Zijue ABC na historia fupi ya 'Rastafarianism'

Ngumu kuwaelewa hawa watu!

Ni wema sana na wapole sana muda wote wanakua wapenda amani

Huwa wanaridhika na hali zao ziwe za furaha au mateso wao huridhika tu,cha ajabu sasa akipata buku ya kula na akakukuta damu yake hujala na huna hrla ya kula anakupa ile buku kisha anaenda kutafuta hela nyingine ale!

Utachoka zaidi pale anapokuwa na tough life halafu uso wake kaufunika na tabasamu muruwaa!

Kuna mchizi mmoja rasta tumesoma nae jamaa ni mbavu ila mpole na mtaratibu sana,sasa pale shuleni kuna mbabe mkuu mbavu haswa,wana tukasema tuwaandalie pambano hawa! Tukawapanga tukaingia porini pambano likaanza mwisho wa siku Ras akapigwa,jioni yake mshkaji alieshinda akitegemea bifu cha ajabu mshkaji alikua peace kinyama!!! Peace mbele kwa mbele kama hakuna kitu vile!

Mwisho kuna mavuta bange mengine mavibaka yanawaharibia image True Rastafari yanaboa haya mambwa!
Yupo mmoja pale msamvu stand mpaka huwa najiuliza dunia ingekuwa na imani kama hii tusingeona mabinadam kama Putin Trump Bush Tonny wanapenda amani upendo
 
Uzi mzuri sana!! Mi naipenda sana Imani ya Rasta kwa sababu moja muhimu. Ndio Imani au dini pekee katika hizi dini za kisasa zenye mlengo na msisitizo wa Kiafrika na kumtukuza mtu mweusi na Utamaduni wake. Ni juhudi za wenzetu waliochukuliwa utumwani kukataa, kuasi na kutukuza Imani na utu wao kupingana na wakandamizaji wao Wazungu waliokuwa wanawatesa na wanaondelea kuwanyonya mpaka leo. Kwa ajili hii Imani hii ni moja ya harakati za kufikia Umoja wa Mwafrika (Mtu mweusi) yaani Pan Africanism. Hata Msomi mbobezi wa historia na siasa marehemu Walter Rodney (Mwandishi wa How Europe Underdeveloped Africa) katika kitabu chake cha Groundings With My Brothers alisema MaRasta ndio jamii pekee ya watu weusi waliokuwa wanaonyesha uwezo mkubwa katika kujitambua na kuweka juhudi katika kujitegemea bila kutegemea cho chote kutoka jamii za Wazungu. Wamejitahidi sana kupigana na kujikwamua kutoka katika Utumwa wa akili unaotukabili watu weusi hata kutufanya mpaka leo hii kuwa watu wenye akili na mitizamo tegemezi na kupoteza kabisa uwezo wa kujiamini katika kupambana na kutatua matatizo yetu kwenye jamii zetu. Kwa hili tunawakubali sana.
Mahali napogongana na Imani ya KiRasta ni pale nisipokubali kuwa ndio iwe Imani wakilishi au kuibeba kama ndio Imani asili ya Mwafrika. Kwa kusema kweli Rasta msingi wake mkubwa ni maandiko ya kitabu cha Wayahudi cha Biblia. Kwa hiyo kwa upande mmoja Rasta ni tawi la Imani ya Kikristo au tusemi inamapokeo ya Imani za Kiyahudi (Judaism) ambayo asili yake haswa ni huko Israel/Palestina Mashariki ya Kati. Na isemwe wazi Imani hii haina mahusiano ya asili ya Mwafrika kabisa. Rastafarian haiwezi kuwa Imani inayoweza kuwa ndio dini ya Mwafrika yenye asili ya Kiafrika, maana hata manabii wa dini ya Rasta ni wale Wayahudi wa kwenye Biblia. Lakini kwa viwango naikubali sana Imani ya KiRasta kuliko haya madhehebu mengine ya Kikristo au Uislamu maana dini hizo ndizo haswa zilizofanya tusahau Mungu na Miungu yetu mpaka leo tumekuwa bendera fuata upepo watu tusio na mbele wala nyuma.
 
Dini ya upotovu kabisa hii inawapeleka wanaoiamini kwenye kupotea kabisa. kweli shetani ni baba wa uongo na ameongoza watu kuanzia kutabiri, kuvuta bangi , kufuga rasta , kubadili maandiko. Kifupi njia ya kwenda uzimani ni nyembamba na ina watu wachache ila njia ya kwenda upotevuni ni pana na inawatu wengi mno. Yaani dini na madhehebu ya uongo yameimaliza dunia.
 
Rastaman chant
Screenshot_20191117-173153.png
 
Haujui unchoongea,
Unadhani usafi ni kuvaa suti na moka
Hapana mkuu. Marastafari wengu ni wachafu wa mwili, na mavazi!

Si kwa hawa walipo Afrika tu bali hata wa kule Carribians. Nadhaniule utamaduni wa kujiona ni waasili na kwamba wanaundugu na mazingira halisi umeawaathiri sana.

Unaweza ukawa na ndevu, lakini ukaziwrka katika hali ya usafi pia radta unaweza ukazitunza uzuri kabisa. Ila hawa hawafanyi haya.

Ukitaka kuona haya angalia hata nyimbo za raggie uwaone wengi ni wachafu!
 
Hapana mkuu. Marastafari wengu ni wachafu wa mwili, na mavazi!

Si kwa hawa walipo Afrika tu bali hata wa kule Carribians. Nadhaniule utamaduni wa kujiona ni waasili na kwamba wanaundugu na mazingira halisi umeawaathiri sana.

Unaweza ukawa na ndevu, lakini ukaziwrka katika hali ya usafi pia radta unaweza ukazitunza uzuri kabisa. Ila hawa hawafanyi haya.

Ukitaka kuona haya angalia hata nyimbo za raggie uwaone wengi ni wachafu!
Umeamua tu kuona hivyo.....
 
Back
Top Bottom