Ziara ya Rais Samia nchini Ufaransa neema kwa Watanzania

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Na Mwl Udadis

Moja ya mambo yanayomfanya Rais Samia Suluhu kuwa kati ya viongozi wenye ushawishi mkubwa ni uwezo wake kiuongozi. Katika kipindi kifupi ameweza kuimarisha Diplomasia na kurejesha hadhi ya Tanzania kimataifa.

Mpaka sasa haya ni baadhi ya mambo yaliyofanyika katika ziara yake nchini Ufaransa;

1. Utiaji saini wa mikataba sita ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ufaransa, nchi hii iliyopo magharibi mwa Bara la Ulaya inakadiriwa kuwa na pato ghafi(GDP) ya zaidi ya USD Trilioni 2.6 hivyo mikataba hii itafungua fursa kubwa ya biashara na uwekezaji.

2. Kufanikisha upatikanaji wa fedha kiasi cha takribani Euro milioni 178 kwaajili ya UJENZI WA MRADI WA MWENDOKASI (BRT) AWAMU YA TANO. Awamu ya tano ya BRT inalenga kulifanya Jiji la Dar es salaam kuwa kati ya miji bora Afrika yenye miundombinu inayovutia uwekezaji.

3. Kufanikisha upatikanaji wa fedha kiasi cha takribani Euro milioni 80 kwaajili ya kuimarisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). Kilimo ndio uti wa mgongo wa watanzania, hivyo kete hii muhimu itakwenda kumgusa kila mtu kwa namna yake.

4. Makubaliano ya Tanzania na Ufaransa kushirikiana katika uchumi wa buluu na usalama wa bahari. Ufaransa imeendelea mno kwa teknolojia hivyo makubaliano haya yatasaidia maeneo ya bahari kuwa yenye tija na kuchangia pato la Taifa.

5. Kutembelea na kufanya mazungumzo na waendeshaji wa kituo cha wabunifu na wafanyabiashara wa Startup F facility kilichosheni fursa mbalimbali. Ili kunufaika na mapinduzi ya nne ya viwanda (4IR) lazima kujenga mahusiano na vituo kama hivi, tutarajie mengi katika ziara hii.

Rais Samia Suluhu anatekeleza sera ya diplomasia ya uchumi kwa vitendo, licha ya kuwa na muda chini ya mwaka mmoja tangu awe Rais wa JMT, tayari ametoa tumaini na dira ya serikali anayoiongoza.

#SisiTumekubali #kaziinafanyika
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Mikataba ingekuwa inawekwa mezani nasi wengine tuione maana mingi imesainiwa huko nyuma na mkwere ina maumivu makali
 
Acha UCHAWA, kwani huyu Raisi ndiye wa kwanza kwenda Ufaransa au ndiyo tumepata Uhuru mwaka huu?
 
Magu alitumia siku moja kwenda na kusaini mkataba south africa kusini na kurudi.
 
tuwe makini na wafaransa na project zao... hawakawii kutudai hawa..
 
Na Mwl Udadis

Moja ya mambo yanayomfanya Rais Samia Suluhu kuwa kati ya viongozi wenye ushawishi mkubwa ni uwezo wake kiuongozi. Katika kipindi kifupi ameweza kuimarisha Diplomasia na kurejesha hadhi ya Tanzania kimataifa.

Mpaka sasa haya ni baadhi ya mambo yaliyofanyika katika ziara yake nchini Ufaransa;

1. Utiaji saini wa mikataba sita ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ufaransa, nchi hii iliyopo magharibi mwa Bara la Ulaya inakadiriwa kuwa na pato ghafi(GDP) ya zaidi ya USD Trilioni 2.6 hivyo mikataba hii itafungua fursa kubwa ya biashara na uwekezaji.

2. Kufanikisha upatikanaji wa fedha kiasi cha takribani Euro milioni 178 kwaajili ya UJENZI WA MRADI WA MWENDOKASI (BRT) AWAMU YA TANO. Awamu ya tano ya BRT inalenga kulifanya Jiji la Dar es salaam kuwa kati ya miji bora Afrika yenye miundombinu inayovutia uwekezaji.

3. Kufanikisha upatikanaji wa fedha kiasi cha takribani Euro milioni 80 kwaajili ya kuimarisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). Kilimo ndio uti wa mgongo wa watanzania, hivyo kete hii muhimu itakwenda kumgusa kila mtu kwa namna yake.

4. Makubaliano ya Tanzania na Ufaransa kushirikiana katika uchumi wa buluu na usalama wa bahari. Ufaransa imeendelea mno kwa teknolojia hivyo makubaliano haya yatasaidia maeneo ya bahari kuwa yenye tija na kuchangia pato la Taifa.

5. Kutembelea na kufanya mazungumzo na waendeshaji wa kituo cha wabunifu na wafanyabiashara wa Startup F facility kilichosheni fursa mbalimbali. Ili kunufaika na mapinduzi ya nne ya viwanda (4IR) lazima kujenga mahusiano na vituo kama hivi, tutarajie mengi katika ziara hii.

Rais Samia Suluhu anatekeleza sera ya diplomasia ya uchumi kwa vitendo, licha ya kuwa na muda chini ya mwaka mmoja tangu awe Rais wa JMT, tayari ametoa tumaini na dira ya serikali anayoiongoza.

#SisiTumekubali #kaziinafanyika
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Neema gani wakati huko west africa nchi zote zilizotawaliwa na wafaransa bado anazinyonya mpaka leo. Mfaransa ni kupe sana ananyonya hadi uroto
 
Kujivunia kukopa ni mambo ya Ajabu (Mikopo inakuja as a last resort na ukikopa sio Majivuno)

Cha kujivunia ni unachotenda baada ya Kukopa na Bora zaidi kama unaweza kutenda bila hata kukopa..., Sana sana wa kuwapongeza ni hao watakaorudishwa / daiwa hio Mikopo...., Tusipoangalia tutaanza kupeana Kongole kwa Kupumua...
 
Mnakwenda ulaya kuomba hela huku nyuma mmeacha dhahabu na tanzanite.

Tanzanite inachotwa na Kenya.

Dhahabu na Almasi hazina mwenyewe.
 
Back
Top Bottom