"Namna ulimwengu ulivyoweza kugawanywa matabaka mawili"

Jul 13, 2021
5
4
Na:Abdull Najad Faiq

Ulimwengu wetu wa leo ni ulimwengu ambao haupo sawa ni ulimwengu ulio matabaka mawili baina ya weusi na walio weupe,baina ya maskini na matajiri,baina ya wenye nguvu na walio dhaifu,baina ya walio bora na walio duni na baina ya watawala na walio watawaliwa

Ulimwengu umeundwa na chombo kinachoitwa Umoja wa Mataifa huyu ni regulator wa mambo yote yanayotendeka duniani akisaidiwa na baadhi ya taasisi zake ikiwemo IMF,WHO,ICC na nyenginezo lakini nyuma ya hiki chombo kuna yule anae kitunza ama kukifadhili kwa kiasi kikubwa na ndio mwenye haki zaid na anae wajibikiwaa kwa yote

Africa na nchi za bara la Asia ni katika nchi zilizo tabaka la pili la ulimwengu ni tabaka la watawaliwa daima ulimwengu ukisimamiwa na kitu kinachoitwa UN umekua haiupi uzito kwa ukubwa matukio yanayowakumba watu wa bara la Africa na Asia ukilinganisha kama inavyoyapa uzito maswaibu ya nchi za ulaya

Kijana na mzee wa kiafrika unapaswa ufungue vyema fikra zako
Tuangalie namna ulimwengu ulivyoweza kusimama na Ukrain katika vita vyake ilichukua hatua gani, kwanza walipeleka dhana za kijeshi,pili waliidhinisha fedha mabilioni ya dolla, tatu walitoa hadhi za kipekee kwa wakimbizi raia wa Ukrain na nne walimuekea vikwazo vya kiuchumi adui yake

Tuangalie kile kinachotokea leo Palestina kati yake na Israel
Palestina haitambuliki kama nchi duniani,haina jeshi,Israel haipigani na nchi bali inapigana na kikundi tu cha wanamgambo mithili ya waasi wa Congo M23 wasio na vifaru wala ndege za kijeshi lakini Marekani ameipa Israel silaha za kivita,kikosi cha jeshi na meli kubwa ya kivita kuhakikisha adui haingii kwake

Hili ni tofauti na namna Marekani na unaoitwa Umoja wa Mataifa unavyoshughulikia mgogoro wa kivita baina ya jeshi la Congo na waasi wa M23,ni tofauti na America inavyoshughulikia njaa katika nchi ya Sudan,Somalia na sehem katika nchi ya Kenya

Laiti kama Marekani wangeamua wangeweza kuwasambaratisha waasi wa Congo na wale wa Nigeria Boko haram kwa siku chache tu kupitia misaada yao ya silaha za kijeshi pekee kwa nchi husika lakini tambua vita yoyote inayotokea duniani katika nchi za kiafrika na za kiarabu zenye rasilimali za madini na mafuta ni mkakati wa Marekani na nchi za kimagharib katika kuiba rasilimali, hakuna amani inayolindwa kwa kuwalinda raia pekee na wakaachwa salama waasi na kama hilo lingekua ni sahihi tusingeshuhudia misaada ya kijeshi kwa nchi zilizo tabaka la kwanza kutoka kwa Marekani

Ikiwa UN na Marekani wanazuia wanajeshi wanaolinda amani wasitumie mizinga ya masafa marefu kuwasambaratisha waasi wa Congo kwa kile wanachosema kwamba hakuna vita ilhali kila siku waasi wanaua wananchi, leo wanaitolea wapi jeuri kutoa ufadhili wa kijeshi kwa Israel kuwauwa wananchi?

Leo mamia ya wahamiaji wakiafrika wanakufa baharini na kutoswa pindi wanapojaribu kuitafuta hiyo inayoitwa amani
Nchi kama Libya haikuwa na wakimbizi ila baada ya kuuwawa kwa Muamar Gadafi aliyekua Raisi wao tulilishuhudia mamia ya wakimbizi wa kivita wa Libya wakifa baharini,kamwe hawakuwahi kupewa hadhi kama ile hadhi wanayopewa leo wakimbizi wa Ukrain

Muafrika huna haki ya kumcheka muarabu kwasababu hadhi yenu ni moja nyote ni daraja la pili la watawaliwa,vita yoyote inayotokea duniani tuombe salama na haki sawa kwa kila upande,haiwezikuwa sawa nchi yenye vikosi na sehem yenye tu wanamgambo

Nalaani ulimwengu kugawanywa matabaka mawili baina ya wenye haki na wale wanaopaswa kufanyiwa ihsani
Hatupongezi mauaji ila tunahitaji dunia imzingatie kila aliye na haki,kuruhusu mmoja apate msaada na mwengine anyimwe usaidizi huko ni katika ile nadharia ya walio bora ni wamagharibi na walio dhalili ni ulimwengu wa waarabu na waafrika.
 
Back
Top Bottom