Zifahamu faida za barua pepe (emails)

Mnyalu Junior

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
573
199
Watu wengi hufungua email accounts kwa sababu maalumu. Moja ya sababu kubwa ya watu wengi kufungua emails kwa sasa ni pamoja na:

-Kuongezeka kwa maombi kwa njia ya mtandao (online applications) ambapo maombi mengi humtaka mwombaji ajaze account yake ya email

-Matumizi ya smartphones zinazotumia android technology ambapo kila mtumiaji wa simu hizo hutakiwa kuweka account ya gmail ili kumuwezesha kuingia play store.

Matumizi mengine ya msingi ya emails ni yapi?

Moja ya matumizi ya msingi ya emails accounts ni kuhifadhi vitu na nyaraka zako muhimu kwenye mtandao (ONLINE)

Kuna nyaraka zako muhimu ambazo ukihifadhi kwenye computer, memory card, flash disk au kwenye CD zinaweza kuibwa, kupotea au kuharibika na hatimaye usizipate tena. Nyaraka hizo ni pamoja na:

-Nyimbo zako za kipekee na uzipendazo (audios &videos

-Mkanda wako wa kuhitimu masomo (graduation)

-Mkanda wako wa harusi

-Picha zako muhimu na za kipekee

-Notice zako muhimu au vitabu (Soft copy)

Ni emails gani unaweza ukafungua na zinatoa online storage kiasi gani?

Kuna emails nyingi lakini zilizo rahisi kutumia kwa watanzania wengi ni hizi tatu; Gmail, Yahoo mail na Microsoft account.

(i) Gmail
Account hii inakupa Gigabytes kumi na tano (GB15) za kuhifadhi vitu vyako online

(ii) Yahoo mail
Account hii inakupa Terabyte moja yaani Gigabytes elfu moja (GB1000) za kuhifadhi vitu vyako online. Hii ni kupitia application yao ya flikr

(iii) Microsoft account
Account hii inakupa Gigabytes thelathini (GB30) za kuhifadhi vitu vyako online. Hii ni kupitia application yao ya "one drive"

Nakukaribisha sasa uanze kjihifadhia nyaraka na vitu vyako muhimu kupitia emails hizo ili kuepuka upotevu.
 
Hebu jaribu kutoa na somo jinsi gani nitaweza kuhidhi nyaraka maana mimi kwenye Gmail nimejaribu Mara nyingi sana nimeshindwa
 
Hebu jaribu kutoa na somo jinsi gani nitaweza kuhidhi nyaraka maana mimi kwenye Gmail nimejaribu Mara nyingi sana nimeshindwa
Ni rahisi sana PTER unaattach documents zako zikizidi MB 25 unatumia Google Drive kisha unasave kama draft. Hakuna kupoteza chochote. Pia kwa watumiaji wa Android App ya Google Photo hufanya backup ya picha zote kwenye simu /tablet yako na kusychronize.
 
Au unaweza kuzihifadhi kwenye Dropbox, One drive au Google Drive, maana ni method rahisi zaidi na inampangilio mzuri pia ni rahisi ku sync kwa devices zako zote..
 
Ni rahisi sana PTER unaattach documents zako zikizidi MB 25 unatumia Google Drive kisha unasave kama draft. Hakuna kupoteza chochote. Pia kwa watumiaji wa Android App ya Google Photo hufanya backup ya picha zote kwenye simu /tablet yako na kusychronize.
Google drive ni ipi
 
Asante sana ngoja nijaribu sasa hivi
 
Hiaiwezekani hackers kuingilia servers za makampuni haya na kupoteza data za watu!?
 
Hiaiwezekani hackers kuingilia servers za makampuni haya na kupoteza data za watu!?
JAYJAY data za watumiaji ni at your own risk, nadhani umesikia jinsi mmiliki wa torrent site iliyokuwa namba 19 kati ya website yenye wingi wa watembeleaji duniani ya www.kat.cr. Alitumia iCloud ya Apple jamaa wa FBI wakafungua na kumkamata. Ana bonge la kesi. Pia jamaa wa Sony Pictures walivamiwa na hackers wa Korea Kusini wanaojiita Guardians of Peace kupitia e-mails. So use e-mail at your own risk. Kuna automated super computers za NSA, Homeland Security, FBI, CIA, TISS, Scotland Yard na wengine wengi zinachuja na kucheck. Ila usiwe na hofu ilimradi haufanyi maovu hakuna shida kwani huwezi kukwepa your electronic foot prints kutokujulikana labda usitumie computer wala Android au OS. Jifunze kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda anatumia simu ya mkononi ya kizamani kukwepa kudukuliwa .

Sent from my TECNO F6 using JamiiForums mobile app
 
Hebu jaribu kutoa na somo jinsi gani nitaweza kuhidhi nyaraka maana mimi kwenye Gmail nimejaribu Mara nyingi sana nimeshindwa

Ni rahisi sana, km una simu ya android ingia play store then download application ya google drive. Baada ya hapo nenda kwenye files zako (km vile ni audios, videos, word documents nk.) Km umeamua uweke audios zifungue then nenda sehemu ya kumark, unaweza ukachagua unazozipenda au ukachagua mark all. Baada ya kumark bonyeza option ya kushare, then chagua upload to google drive. Ukishafanya hvo tayari application itaanza kuapload files zako.
 
Kujulikana akukwepeki katika dunia ya digital.
Na ndio maana watu wengi katika mataifa yanayoendelea wanakuwa wanaogopa ogopa sana na wengi uwakuti katika Wikipedia, kuogopa Kujulikana
 
Hebu jaribu kutoa na somo jinsi gani nitaweza kuhidhi nyaraka maana mimi kwenye Gmail nimejaribu Mara nyingi sana nimeshindwa
Mkuu hii unaweza tumia Google Drive ambayo inakusaidia kutumza na kushare file yenye ukubwa zaidi ya 5Gb, na hii utaipata kwenye account yako ya Gmail maana zote ni product za Google.
 
JAYJAY data za watumiaji ni at your own risk, nadhani umesikia jinsi mmiliki wa torrent site iliyokuwa namba 19 kati ya website yenye wingi wa watembeleaji duniani ya www.kat.cr. Alitumia iCloud ya Apple jamaa wa FBI wakafungua na kumkamata. Ana bonge la kesi. Pia jamaa wa Sony Pictures walivamiwa na hackers wa Korea Kusini wanaojiita Guardians of Peace kupitia e-mails. So use e-mail at your own risk. Kuna automated super computers za NSA, Homeland Security, FBI, CIA, TISS, Scotland Yard na wengine wengi zinachuja na kucheck. Ila usiwe na hofu ilimradi haufanyi maovu hakuna shida kwani huwezi kukwepa your electronic foot prints kutokujulikana labda usitumie computer wala Android au OS. Jifunze kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda anatumia simu ya mkononi ya kizamani kukwepa kudukuliwa .

Sent from my TECNO F6 using JamiiForums mobile app
Ni ngumu Sana kuingia kwenye server za watu kama Google maana technology yao ni ya Hali ya juu na wana kitu kinachoitwa Rubust disaster destroyer(RDD), hii ni Aina ya technology iliyopo kwenye data center zao, inayofanya kazi ya kumomonitor suspicious hardware au software inayotaka kuleta damager kwenye product zao mfano, wewe una virus yupo kwenye hard disk yako na anataka kuleta madhara kwa huduma zao, wao kupitia robust data destroyer wanauwezo wa kuziwia hii kitu hata kabda hakijawafikia na kuleta madhara kwao. Na pia wana kitu kinaitwa Robust data disaster recovery (RDDR) hii ni kitu kinacho recovery data pale inapotokea ajali au majanga ya kimtandao.
 
Mfano nimepoteza simu alafu vitu vyangu nimeviifadhi GOOGLE DRIVE nitafanyaje kuvipata pindi nikipata simu nyingine
 
Mfano nimepoteza simu alafu vitu vyangu nimeviifadhi GOOGLE DRIVE nitafanyaje kuvipata pindi nikipata simu nyingine
Hili swali nami huwa najiuliza lakini sijui majibu yake basi kwa wajuzi wa mambo naomba watusaidie.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom