Swali la kujiuliza, ni juhudi zipi zimefanyika kuhakikisha Gesi yetu imesambazwa kwanza kwa viwanda vyetu vya ndani na kutosheleza mahitaji yetu ya ndani??
Jibu ni rahisi sana, hakuna kilichofanyika. Hii maana yake ni kwamba Gesi yetu itawanufaisha zaidi Wakenya kuliko sisi Watanzania. Ni kama vile madini yetu ya Tanzanite yalivyoinufaisha Kenya na India.
Viongozi wa hii nchi sijui ni nani aliyewaroga. Hawana akili za kufikiri, hawana maono, hawana mwelekeo. Yule Mwendazake, unaweza sema labda, lakini na yeye alikuwa wale wale, mfano, kupoteza mabilioni kwenye midege isiyokuwa na faida.
Nionavyo mimi huyu SSH atakuwa Rais mbovu kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya Taifa hili. Tusubiri tutaona mengi. Time will tell.