukiwa na bafu ndani.
Msosi wake huandaliwa na wapishi na huwa na vyakula muhimu kwa afya ya mfungwa mmoja mpaka Mwingine. Hata kwa wale wasiotumia baadhi ya vyakula upewa uzito wao.
Lengo la magereza linatofautiana sana kwa fikra za mtu na mtu.
Naomba niishie hapa kwa leo.
@Mshana Jr @Malcom_X @Madame B
Sina maana mbaya kutumia neno hatari 