Hussein Shebe na Haile Selassie

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,274
HUSSEIN SHEBE NA HAILE SELASSIE

Kipande hicho hapo chini kipo hapa tayari katika makala nyingine.

Hata hivyo nimetamani nikiweke kipande hiki hapo chini kijitegemee na sababu ni mapenzi niliyonayo kwa Hussein Shebe.

Siku moja Hussein alikutana na mke wangu Masjid Maamur akampa mke wangu salamu anifikishie.

Mke wangu akajibu, ''Salamu zako In Shaa Allah zimefika kwa rafiki yako.''

Husseina akamkatiza kwa haraka akamwambia, ''Mohamed si rafiki yangu ni ndugu yangu.'':

''...kwangu mimi ilikuwa furaha mara mbili kwanza nikipenda historia kumsikiliza Martin Kiama akimweleza Haile Selassie wa Ethiopia akimwita, "Simba wa Yuda."

Maisha hakika ni safari ndefu.

Miaka mingi baadae nikiwa mwanafunzi Uingereza nitabahatika kuwajua kwa mbali wajukuu wa Haile Selassie wanafunzi wenzangu.

Ufalme wao umepinduliwa na baadhi yao wakajikuta Uingereza kama wakimbizi.

Hakika ufalme ulikuwa umewatoka lakini hawa vijana ndani ya nafsi zao walikuwa bado wanajiona ni wafalme.

Walikuwa wakija mfano kwenye ''party'' za wanafunzi utawaona vichwa juu na mabega juu vilevile na hawachanganyiki na watu wao huwa katika kundi lao vijana sita, saba au kumi hivi na dada zao wamesimama pembeni wamevaa suti na hawapazi sauti kuzungumza inapobidi. waongee.

Hivi ndivyo walivyolelewa na kufunzwa.
Ukoo wa Kifalme lazima uwe tofauti kwa kila hali.

Siku moja rafiki yangu wa Kiethiopia akanieleza haya akaniambia, ''Hawa ndugu zangu hawajaamini kuwa wao si wafalme tena hata hapa Uingereza wanataka watambulike kuwa wao ni watu wa daraja la juu; hebu waangalie.''

Kabla sijafika Uingereza nilibahatika kufika Addis Ababa na kuona hali ya dhiki iliyotamalaki wakati wa utawala wa Mengitsu Haile Mariam.

Nilikaa hoteli iliyokuwa maarufu wakati wa Haile Selassie - Wabe Shebele Hotel.

Hoteli hii nimeikuta imechoka haitamaniki imebakia jina lake na historia yake ya zamani.

Miaka hii ya karibuni nilikuwa nafanya mahojiano na Hussein Shebe.

Hussein ni kijana wa Kariakoo ambae alikuwa na kipaji kikubwa cha uimbaji kiasi alihamia Nairobi akaweka jina kisha akiwa na bendi maarufu pale mjini The Ashantis walikwenda Ethiopia wakawa wanapiga Wabe Shebele Hotel, Addis Ababa Hussein akiwa ndiye nyota wa bendi.

Katiika mazungumzo yetu Hussein akaniambia kuwa wajukuu wa Haile Selassie walikuwa hawapungui Wabe Shebele kuja kucheza muziki wa The Ashantis na wakawa rafiki zake.

Siku moja mmoja katika wale wajukuu wa Haile Selassie alipembeni mvuta akamwambia, ''Hussein fanyeni muondoke hapa kwani kunakuja balaa kubwa ondokeni balaa hilo lisiwakute mkiwa nchi hii.''

The Ashantis wakafunga virago wakaenda Italy.
Haukupita muda mrefu Haile Selassie akapinduliwa.

Hussein alipokuwa ananihadithia habari hii nikawakumbuka wale wajukuu wa Haile Selassie niliokuwanao Uingereza.''

Kwangu mimi ilikuwa furaha mara mbili kwanza nikipenda historia kumsikiliza Martin Kiama akimweleza Haile Selassie wa Ethiopia akimwita, "Simba wa Yuda."

Siku moja rafiki yangu wa Kiethiopia akanieleza haya akaniambia,

''Hawa ndugu zangu hawajaamini kuwa wao si wafalme tena hata hapa Uingereza wanataka watambulike kuwa wao ni watu wa daraja la juu; hebu waangalie.''

Picha: Kulia ni Hussein Shebe akiwa na Haile Selassie, Addis Ababa, Hussein na Mwandishi Dar es Salaam.

May be an image of 3 people
1698259893267.jpeg

1699128736728.jpeg
Ashantis,left to right Lead Guitarist Paddy Gwada,Lead singer Hussein Shebe,Keyboard Emmanuel Esposito,Bass Guitarist Rocky Gwada(This was the last formation
Members who passed away not on the picture
George Mzinga Percussions
Jonathan Jones Saxophonist
Jay Omondi Trumpet.
Philip Ogaye Trumpet
Gregory Becker Trambone
Angelo Mastrangelo keyboardist

Napenda sana histori zako mkuu asante
 
Back
Top Bottom