Zijue aina ya sheria na mchanganuo wake

Zijue aina ya sheria na mchanganuo wake

SirAlfred006

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2020
Posts
550
Reaction score
1,299

Aina za Sheria na Kazi Zake


1. Sheria ya Jinai (Criminal Law)

Inahusika na makosa ya uhalifu.
  • Kuwashtaki na kuwatetea wahalifu.
  • Uhalifu wa mtandaoni na makosa ya kifedha.
  • Uchunguzi wa ufisadi na makosa ya ofisini.
  • Maamuzi ya vifungo na kukata rufaa.

2. Sheria ya Madai (Civil Law)

Inahusika na migogoro kati ya mtu na mtu au kampuni.

  • Migogoro ya mikataba.
  • Keshi za ardhi na mali.
  • Madai ya kuumia/kudhuriwa mwili.
  • Usuluhishi wa migogoro nje ya mahakama.

3. Sheria ya Makampuni (Corporate Law)

Inahusika na biashara na mashirika.

  • Kuunganisha au kununua makampuni.
  • Uongozi na uendeshaji wa makampuni.
  • Kusimamia sheria za hisa na uwekezaji.

4. Sheria ya Katiba (Constitutional Law)

Hii ndiyo sheria mama ya nchi.

  • Haki za msingi za binadamu.
  • Kuangalia kama maamuzi ya viongozi yanafuata sheria.
  • Tafsiri ya vipengele vya Katiba.

5. Sheria ya Hakimiliki (Intellectual Property Law)

Inalinda kazi za ubunifu.

  • Haki za uvumbuzi na alama za biashara (Logo).
  • Kulinda kazi za sanaa (muziki, vitabu, filamu).
  • Haki za maudhui ya kidijitali na mtandaoni.

6. Sheria ya Mazingira (Environmental Law)

Inalinda asili na dunia.

  • Kanuni za mabadiliko ya tabianchi.
  • Udhibiti wa uchafuzi wa mazingira (hewa, maji, ardhi).
  • Sheria za nishati mbadala (kama umeme wa jua).

7. Sheria ya Familia (Family Law)

Inahusika na mambo ya nyumbani.

  • Talaka na haki ya kulea watoto.
  • Sheria za kuasili watoto.
  • Kulinda wahanga wa ukatili wa kijinsia/nyumbani.
  • Mgawanyo wa mali baada ya kutengana.

8. Sheria ya Kazi (Labour & Employment Law)

Inahusika na uhusiano kati ya bosi na mfanyakazi.

  • Mikataba ya kazi.
  • Kupambana na ubaguzi mahali pa kazi.
  • Migogoro ya mishahara na maslahi.

9. Sheria ya Kodi (Tax Law)

Inahusika na malipo ya serikali.

  • Kupanga kodi za makampuni.
  • Sheria za kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
  • Masuala ya kodi za kimataifa.

10. Sheria ya Kimataifa (International Law)

Inahusika na uhusiano kati ya nchi na nchi.

  • Sheria za biashara duniani.
  • Haki za binadamu kimataifa.
  • Mikataba kati ya mataifa mbalimbali.


20260303_225131.jpg
types of laws
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom