Ziara za kushtukiza sio dhambi: Mrejesho kwa Ulimwengu

nivoj.sued

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
221
190
"Na Nivoj Sued

Jenerali Ulimwengu amechapisha makala yenye kichwa cha maneno “Staili ya zimamoto na ziara za kushitukiza haziwezi kuendesha nchi” katika gazeti la Raia Mwema, Namba 437, la tarehe 23 Dec 2015, kwenye ukurasa wa saba. Sehemu kadhaa za makala hiyo zinasema:

“Iwapo tunataka kufanya mabadiliko ya kweli katika jinsi tunavyoendesha mambo yetu hatuna budi kuyawekea mifumo na mipangilio ya kuyafanya hayo mabadiliko …

"Ili kutimiza hilo hatuna budi kwanza kuanza na katiba mpya ambayo itatuwezesha kutunga sheria, taratibu na kanuni mwafaka zitakazosimamia utekelezaji wa vipengele vya katiba hiyo...

"Inaelekea mawaziri walioteuliwa walikuwa wamedurusu bosi wao mpya na kubaini kwamba staili yake pamoja na waziri mkuu wake ni (staili ya zimamoto na ziara za kushtukiza) kwenda kwenye maeneo yenye matatizo na kutoa maelekezo ya papo kwa hapo, na baadhi yao wakaanza kuiga staili hiyo...

"Lakini hiyo si dawa. Dawa mujarrab ni kuweka misingi inayoeleweka na kutabirika, na kujenga mifumo imara na inayoaminika ya utekelezaji na utoaji wa taarifa...

"Katiba ndiyo inaweza kutuelekeza ni namna gani iliyo bora ya kuiendesha nchi yetu, kuwapa wote wanaohusika majukumu mahsusi ya kutekeleza na kuainisha mifumo ya utawala.”

Katika maneno yake haya, Ulimwengu anahimiza usanifu na ujenzi wa "mifumo imara" ya utawala na wakati huo kupinga "staili ya zimamoto na ziara za kushtukiza" kama mbinu ya kufuatilia na kutathmini utendaji kazi.

Hata hivyo, kama wanafunzi wa sayansi ya utawala na uongozi wanavyojua, kuna mahusiano yasiyotenganishika kati ya mambo haya mawili. Na mahusiano hayo yana sura ya "kitu-kizima-na-sehemu-zake," ambapo "staili ya zimamoto na ziara za kushtukiza" ni sehemu ya kitu kizima kiitwacho "mfumo wa utawala." Kupindisha ukweli huu sio kosa dogo la kiuandishi, na hasa pale kosa hilo linapokuwa linawaathiri wasomaji wengi wa kawaida wasioweza kulibaini. Wanahitaji msaada dhidi ya "epistemic violence" ya aina hii.

Hivyo, maudhui ya makala yake yanatulazimisha kufanya tafakari ya kina kuhusu oganogramu za taasisi mbalimbali ikiwemo oganogramu ya mamlaka ya nchi.

Oganogramu ni mfumo wa mamlaka ya kiutawala katika taasisi ukiwa unabainisha mgawanyo wa majukumu, mifereji ya maagizo ya kiutendaji, mikondo ya taarifa za utekelezaji, na mahusiano mengine ya kiutawala kati ya mabosi na mawakala waliomo katika taasisi husika.

Katika katiba ya nchi, ukiachilia mbali matamko matatu kuhusu hulka ya taifa, haki na majukumu ya watawaliwa, na jinsi ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, mfumo wa mamlaka ya utawala wa nchi ni tamko la nne ambalo lazima liwemo.

Kwa mfano, katika ngazi ya kitaifa, mfumo wa mamlaka ya utawala katika Tanzania, kama ukiandaliwa kwa kuzingatia Katiba ya Tanzania (1977) utaonekana kama mchoro namba 01.

Kielelezo Namba 01--Mfumo wa Utawala wa nchi ukijumuisha bunge, mahakama na serikali.jpg


Na kwa upande wa serikali pekee, yaani tukiachilia pembeni bunge na mahakama, mfano mzuri wa oganogramu ni mfumo wa mamlaka za kiutawala katika serikali ya Tanzania, kama mchoro namba 02.
Kielelezo Namba 02--Mfumo wa Utawala wa nchi ukijumuisha serikali kuu na serikali za mitaa.jpg

Ni katika mazingira haya ya kitaasisi, Ulimwengu ameandika makala kukosoa mtiririko wa maagizo na mikondo ya taarifa za utendaji kama zinavyopatikana katika mfumo huu wa mamlaka za kiutawala katika serikali ya Magufuli.

Katika makala yake, Ulimwengu alisanifu hoja yenye madokezo mawili na hitimisho linalotokana na madokezo hayo.Makala hii ni kwa ajili ya kuifanyia tahakiki hoja yake ili kuwaondolea wasomaji wetu uwezekano wa kufyonza baadhi ya mawazo yasiyokubaliana na kanuni muhimu za sayansi ya siasa na utawala (politology), na hasa kanuni ya ubosi na uwakala (principal-agent relationship).

Kwa ajili hii, katika aya zifuatazo nitafanya mambo manne: Nitawakumbusha wasomaji kuhusu kanuni ya ubosi na uwakala, nitaichambua hoja ya Ulimwengu, nitaihakiki hoja hiyo, nitaleta ushahidi mzito zaidi kama utetezi wa rai yake ya masingi, na hatimaye nitatoa mapendekezo mwafaka.

Muhtasari wa kanuni ya ubosi na uwakala
Kila wakati linapofanyika tendo la kukasimu madaraka toka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine, huzaliwa uhusiano wa ubosi na uwakala, ambapo, aliyekasimu madaraka ni bosi na aliyekasimishwa madaraka ni wakala wa bosi.

Katika uhusiano huu wa ubosi na uwakala, wakala hutakiwa kutenda kazi katika eneo mahsusi la uamuzi analoaminika kuwa na ustadi nalo, akiwa anafanya kazi hiyo kwa ajili ya, kwa niaba ya, na kama mwakilishi wa bosi.

Hivyo, baada ya zoezi la kukasimishana madaraka, huzaliwa mkataba wenye sura ya ubosi na uwakala kati ya mtoa kasma na mpokea kasma, kila upande katika mkataba huu ukiwa na haki na majukumu yake ndani ya mkataba huu.

Katika utekelezaji wa mkataba wenye sura ya ubosi na uwakala, mambo makubwa mawili yanaweza kutokea.

Kwanza, mkataba huu unaweza kutekelezwa vizuri bila dosari yoyote. Yaani, wakala atatimiza majukumu yake, kwa viwango na kwa wakati, kwa kuzingatia malengo ya bosi; na bosi atatoa vitendea kazi husika, kwa wakati na kwa kiwango stahiki, bila kusahau kumlipa stahiki yake wakala.

Na pili, utekelezaji wa mkataba huu unaweza kwenda mrama kwa sababu ya makosa yatakayokuwa yamefanywa ama na bosi au wakala wake. Nitaeleza hili kwa ufupi.

Uamuzi wa bosi kukasimu madaraka yake kwa wakala, ni uamuzi ambao mara zote huambatana na hatari kadhaa kutoka pande zote mbili—upande wa bosi na upande wa wakala.

Tuanze na upande wa wakala unaohusisha hatari kuu tatu.

Awali ya yote, wakala anaweza kutoa taarifa za uwongo kuhusu elimu, ujuzi, uzoefu na upatikanaji wake kabla na wakati wa kuajiriwa. Kwa sababu hii, bosi akajikuta ametoa madaraka, kuajiri au kuteua mtu asiye na sifa stahiki (adverse selection).

Aidha, baada ya wakala sahihi kupewa kazi, kwa makusudi, anaweza akayaweka pembeni baadhi ya malengo aliyokubaliana na bosi wake na, badala yake, akaanza kutumia sehemu ya muda wa ofisi kufukuzia malengo binafsi (agent shirking/drift). Katika hali hii wakala atafanya kazi chini ya kiwango, na hivyo bosi wake kusababishiwa hasara (agent loss).

Lakini pia, wakala anaweza kujitahidi kutekeleza malengo ya bosi vizuri kwa moyo wote akiwa anafuata taratibu zote, kwa mujibu wa makubaliano lakini bado ikatokea kwamba malengo ya bosi hayatimii.

Hapa, huwa kuna dosari ya kimfumo, kiasi kwamba hata bila wakala kufukuzia malengo binafsi kwa kufanya kazi zilizo nje ya makubaliano na bosi wake, lakini bado utendaji wake unakuwa chini ya kiwango (agent slippage).

Kwa hiyo, kwa mujibu wa kanuni ya ubosi na uwakala, ili kupunguza uwezekano wa matatizo haya ya wakala kutokea, ni lazima bosi afanye jitihada za aina tatu.

Kwanza; ni lazima mifumo ya kuchuja watu kabla ya kuwaingiza ofisini iimarishwe, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba mikataba yao ya kazi inaandaliwa kisayansi bila utata wowote (ex-ante control mechanisms).
Pili; mfumo wa kusimamia utendaji kazi wa watumishi wa umma kila mara wanapokuwa kazini lazima ibuniwe (on-the-spot control mechanisms).

Mifano mizuri ya mfumo huu ni Kamati za Bunge za kisekta zinazofanya kazi kwa utaratibu ulio “overt,” na ziara za ukaguzi wa kushtukiza kama wafanyavyo wakaguzi wa elimu nchini. Idara ya Usalama wa Taifa inayo nafasi kubwa katika kufanikisha utaratibu kupitia ziara za siri (“covert operations”). Kawaida, afisa usalama aliye eneo la tukio anafanya kazi kama "fire alarm" halafu mtedaji wa serik ali kama vile DC, RC au Waziri anafika eneo la tukio kupitia ziara za wazi (overt operations) ili "kuzima moto" ulioripotiwa na afisa usalama. Ni kwa sababu hii nilipoona makala yenye kichwa cha maneno “Staili ya zimamoto na ziara za kushitukiza haziwezi kuendesha nchi” nikahisi tatizo mara moja.

Na tatu; ni lazima kuimarisha mfumo wa kupata mrejesho wa taarifa za utendaji kazi wa wakala, kuboresha maslahi yake, na kusimamia nidhamu yake kwa njia ya adhabu zilizopo kwa mujibu wa sheria (ex-post control mechanisms).

Hata hivyo, kwa mujibu wa kanuni ya ubosi na uwakala, haitoshi kudhibiti dosari zinazoweza kujitokeza katika mienendo ya wakala.

Uhusiano wenye sura ya ubosi na uwakala unaweza kukwama pia kwa sababu ya dosari zilizo katika mwenendo wa bosi mwenyewe.

Kwanza; bosi anaweza kushindwa kutoa rasilimali za kutosha, na hivyo mawakala wake kukosa vitendea kazi vya kutosha (principal shirking/drift).

Pili; bosi mkubwa pamoja na mabosi wengine wanaofanya maamuzi ya pamoja naye, wanaweza kushindwa kukubaliana kuhusu dira na dhima ya kitaasisi iliyo mbele yao, hivyo kushindwa kufanya kazi kama timu moja (mission creep).

Tatu; baadhi ya mabosi wanaofanya maamuzi ya pamoja na bosi mkubwa wanaweza kula njama za kuhujumu utendaji kazi wa wakala kwa kumpa maelekezo yanayokwamisha kazi ya kufukuzia malengo ya yaliyokubaliwa kwa pamoja (principal subversion).

Na nne; bosi anaweza kumpa wakala majukumu yenye kugongana na hivyo kumfanya wakala ashindwe kujua afanye lipi na kuacha lipi (antinomic delegation).

Kwa ufupi hiyo ndiyo kanuni ya ubosi na uwakala. Ni kanuni muhimu katika sehemu zote ambako kunafanyika zoezi la kukasimu madaraka, kufuatilia utendaji wa kazi na kusimamia nidhamu kati ya mabosi na mawakala wao.

Uchambuzi wa hoja ya Ulimwengu

Baada ya kuiona kanuni ya ubosi na uwakala, sasa tuelekee kwenye uchambuzi na uhakiki wa hoja ya Ulimwengu. Tuanze na uchambuzi.

Katika ngazi ya uchambuzi, nataka kubainisha anatomia ya kimantiki ili kuweza kuchunguza usahihi wa kimuundo (logical validity) wa hoja hii. Usahihi wa kimuundo unakuwepo ka a hoja inalo dokezo kuu, dokezo dogo na hitimisho linalotokana kihalali na madokezo hayo mawili.

Kianatomia, hoja ya Ulimwengu imegawanyika katika sehemu tatu kuu, yaani madokezo mawili na hitimisho.

Katika dokezo la kwanza, Ulimwengu amedai kwamba, muundo wa mamlaka ya utawala wa nchi ulio hafifu hutokana na Katiba ya nchi isiyo na mwongozo thabiti kuhusu namna sahihi ya kusanifu muundo wa mamlaka ya utawala wa nchi ulio bora.

Katika dokezo la pili, Ulimwengu amedai kwamba, nchini Tanzania kuna muundo wa mamlaka ya utawala wa nchi ulio hafifu na wenye utata unakwaza kasi na ufanisi unaotafutwa na serikali ya Magufuli.

Kutokana na madokezo haya, hatimaye Ulimwengu alihitimisha hoja kwa kudai kwamba, Watanzania lazima tuharakishe kazi ya uandishi wa Katiba Mpya ili tuweze kuondokana na mfumo hafifu wa mamlaka ya utawala wa nchi unakwaza kasi na ufanisi unaotafutwa na serikali ya Magufuli.

Kwa maoni yangu, hitimisho hili linatokana na madokezo yaliyolitangulia. na hivyo, lazima nisema kwamba, sina tatizo na usahihi wa kimuundo wa hoja ya Ulimwengu kwa sababu madokezo na hitimisho lake vinakubaliana.

Uhakiki wa hoja ya Ulimwengu

Baada ya uchambuzi sasa ni uhakiki. Na katika ngazi ya uhakiki nitachunguza usahihi wa kimaudhui (logical soundness). Usahihi wa kimaudhui inakuwepo kama madokezo yanayounda hoja ni ya ukweli, kwa maana kwamba, sababu za kuyatetea zilizotolewa na mleta hoja zinaendana na ukweli halisi kama ulivyo katika ulimwengu halisi.

Pamoja na usahihi wa kimuundo nilioutaja hapo juu, hakuna usahihi wa kimaudhui (logical soundness) katika hoja ya Ulimwengu. Haupo kwa kuwa, sababu zilizo tolewa na mleta hoja ili kutetea dokezo la pili haziendani na ukweli halisi kama ulivyo katika ulimwengu halisi wa menejimenti. Na dosari katika dokezo moja pekee inatosha kuitia doa hoja yote. Nitaeleza hili kwa kina.

Katika makala yake, Ulimwengu alitoa sababu tano za kutetea uhalali wa madai kwamba, nchini Tanzania kuna muundo wa mamlaka ya utawala wa nchi ulio hafifu na wenye utata unaoweza kukwaza kasi na ufanisi unaotafutwa na serikali ya Magufuli.

Mosi, Ulimwengu alidai kwamba, Rais Magufuli amewarudisha mawaziri ambao tayari wanabeba tuhuma za kufanya vibaya kutoka baraza lililopita. Ulimwengu hakuwataja wahusika hao wala kutoa ushahidi wa kuthibitisha tuhima zinazowakabili. Lakini, tuhuma huwa zinabaki ni tuhuma mpaka hapo zitakaothibitishwa kwa ushahidi usioacha chembe ya shaka. Kwa hiyo, madai yake haya yanabaki ni maoni yasiyo na nguvu ya kiushahidi, mpaka hapo atakapoyafafanua.

Pili, Ulimwengu alidai kwamba, Rais Magufuli na Mawaziri wake wanatumia staili ya ziara za kushtukiza kwenda kwenye maeneo yenye matatizo na kutoa maelekezo ya papo kwa hapo, wakati staili hii haipaswi kutumika kuendesha serikali. Hata hivyo, kuna staili nyingi za menejimenti. Kuna menejimenti staili ya MBWA (management by walking around), menejimenti staili ya MBO (management by objectives), na menejimenti staili ya MBC (management by crisis). Wakati nakubaliana naye katika kupinga menejimenti staili ya MBC, sikubaliani naye anapopinga menejimenti staili ya MBWA. Staili ya ukaguzi wa kushtukiza inahalishwa na umuhimu wa kuwepo kwa mifumo ya kuwadhbiti mawakala wakati wanapokuwa wanaendelea na kazi zao (on-the-spot control mechanisms). Kwa hiyo, madai haya ya Ulimwengu pia yanabaki ni maoni yasiyo na uwiano na tunayoyafahamu katika ulimwengu halisi wa menejimenti. Yanatupwa.

Tatu, Ulimwengu alidai kwamba, Rais Magufuli na mawaziri wake wanayo tabia ya kutoa maelekezo na maagizo ya papo kwa papo mbele ya vyombo vya habari, ili watu baki waone kwamba wanachapa kazi, tabia ambayo anasema inalenga kujitafutia sifa za gharama nafuu, na hivyo upuuzi mtupu. Tafsiri yake kwamba, hii nia tabia ambayo inalenga kujitafutia sifa za gharama nafuu imemfanya ashindwe kuona jambo chanya ndani ya tabia hii. Vyombo vya habari ni mfereji ya taarifa kutoka eneo la tukio mpaka kwa watu ambao hawakuwa eneo hilo. Sio kosa, waziri kuvitumia kuambukiza mawazo na staili ya uongozi anayoipendelea kwa wasaidizi wake walioko nje ya eneo la tukio. Kwa hiyo, madai yake haya pia yanabaki ni maoni yasiyo na uwiano na tunayoyafahamu katika ulimwengu halisi. Yanatupwa pia.

Nne, Ulimwengu alidai kwamba, baadhi ya vigogo wanafanya kazi za vigogo wengine na kuacha kazi zao. Alitoa mfano kwamba, Rais ameonekana akifanya kazi za mawaziri, mawaziri wakifanya kazi za makatibu wakuu, makatibu wakuu wakifanya kazi za makamishna na makamishna wameonekana wakifanya kazi za maofisa wa ngazi za chini. Hapa Ulimwengu amesahau jambo moja muhimu katika tukio la kukasimu madaraka kutoka kwa mtu mmoja (X) kwenda kwa mtu wa pili (Y).

Kwa uelewa wangu, tukio hili halina sura ya “utekelezaji ni jukumu la X au Y.” Pia, tukio hili halina sura ya “utekelezaji ni jukumu la X pamoja na Y.” Badala yake, tukio la kukasimisha madaraka lina sura ya “utekelezaji ni jukumu la X kama Y akishindwa.” Yaani, kadiri atakavyoona inafaa, mtoa kasma ya madaraka anayo fursa ya kutwaa sehemu ya majukumu aliyoyakabidhi kwa wakala wake. Ziara za kushtukiza zinakuja katika sura hii. Kwa hiyo, madai ya Ulimwengu hapa pia yanabaki ni maoni yasiyo na uwiano na tunayoyafahamu katika ulimwengu halisi wa menejimenti. Yanatupwa pia.

Na tano, Ulimwengu alidai kwamba, Waziri wa wizara moja ameonekana akifanya kazi ya wizara ya pili kimakosa, huku waziri wa wizara ya pili akifanya kazi ya wizara ya tatu kimakosa pia. Ulimwengu hakuwataja mawaziri wanaohusiana na madai haya ili tuweze kupima ushahidi wake. Kwa hiyo, madai ya Ulimwengu hapa pia yanabaki ni maoni yasiyo na nguvu za kiushahidi, mpaka hapo atakapoyafafanua.

Kwa ufupi kabisa, Ulimwengu hakuweza kutetea usahihi wa dokezo lake la pili, na jambo hili linaitia dosari ya kimantiki hoja yake.

Sababu za ubovu katika muundo wa utawala

Tukirejea katika mchoro namba moja hapo juu ni rahisi kuona sababu mahususi za kutetea madai ya Ulimwengu kuhusu ubovu katika mfumo wa utawala wetu.

Sababu mbili za kwanza zinatokana na ukweli kuwa, mahali fulani, mfumo wa utawala katika serikali kuu unabebana na mfumo wa utawala katika serikali mitaa.

Kwanza, ofisi ya mkuu wa wilaya inafanya kazi sambamba na ofisi ya mkurugenzi wa maendeleo ya wilaya. Hivyo, hapa kuna watumishi wengi kuliko kazi zilizopo. Na pili, ofisi ya mtendaji wa kata inafanya kazi sambamba na ofisi ya afisa tarafa. Hivyo, hapa pia kuna watumishi wengi kuliko kazi zilizopo.

Tukiachilia mbali tatizo la mifumo ya utawala inayobebana, kuna tatizo la mgawanyo tata wa majukumu.

Kama mchoro namba moja unavyoonyesha hapo juu, kuna mahusiano ya aina tatu kati ya serikali kuu na serikali za mitaa.

Kwanza, ni mahusiano katika masuala ya kitaalamu. Pili, ni mahusiano katika masuala ya ushauri. Na tatu, ni mahusiano katika masuala ya utawala na udhibiti.

Kadiri ninavyofahamu, tangu 1996 tulipoamua kufanya ugatuzi wa madaraka kwa staili ya “decentralisation-by-devolution,” hakuna mwongozo ulio wazi kuhusiana na mgawanyo wa majukumu haya.

Katika utaratibu huu, mawaziri wanayo mawasiliano ya moja kwa moja na wakuu wa idara za kitaalam zilizoko katika ofisi za mikoa na wilaya, hata bila kupitia kwa mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya.

Hitimisho na mapendekezo

Kata andiko hili nimefanya kazi mbili kuu. Kwanza nimechambua hoja ya Ulimwengu ili kuipa muundo wa kimantiki lakini bila kupoteza maana ya msingi iliyokusudiwa na mwandishi (argument analysis). Na pili nimehakiki hoja hiyo (argument evaluation).

Katika kufanya haya mawili, nimejaribu kuonyesha kuwa, pamoja na kwamba ni madai ya kweli kusema kuwa, nchini Tanzania kuna muundo wa mamlaka ya utawala wa nchi ulio hafifu na wenye utata unakwaza kasi na ufanisi unaotafutwa na serikali ya Magufuli, lakini bado, sababu zilizotolewa na Uliwengu hazisaidii kuthibitisha madai haya.

Kwa maneno mengine, alichofanya Ulimwengu ni sawa na kumkamata mwizi wa “mbuzi” wako ukampeleka polisi, halafu katika ngazi ya ushahidi unaleta ngozi ya “kondoo.” Ni kweli mtu huyo alikuibia, lakini hakuiba kondoo. Hivyo, huwezi kushinda kesi. Hii ndiyo pointi yangu kuu hapa.

Baada ya kuyasema hayo, napenda kuhitimisha kwa kusema mambo machache.

Kwanza, menejimenti ya staili ya ziara za ukaguzi wa kushtukiza ni kanuni mojawapo na muhimu katika kuendesha nchi. Kwa mfano, kwa muda mrefu imekuwa ikitumiwa na wakaguzi wa elimu hapa Tanzania.

Na pili, ni madai a kweli kusema kwamba, nchini Tanzania kuna muundo wa mamlaka ya utawala wa nchi ulio hafifu na wenye utata unakwaza kasi na ufanisi unaotafutwa na serikali ya Magufuli. Hata hivyo, kunahitajika sababu nzuri ili kuthibitisha madai haya. Sababu zilizotolewa na ulimwengu hazikidhi mahitaji.

Kwa hiyo, sasa namwomba Ulimwengu atusaidie kubainisha mapungufu yaliyomo katika mfumo wa utawala wa nchi ya Tanzania kwa ufasaha zaidi ili wasomaji wake tufaidike.

Kimsingi, naamini kwamba wasomaji tutafaidika zaidi katika eneo hili iwapo tutapatiwa majibu kwa maswali haya:

Mosi, ni kwa kiwango gani, majukumu ya watumishi wa umma yanapaswa kusanifiwa na kugawanywa katika vijikazi tofauti? (work specialisation principle). Pili, ni kwa kuzingatia vigezo gani vijikazi vinapaswa kukusanywa pamoja katika wizara na idara tofauti? (departmentation principle)

Tatu, ni kwa bosi gani mfanyakazi mmoja mmoja au makundi ya wafanyakazi wanapaswa kuwa anaripoti? (chain of command principle). Nne, ili ufuatiliaji na tathmini ya kazi ifanyike kwa ufanisi na kasi, ni watumishi wangapi wanapaswa kuwa katika wigo wa udhibiti wa kiongozi mmoja katika ngazi yoyote? (span of control principle)

Tano, kwa ajili ya kuleta ufanisi na kasi, ni kwa kiwango gani maamuzi ya kiutawala yagatuliwe? (decentralization and centralisation principle). Sita, ni kwa kiwango gani serikali inapaswa kuwa na kanuni na taatibu za kuongoza matendo ya watumishi wa umma na mabosi wao? (formalisation principle)

Saba, Katiba ya Tanzania (1977) kama inavyotumika sasa, pamoja na sheria mbalimbali za Bunge la Tanzania, vinajibu maswali haya katika upeo upi? Nane, rasimu ya pili ya Tume ya Warioba inajibu maswali haya katika upeo upi? Tisa, Katiba Inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba inajibu maswali haya katika upeo upi?

Na mwisho, kumi, tunapaswa kwenda wapi baada ya kuyajua yote haya?
 
Last edited:
Ahsante sana.....chapisho kama hizi ndo zitakuja ipa jamii forum sifa yake ya zaman. Hope tutajadili hapa kwa mustakabali wa taifa letu na sio kwa mihemko. Pia tutapata nafasi ya kuwachambua waandishi wetu hususan wa makala na habari za kiuchunguzi.
 
Ahsante sana.....chapisho kama hizi ndo zitakuja ipa jamii forum sifa yake ya zaman. Hope tutajadili hapa kwa mustakabali wa taifa letu na sio kwa mihemko. Pia tutapata nafasi ya kuwachambua waandishi wetu hususan wa makala na habari za kiuchunguzi.
Ukisikia ujinga na upumbavu uliopitiliza mipaka ndio huu. Mtu anapinga nchi kuwa na mifumo thabiti na anasema uendeshaji wa zimamoto ndio sahihi! Halfu anatokea nyumbu mwingine anaunga mkono!
 
Tatizo la ulimengu tangu zamani alikuwa kwa lowassa.angedeclare interest ingekuwa bora. Lakini ni watanzania hawahawa tumelaumu utawala wa kikwete wa kuwaachia watu wafanye mambo ya kumdanganya.sasa magufuri kafuatilia yeye mwenyewe kujiridhisha kama pale muhimbili wakati mawaziri hawajateuliwa sijui alitaka magufuri akae tu asubiri report ambazo zinakuja zimepikwa na makatibu wakuu.nadhani bwana ulimwengu inabidi awe more analyitical kuliko huu usanii wa kulaumu bila kuonyesha njia.

Any way mia ni ukawa lakini katika hoja za kitaifa tutaendelea kukosoana
 
Tatizo la ulimengu tangu zamani alikuwa kwa lowassa.angedeclare interest ingekuwa bora. Lakini ni watanzania hawahawa tumelaumu utawala wa kikwete wa kuwaachia watu wafanye mambo ya kumdanganya.sasa magufuri kafuatilia yeye mwenyewe kujiridhisha kama pale muhimbili wakati mawaziri hawajateuliwa sijui alitaka magufuri akae tu asubiri report ambazo zinakuja zimepikwa na makatibu wakuu.nadhani bwana ulimwengu inabidi awe more analyitical kuliko huu usanii wa kulaumu bila kuonyesha njia.

Any way mia ni ukawa lakini katika hoja za kitaifa tutaendelea kukosoana

Ukisoma maandishi ya Jenerali kuna sehemu anaishambulia serikali kutokuweka mifumo ya kufanya kazi. Baadae unajiuliza, hivi serikali ya mwezi mmoja inaweza kuwa imeweka mifumo gani? na ni mifumo gani itaanzishwa pasipo binge kukaa? unajiuliza hili bunge lina siku ngapi, je limefanya vikao vingapi ukiachia kusajiri, kuidhinisha teuzi n.k ni kazi gani imeshafanywa na binge hili kama hata hotuba ya rais bado kuanza kujadiriwa? Mzee Ulimwengu amekosea timing ya makala yake, naona amekuwa kinadharia zaidi.
 
Na Nivoj Sued



Mfano mzuri wa oganogramu ni mfumo wa mamlaka za kiutawala katika serikali ya Tanzania, kama mchoro namaba moja hapa chini unavyoonyesha. Huu ni mchoro wa mti wenye matawi mengi ukiwa katika mkao wa wima.

attachment.php
Bila kufifisha hoja ningependa kufahamu kama kielelezo hapo juu hakijaathiriwa na mabadiliko ya TAMISEMI kuhamishwa kutoka kwa waziri mkuu.

Kwa upanuzi wa hoja napenda kumulika pia suala la waziri mkuu na katibu kiongozi, TAMISEMI kuhamia kwa Rais ina maana itakuwa chini ya katibu kiongozi ambaye ndiye muajiri mkuu? Kama ndivyo hii haimpunguzii nguvu Waziri Mkuu ambaye ni nembo ya Serikali bungeni lakini hatakuwa na mamlaka ya moja kwa moja kwa makatibu tawala.

Mnaofahamu mgawanyo wa madaraka na majukumu mtupe elimu.
 
Ulimwengu bado ni legendary kwangu, cheap attention ya JPM na Majaliwa ni upuuzi sana. Tunahitaji mikakati na siyo mishutokizo.
 
Hoja ya msingi ya Ulimwengu ni kupinga dhana ya kuendesha nchi kwa kutegemea misuli ya individuals badala ya misuli ya taasisi. Misuli ya individuals ni midogo na mifupi mno kuweza kufika kila kona wakati misuli ya taasisi ikiimarishwa ina uwezo usio na mipaka. Ni Kwa sababu hii ni muhimu viongozi Kufanya kazi kujenga na kuimarisha taasisi za kiutawala. Nadhani bado tunakumbuka hotuba maarufu ya Obama huko Ghana miaka miwili iliyopita aliposema Africa doesn't need strong individuals; it needs strong institutions"! Naamini mjibuji wa makala ya Ulimwengu anahitaji kumsoma tena.
 
Hoja ya msingi ya Ulimwengu ni kupinga dhana ya kuendesha nchi kwa kutegemea misuli ya individuals badala ya misuli ya taasisi. Misuli ya individuals ni midogo na mifupi mno kuweza kufika kila kona wakati misuli ya taasisi ikiimarishwa ina uwezo usio na mipaka. Ni Kwa sababu hii ni muhimu viongozi Kufanya kazi kujenga na kuimarisha taasisi za kiutawala. Nadhani bado tunakumbuka hotuba maarufu ya Obama huko Ghana miaka miwili iliyopita aliposema Africa doesn't need strong individuals; it needs strong institutions"! Naamini mjibuji wa makala ya Ulimwengu anahitaji kumsoma tena.

Ulimwengu ni mwanaharakati sio mwanazuoni. Yeye ni aina ya akina Bisimba Kijo na amewahi hata kuwa mmoja wa wanakamati zao, siku zote ni mtu wa ku criticize hoja yenye nguvu na katika wachambuzi hawezi kuchukuliwa katika ujengaji hoja madhubuti za mifano k.v.y. Kufuata falsafa za "Iron law of Oligarchy" alishashindwa!
 
Prof Mkumbo samahani kidogo: Mfumo wa kiutawala kuongoza nchi unaweza kukamilika kwa siku moja au miezi kadhaa?
Je mfumo huo unatengenezwa na MTU mmoja (rais) bila kushirikisha mihimili mingine kwa ushirika wa wadau wengine?
Wakati mfumo ukijengwa; je maisha ya watanzania yausubiri mfumo uive.?
Je prof unahakika kuwa mfumo wa utawala wa Mh rais utaendelea kuwa huu huu?
Mzee Jenerali Twaha Ulimwengu amewahi sana kuleta makala yake. Angeweka kama USHAURI ninaamini tungemuelewa vizuri zaidi.
Si rahisi Prof kufundisha chekechea.
 
Hoja ya msingi ya Ulimwengu ni kupinga dhana ya kuendesha nchi kwa kutegemea misuli ya individuals badala ya misuli ya taasisi. Misuli ya individuals ni midogo na mifupi mno kuweza kufika kila kona wakati misuli ya taasisi ikiimarishwa ina uwezo usio na mipaka. Ni Kwa sababu hii ni muhimu viongozi Kufanya kazi kujenga na kuimarisha taasisi za kiutawala. Nadhani bado tunakumbuka hotuba maarufu ya Obama huko Ghana miaka miwili iliyopita aliposema Africa doesn't need strong individuals; it needs strong institutions"! Naamini mjibuji wa makala ya Ulimwengu anahitaji kumsoma tena.

Ulimwengu ni mwanaharakati sio mwanazuoni. Yeye ni aina ya akina Bisimba Kijo na amewahi hata kuwa mmoja wa wanakamati zao, siku zote ni mtu wa ku criticize hoja yenye nguvu na katika wachambuzi hawezi kuchukuliwa katika ujengaji hoja madhubuti za mifano k.v.y. Kufuata falsafa za "Iron law of Oligarchy" alishashindwa!
 
Prof Mkumbo samahani kidogo: Mfumo wa kiutawala kuongoza nchi unaweza kukamilika kwa siku moja au miezi kadhaa?
Je mfumo huo unatengenezwa na MTU mmoja (rais) bila kushirikisha mihimili mingine kwa ushirika wa wadau wengine?
Wakati mfumo ukijengwa; je maisha ya watanzania yausubiri mfumo uive.?
Je prof unahakika kuwa mfumo wa utawala wa Mh rais utaendelea kuwa huu huu?
Mzee Jenerali Twaha Ulimwengu amewahi sana kuleta makala yake. Angeweka kama USHAURI ninaamini tungemuelewa vizuri zaidi.
Si rahisi Prof kufundisha chekechea.

Very good question. Nilikuwa na swali hilihili. Standby for Professor Mkumbo to answer.
 
naungana na msingi wa hoja ya ulimwengu, japo namna ya uongozi wa JPM umeonyesha tija kwa kiasi ila si endelevu, unahitajika mfumo dhabiti ambao hata kiongozi dhaifu utambainisha na kumwadhibu.
 
naungana na msingi wa hoja ya ulimwengu, japo namna ya uongozi wa JPM umeonyesha tija kwa kiasi ila si endelevu, unahitajika mfumo dhabiti ambao hata kiongozi dhaifu utambainisha na kumwadhibu.

mfumo ni mchakato sio kitu cha overnights. Kama nchi lazima tujue tunakwama wapi. Nani ni msababishi.
Mfumo ni watu (key players) Tukishabainisha mfumo ndio tunajaza nafasi.
Hoja imekuja kwa staili ya lawama.
 
Hoja ya msingi ya Ulimwengu ni kupinga dhana ya kuendesha nchi kwa kutegemea misuli ya individuals badala ya misuli ya taasisi. Misuli ya individuals ni midogo na mifupi mno kuweza kufika kila kona wakati misuli ya taasisi ikiimarishwa ina uwezo usio na mipaka. Ni Kwa sababu hii ni muhimu viongozi Kufanya kazi kujenga na kuimarisha taasisi za kiutawala. Nadhani bado tunakumbuka hotuba maarufu ya Obama huko Ghana miaka miwili iliyopita aliposema Africa doesn't need strong individuals; it needs strong institutions"! Naamini mjibuji wa makala ya Ulimwengu anahitaji kumsoma tena.

Ni kweli kabisa Prof, lakini tukumbuke kwamba kufanya taasisi zifanye vizuri ni mchakato unaoishi, na unahitaji muda wa kutosha, ila kwa kipindi ambapo taasisi zipo lakini zimeshindwa kutenda ipasavo, nchi, taasisi au kampuni inahitaji maamuzi ya haraka kunusuru hali halisi, mfano TRA na TPA. Kisha, kuwakumbusha watendaji kwamba serikali ipo.

Naamini Mh JPM ni transformational leader na atatekeleza lengo kuu la kuunda taasisi nguvu kwa muda muafaka,lakini kwa sasa tuache hatua okoa zifanye kazi, halafu tuataendelea kwa utaratubu kutengeza utaratibu utakaofuatwa na mtu yeyote atakaye shika hatamu.
 
Duh! Unatumia maelezo magumu kueleza kitu rahisi kueleweka. Unatoa sababu nyepesi kupinga mada iliyojitosheleza, hitimisho langu ni kuwa:- unataka uonekane uajua zaidi ya unae mkosoa- wish all the best with that.
 
Back
Top Bottom