G.MWAKASEGE
Senior Member
- Jun 29, 2007
- 153
- 15
Tulikuwa na family day na haya ndio niliyoambulia nikaona they are good news worth sharing.
View attachment The Moringa Oleifera Tree.doc
======================
View attachment The Moringa Oleifera Tree.doc
======================
Moringa (Moringa spp.) maarufu kama Mlonge ni miongoni mwa miti muhimu kuliko yote duniani. Mti huu ukuao
haraka hupandwa katika maeneo mengi na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na
kusafisha maji.
![]()
1. Karibu kila sehemu ya mti wa Moringa inatumika au inalika kama chakula. Majani ndio sehemu kuu ya mti wa Moringa, unaweza kuyala yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa kama mboga yoyote ya majani, na pia unaweza ukayakausha na kuyahifadhi kama unga-unga kwa miezi mingi huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi.
Pia majani yanaweza kutumika kama lishe bora ya mifugo.
Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa majani ya Moringa ni chanzo kikubwa cha virutubishi vingi sana. Virutubishi hivi ni pamoja na;
Vitamini C - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Kiwango chake katikamajani ya Moringa ni zaidi ya mara saba ya ile inayopatikana kutoka kwenye machungwa.
Calcium (madini chuma) - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha pamoja na kujenga mifupa na meno mwilini. Kiwango chake katika majani ya Moringa nimara nne zaidi ya yale yanayopatikana kutoka kwenye maziwa.
Protini - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga mwili na kuimarisha ngozi. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara mbili zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye maziwa.
Vitamini A - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha macho na kuongeza uwezo wa kuona. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara nne zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye Karoti.
Potassium - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga na kuupatia mwili nguvu. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara tatu zaidi ya ile ipatikanayo kutoka kwenye ndizi. Maua ya Moringa yamejaliwa madini chuma (calcium) na Potassium kwa wingi na yanaweza kuchemshwa au kupikwa na kuliwa kama mboga.
2. Mboga
Majani ya Moringa huliwa kama mboga nyingine za majani kwa mfano mchicha. Majani yanaweza kuvunwa wakati wa kiangazi ambapo mboga nyingine hazipatikani. Pia matunda mateke ya Moringa huweza kutumika kama mboga, hutayariswa kama maharage mabichi (machanga). Matunda yalikomaa hutoa mbegu ambazo zinaweza kutumika kama njegere au kukaangwa kama karanga.
3. Mafuta
Mafuta kutoka kwenye mbegu za mti wa Moringa huweza kutumika katika kupikia na kuwasha katika nyumba. Pia hutumika sana kwenye viwanda katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo. Mafuta hukamuliwa kutoka kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa.
4. Lishe ya Mifugo
Majani ya Moringa huliwa na ng'ombe, mbuzi, kondoo, sungura na kuku. Mbegu huliwa na kuku pamoja na wanyama wengine kwenye jamii ya ndege.
5. Pambo la nyumba
Mti wa Moringa hupandwa kwa wingi kwenye bustani kama ua au mti wa kivuli na hutumika katika upambaji. Pia miti ya moringa ikipandwa karibu karibu inaweza kutumika kama fensi.
6. Chanzo cha kipato
Mti wa Moringa ukitumiwa vizuri ni chanzo kizuri cha kipato. Mfano ni uuzaji wa miche ya mti wa moringa na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na moringa.
7. Tiba mbadala
Moringa ni mti muhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali.
Majani
- Majani mabichi ya Moringa ni mazuri kwa kina mama wajawazito na wenye kunyonyesha, huongeza wingi wa maziwa na hushauriwa kwa kutibu Anaemia.
- Juisi ya majani ya Moringa hutumika kusafisha tumbo na hutibu magonjwa ya zinaa. Juisi ikichanganywa na asali inatibu kuharisha.
- Pia juisi ina uwezo wa kusawazisha presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye
- kisukari.
- Majani pia huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.
Mbegu
- Mbegu za mti wa Moringa ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi.
- Pia mbegu hutuminka katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa baada ya kuchemsha.
Magome
- Magome ya mti wa Moringa hupondwa na kuwa rojorojo kisha hutumika kutibu majipu pia hupakwa ili kupunguza maumivu yatokanayo na kung'atwa na wadudu kama nyoka na nge.
Matumizi mengineyo
Miti ya Moringa ikipandwa shambani huweza kuwa msaada kwa mimea ipandayo kama vile maharage. Pia Moringa ikipandwa bustanini husaidia kupunguza joto la moja kwa moja kufikia mimea kama vile mboga mboga na kupunguza uwezekano wa mboga kusinyaa au kukauka. Mti wa Moringa unaota katika mazingira yote, kwenye ukame na meneo yenye maji. Angalizo huchukuliwa kuhakikisha kuwa maji hayatuami kwenye mti kwasababu maji huweza kusababisha ugonjwa na kufanya mizizi ioze. Karibu aina zote za udongo zinafaa kwa mti wa Moringa. Mbegu, kipande cha tawi na hata mzizi vinaweza kutumika kuotesha mti wa moringa.
![]()
Namna ya kupanda mti wa Moringa
I. Mbegu
Mbegu iliyokomaa ya mti wa Moringa hulowekwa siku moja kabla ya kuoteshwa, kama maji sio tatizo mbegu inaweza kupandwa moja kwa moja kwenye udongo baada ya kuchimba shimo, weka maji na kisha changanya udongo na samadi angalau kilo tano kabla ya kupanda mbegu halafu endelea kumwagilia katika miezi ya mwanzo. Baada ya angalau siku kumi na tano mbegu inatakiwa iwe imeshachipua. Pia unaweza kuotesha mbegu za Moringa katika vifuko kwenye kitalu kisha kuhamishia shambani baada ya kuota.
II. Kipande cha tawi
Vipande vya tawi lililo komaa huweza kutumika katika kupanda mti wa Moringa, hivi hupandwa eidha moja kwa moja shambani au kwenye vifuko katika kitalu. Kama ukipandwa moja kwa moja angalau robo moja ya tawi inatakiwa ipandwe kwenye udongo, usimwagilie maji mengi sana kwani inaweza kusababisha kuoza.
UNAHITAJI MLONGE? PIGA 0769142586
Mlonge au moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu.
Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.
Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China na kwa mujibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka 45000 ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walikuwepo hapa bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu. Taarifa zisizo rasmi zinadai wachinja hawa walikimbia nchini baada ya serikali kuanza kufuatilia na kuwakamata wakwepaji kodi bandarini. Isingekuwa hivi mpaka leo mlonge ungekuwa umeshatowka wote Tanzania.
Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani. Kile ulikuwa hujui ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajioli ya binadamu na wanyama.
Mlonge una:
Kalsiumu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe
Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi
Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti
Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi
Una klorpfiti (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)
Una madini chuma mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach
Una vitamini A mpaka Z
Una omega 3, 6 na 9
Una asidi amino zile muhimu zinazohitajika na mwili
Una kiasi cha kutosha cha madini ya zinc ambayo ni madini muhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla
Mlonge ndicho chakula chenye afya zaidi juu ya ardhi:
Mlonge una jumla ya virutubishi 92, mmea au mti mwingine wenye virutubishi vingi basda ya mlonge una virutubishi 28. Mlonge una vionsa suku 46 na viondoa uvimbe mbalimbali mwilini 36, una asidi amino 18 na asidi amino muhimu zaidi 9 ambazo miili yetu haina uwezo wa kuzitengeneza.
Unga wa majani ya mlonge unao uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya 300 mwilini, magonjwa hayo ni pamoja na :
1. HUko Afrika magharibi madaktari hutumia mlonge kutibu kisukari.
2. HUko India mlonge hutumika kutibu shinikizo la juu la damu
3. HUtibu matatizo u maumivu ya mishipa
4. Hutuliza mapigo ya juu ya moyo
5. Hutibu kansa
6. Pumu
7. Hutuliza wasiwasi
8. Kikohozi
9. Maumivu ya kichwa
10. Inazuia na kushusha ile lehemu hata ile ya juu zaidi
11. Inapunguza mafuta tumboni
12. Inaweza sawa homoni
13. Inatibu maumivu wakati wa hedhi
14. Unasafisha ini
15. Inasafisha mkojo na kibofu cha mkojo
16. Inarekebisha matatizo kwenye tezi
17. Unatibu kipindupindu na kuharisha
18. Kifua kikuu
19. Kichwa kizito
20. Uchovu
21. Mzio
22. Vidonda vya tumbo
23. Maambukizi kwenye ngozi
24. Maumivu mbalimbali mwilini
25. Huondoa madoa doa meusi kwenye ngozi
26. Husafisha damu
27. Hutibu matatizo kwenye koo
28. Huondoa makohozi mazito kooni
29. Huondoa taka na msongamano kifuani
30. Hutibu kipindipindu
31. Huondoa moto wa jicho au uvimbe kwenye jicho
32. Hutibu maambukizi kwenye macho na kwenye masikio
33. Unatibu homa
34. Maumivu kwenye maungio
35. Huondoa chunusi
36. Hutibu matatizo karibu yote ya ngozi na kinga ya mwili
37. Matatizo kwenye mfumo wa upumuaji
38. Inatibu kiseyeye
39. Huongeza uwingi wa mbegu za kiume na nguvu kwa ujumla
40. Inatibu minyoo
41. Huongeza maziwa kwa wingi kwa mama anayenyonyesha
42. Huondoa uvimbe kwenye utumbo mpana
43. Inatibu ugonjwa wa kuvimba mwili
44. Inatibu kuhara damu
45. Inatibu kisonono
46. Unatibu tatizo la kukosa usingizi
47. Unatibu homa ya manjano
48. Unatibu malaria
49. Unatibu U.T.I na matatizo mengine kwenye mfumo wa mkojo
50. Unasaidia pia kujenga na kuimarisha misuli
51. Unatibu magonjwa ya mifupa
Mlonge uansafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele. Wakati unatumia mlonge unakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya na mwenye nguvu. Watu wengi wanaotumia mlonge huwa ni wenye afya nzuri hata kwa muonekano tu hata wanapokuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 90.
Majani ya mti wa mlonge pia yanaweza kutumika kutengeneza biogas. Hutumika pia kama chakala cha wanyama kama sungura , mbuzi, ng’mbe. Mbwa n.k. Sungura wanaonekana kupenda zaidi mlonge kuliko wanyama wote