Ziara ya Rais Kikwete Mkoani Tabora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ziara ya Rais Kikwete Mkoani Tabora

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MegaPyne, Oct 27, 2008.

 1. MADAI YA MALIPO YA WALIMU NCHINI

  JK: Ama hatuna ufanisi kabisa
  ama tumekuwa wadanganyifu

  Na Mwandishi Maalum, Tabora

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa madai yasiyoisha ya malipo mbalimbali ya walimu nchini yanathibitisha kuwa baadhi ya viongozi ama wana ukosefu wa kiwango kikubwa cha ufanisi ama ni wadanganyifu.

  “Ama sisi viongozi ni wakosefu wakubwa wa ufanisi –grossly incompetent – ama na sisi tumekuwa wadanganyifu - we have simply become cheats. Huwezi mwezi huu ukalipa kiasi cha sh bilioni saba, na miezi mitatu baadaye ukaletewa madai mengine ya sh bilioni 12. Haizekani madeni haya yakawa hayaishi. Hatuwezi kuendelea to run in circles kama wanavyosema Waingereza,” amesema Rais Kikwete.

  Ameelekeza Rais Kikwete: “Jibu la udanganyifu ni kupelekwa kortini na kufungwa tu. Jibu la kukosa ufanisi kwa mtumishi wa umma ni kuondolewa katika nafasi yake na akapatikana mtu mwingine wa kufanya kazi.”

  Rais ametoa ufafanuzi huo wakati anapokea taarifa ya utendaji ya Wilaya ya Tabora katika siku ya tatu ya ziara yake ya siku nane katika mkoa huo leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2008 mjini Tabora.

  Rais alikuwa ameambiwa kuwa walimu katika wilaya hiyo walikuwa bado wanaidai Serikali, hata baada ya kuwa baadhi ya madeni yao yamelipwa.

  Ilielezwa kuwa walimu katika wilaya hiyo bado wanaidai Serikali sh milioni 93 ikiwa ni posho ya likizo na za kujikimu, hata baada ya kuwa wamelipwa baadhi ya madai yao Machi, mwaka huu.

  “Kama nilivyosema juzi Sikonge nataka hili limalizike kwa kufanya ukahiki wa shule kwa shule, mwalimu kwa mwalimu, kichwa kwa kichwa, ili tujue nani hasa anadai nini. Baada ya kupata uhakika huo wale wanaodai tutawalipa, ili tuondokane na madai haya yasiyoisha.”

  Rais ameongeza: “Lazima tukate mzizi wa fitina. Nataka madeni haya yalipwe baada ya kuwa yamehakikiwa. Lazima tumalize misuguano hii. Mwezi Machi tumelipa sh bilioni saba, miezi mitatu baadaye tunaletewa madai mengine ya sh bilioni 12. Sasa nataka hili limemalizike kwa namna ya kudumu,” amesema Rais.

  Rais ambaye ameonekana kukerwa na hali hiyo amesisitiza: “Sasa mwezi Machi tulilipa nini? Hata nyie kama viongozi jiulizeni. Tulimlipa nani, kiasi gani na kwa nini?. Hatuwezi kuendelea na biashara hii bila kuifikisha mwisho.”

  Kuhusu malalamiko ya uongozi wa wilaya hiyo kuwa hauna nafasi ya kutosha kujenga hospitali ya wilaya, Rais ameelekeza: “Nyie viongozi acheni kulalamika na kunung’unika. Fanyeni uamuzi. Ama jengeni hospitali ya wilaya katika eneo la wilaya jirani ya Uyui, ama jengeni mjini kwa kupandisha ghorofa kama hamnayo ardhi ya kutosha.”

  Rais alikuwa ameambiwa kuwa uongozi wa wilaya hiyo unataka kujenga hospitali ya wilaya, lakini hauna ardhi ya kutosha kuweza kujenga hospitali yenye hadhi hiyo.
   
 2. Mishahara midogo itawazulia migogoro na wafanyakazi wenu, Rais awaonya waajiri

  Na Mwandishi Maalum, Tabora

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonya kuwa tabia ya baadhi ya waajiri nchini kuwalipa mishahara kidogo wafanyakazi wao itazua migogoro kati yao na wafanyakazi wao.

  Amesema kuwa ni jambo la kushangaza kuwa waajiri wanawakabidhi wafanyakazi mashine za mamilioni ya fedha, ili wazilinde na kuzitumia, lakini wakati huo wanawalipa mishahara “kiduchu”.

  Rais Kikwete ametoa onyo hilo leo, Jumapili, Oktoba 26, 2008 wakati alipokagua kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha New Tabora Textille Mills cha mjini Tabora, na kuzungumza na wafanyakazi na uongozi wa kiwanda hicho, katika siku ya nne ya ziara yake ya siku nane mkoani Tabora kukagua shughuli za maendeleo.

  Rais Kikwete ameuambia uongozi wa kiwanda hicho: “Ni jambo gumu kidogo kueleweka hili. Mnawakabidhi wafanyakazi wenu mashine na mitambo ya mamilioni ya fedha, lakini bado mnawalipa mishahara kiduchu.”

  Amesema Rais: “Msibane maslahi ya wafanyakazi. Mnaweza kuwalipa mishahara kidogo kwa muda, lakini hatimaye hili litawaingiza katika migogoro na wafanyakazi wenu wenyewe.”

  Hata hivyo, Rais ameusifia uongozi wa kiwanda hicho kwa kuonyesha mfano wa nini kinatakiwa kufanywa na viwanda vya nguo nchini.

  “Nashukuru na kuwapongeza sana kwa sababu nyie mmeonyesha mfano. Tusiishie kwenye kuchambua pamba tu, tusiishie kwenye ginnery tu. Hatua inayofuata sasa ni kutengeneza nyuzi na hatimaye kutengeneza nguo hapa hapa nchini,” amesema Rais na kuongeza:

  “Kwa sababu tunaposafirisha na kuuza pamba nje, tunachofanya ni kumpelekea malighafi mwenye kiwanda kama hiki hiki cha hapa.”

  Amesisitiza Rais Kikwete: “Tusijisifie kwa uhodari wa kuwa na viwanda vingi vya nguo na kuuza pamba yetu nje ya nchi. Tuanze sasa safari ya kutengeneza nguo. Lazima tuongeze thamani kwenye malighafi yetu. Nyie mnajua kuwa kilo mbili tu za pamba zinatengeneza shati moja?

  Uongozi wa kiwanda umesifia sera za ubinafsishaji na kusema kuwa bila sera hizo, kiwanda hicho kingeendelea kufungwa hata kama mpaka sasa kinazalisha kwa asilimia 50 tu ya uwezo wake.

  Kiwanda hicho kilichojengwa mwaka 1981 kikiwa kiwanda cha umma, kilifungwa mwaka 1981 kutokana na matatizo ya menejimenti. Hakikufunguliwa tena hadi mwaka 2004, kiliponunuliwa na watu binafsi.

  Tokea wakati huo zaidi ya dola za Marekani milioni tatu zimewekezwa katika kiwanda hicho ambacho kinaajiri watu 355 ambao wanafanya kazi kwa shifti tatu. Kiwanda hicho kinatumia kati ya marobota 900 na 1,000 ya pamba.

  Mpaka sasa kiwanda hicho kinasafirisha nyuzi kwenda Italia, Ureno, Uturuki, Colombia na China. “Tunaishukuru Serikali kwa kutuwekea mazingira mazuri yanayotuwezesha kuendelea na uzalishaji katika kiwanda chetu.

  Baadaye leo, Rais amezidua mradi wa josho na lambo la maji kwa ajili ya binadamu na mifugo na hata kufungia samaki katika kijiji cha Imalamihayo, nje kidogo ya mji wa Tabora.
   
 3. USHIRIKISHWAJI WANANCHI KATIKA KUIBUA MIRADI YA MAENDELEO

  Viongozi msikwepe wajibu wenu – Rais Kikwete


  Na Mwandishi Maalum, Tabora

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa utaratibu wa kuwashirikisha wananchi katika kubuni na kuibua miradi mbali mbali ya maendeleo usitumiwe na viongozi kama kisingizio cha wao kukwepa wajibu wao wa kuwa chachu ya maendeleo katika nafasi zao za uongozi nchini.

  “Hii tabia ya viongozi kudai kuwa wananchi hawajaibua miradi sasa inatumiwa na sisi viongozi kukwepa majukumu yetu kama wakala wa mageuzi ya maisha ya wananchi nchini,” Rais Kikwete amewaambia viongozi wa Wilaya ya Tabora leo, Jumamosi, Oktoba 25, 2008.

  Rais ametoa maelekezo hayo kwa viongozi wakati akipokea taarifa ya utendaji ya Wilaya ya Tabora katika siku ya tatu ya ziara yake ya siku nane katika Mkoa wa Tabora wakati alipowasili mjini Tabora akitokea wilaya za Sikonge na Urambo.

  Amesisitiza Rais: “Hiki ni kisingizio tu cha sisi viongozi kukwepa wajibu wao. Mwananchi ambaye hajui aibue mradi gani wa jinsi ya kuleta mageuzi katika mifugo yake ataibua nini?”

  Ameongeza: “Hivi sisi viongozi tunatarajia wafanye nini wananchi? Kwa sababu hata hicho tunachodai hawajaibua miradi hawakijua. Na hawakijua kwa sababu hawajaelimishwa kiasi cha kutosha.”

  Rais ameonekana kukerwa na jitihada kidogo zinazofanywa na viongozi wa Wilaya ya Tabora katika kuleta mageuzi ya mifugo katika wilaya hiyo kwa kutumia utaalam wa kisasa wa uhamilishaji (artificial insemination).

  Ameambiwa kuwa wilaya hiyo imezalisha ndama 15 tu wa kisasa katika jitihada za kuleta mageuzi katika sekta hiyo kwenye wilaya hiyo yenye ngombe majike 990 na madume ya kisasa 10 kwa ajili ya kuzalisha ng’ombe bora na wa kisasa zaidi.

  “Hii haiwezi kuwa taarifa ya wilaya nzima. Inaelekea jambo hili la kuleta mageuzi ya mifugo halina maana wala uzito kabisa kwetu. Hii haiwezi kuwa taarifa ya wilaya yenye heshima. Hamwezi kumdanganya mtu yoyote kuwa nyie mko makini katika jambo hili. Nyie hampo kabisa katika shughuli hii.”

  Ameongeza Rais Kikwete: “Hii dhana ya kushirikisha wananchi katika kuibua miradi yao ya maendeleo haina maana ya kuondoa wajibu wenu kama viongozi. Ni sawa na watu kuwa wanakufa kwa kiu ya maji, na nyie mnadai kuwa wananchi hawajaibua miradi ya maji, mnasubiri tu wananchi wabuni miradi ya kujiongezea maji. Nyie mnafanya nini?”

  Rais ameonya kuwa viongozi wasiichukue dhana ya wananchi kuibua miradi yao, kama kisingizio cha viongozi kukwepa majibu na wajibu wao.

  “Kwenye dhana nzima ya ushirikishwaji wa wananchi katika kuibua miradi yao ya maendeleo, ni lazima kiongozi awe wakala na chachu ya maendeleo.Kazi yenu ni kuwashawishi wananchi watambue umuhimu wa mabadiliko, na wala siyo nyie kusubiri wananchi waibue wenyewe miradi ya maendeleo.”

  Rais amesisitiza, “msichukue dhana ya kushirikisha wananchi kama kisingizio cha nyie kukwepa majukumu na wajibu wenu wa uongozi.”

  Kuhusu mikopo ya uwezeshaji chini ya mpango wa “Mamilioni ya JK”, Rais Kikwete ametaka viongozi kudai taarifa kutoka kwa taasisi mbali mbali zinazokopeshwa, ili wajue kama kweli mpango huo unawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.

  “Daini na kupata taarifa, ili sote tujue kama waliokopeshwa ni wahitaji wa kweli, kama kweli wamekopeshwa, kama maisha yao yameanza kubadilika kusudi tuwe na uhakika wa manufaa ya jambo hilo,” amesema Rais wakati anapokea taarifa hiyo.

  Kauli yake ilifuatia malalamiko ya viongozi wa wilaya kuwa wamekuwa hawapewi taarifa za utekelezaji wa mradi hiyo na taasisi za fedha zilizopewa fedha hizo za Serikali kukopesha wananchi.

  Kuhusu albino, Rais amesema kuwa matatizo yao ya sasa ya kusakwa na “watu wajinga” kwa maana ya kujinufaisha kibiashara, yasitumike kuwatenga albino kutoka katika jamii.

  “Tusiwatenge, lakini tuendelee kuwalinda mpaka wimbi la sasa la kuwashambulia litakapopita kwa sababu hilo ni wingi tu la kupita tu. Hawa wajinga wakiona kuwa vidole na nywele za albino hazileti utajiri, wataacha tu,”amesema Rais.

  Alikuwa akitoa maelekezo baada ya kuwa ameambiwa kuwa watoto albino katika wilaya hiyo wanasoma katika shule za walemavu wa kuona na kusikia katika wilaya hiyo.

  “Tusiwatenge. Kwa sababu kwa kufanya hivyo, tutawatia hofu zaidi,” ameeleza Rais kabla ya kuambia kuwa wanafunzi hao wamewekwa katika shule hizo kwa sababu ya udhaifa wa kuona.

  Kabla ya kuwasili mjini Tabora leo, Rais ametembelea Wilaya ya Urambo ambako ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki na kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Urambo.

  Baadaye alikwenda katika Jimbo la Uchaguzi la Urambo Magharibi ambako amefungua mradi wa maji kwa ajili ya mji wa kijiji cha Kashishi na kuzindua shule ya sekondari ya Kashishi.
   
 4. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #4
  Oct 27, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  ..hivi ziara imeshaisha au inaendelea cos muhashimiwa amerudi dar leo jioni...!
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tunaweza kupiga kelele za ufisadi kila siku hapa, lakini hatari kubwa zaidi iko kwenye lack of capacity kwa watendaji hasa kule kwenye ngazi za wilaya na mikoa.

  Mabilioni yanapotea kwa kukosa ubunifu pamoja na ufisadi. Sijui tufanyeje?
   
 6. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Jamani hawa watu naona hawamwambii ukweli mkuu wa kaya, hizi pesa zinazotolewa haziwafikii walimu zinaishia mifukoni mwa maafisa wa elimu na wahasibu wao, miaka yote thats what happens, ndio maana madai hayaishi kila siku.
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Mh Rais na yeye akipatia pahala pake basi inakuwa burdaani kweli.
  Naona huko Tabora anaongea sana...Huko ndio CHADEMA wanaendelea na operation yao Sangara ambayo nadhani wameisimamisha kutokana na uapisho wa Mh to be Mwera huko bungeni.

  JK na yeye naona yuko hapo nyuma yao tu...Sijui kama na Tarime ataenda ama la..Ila ni wazi kuna mikoa anayoipenda zaidi kutokana na hospitality nk.

  Tunaomba wale wenye taarifa watuwekee hapa kama na huko Tabora analala kabla ya giza ama kama mambo ni mswanu tu.

  Hayo lazima ni maeneo ya kujidai ya Mh Rais.

  Kaazi kweli kweli.
   
 8. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #8
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Moja ya kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi hii ni wilaya na halmashauri kushindwa kutekeleza majukumu yake. Wilaya hazina wataalamu, wilaya zinamwagiwa fedha nyingi za miradi mbali mbali lakini tatizo kubwa limekuwa ni utaalam na ubunifu.

  Watu wengi hawapendi kufanya kazi wilayani. Wasomi wengi wamerundikana Dar tu na sehemu nyingine za miji mikubwa.

  Katika shughuli zangu mara nyingi huwa napita katika hizi ofisi za wilaya. Watu hawafanyi kazi kabisa. Saa nne utakuta watu wanapiga story tu nje za ofisi wanasubiri kulipana posho n.k. Inapotokea kuwa kuna kiongozi anakuja ndo wana aandaa taarifa haraka haraka kwa ajili ya kiongo.

  Tuondoe wataalam waliorundikana kwenye mawizara. Tuwapeleke wilayani wafanye kazi. Otherwise tutakuo tuna zunguka tu kwenye circle. Bahati mbaya sana JK haambiwi ukweli, maana taarifa nyingi ni za kisiasa na zinazolenga kuonyesha kuwa mambo yanaenda wakati hayaendi. Ni lazima Raisi awe na mfumo wa utakaomwezesha kupata taarifa za kweli na kwa wakati muafaka. Hizi taarifa za wilaya na taasisi nyingine lazima zihakikiwe kabla ya kufikishwa kwa raisi.

  Marekani wana ofisi/kitengo maalum kwa ajili ya kuchambua na kufanya tathmin ya utendaji wa vitenfo na wakala na ofisi zote za serikali. Ofisi hiyo inaitwa GAO - General accountability ofisi. Kwa kupitia ofisi hii bunge na raisi wanapata taarifa sasa. Hawezekani wakuu wa wilaya na viongozi wengine wakajitengenezea taarifa chafu. Ni lazima waandike taarifa ya kujisafisha tu hata pale ambapo mambo hayaendi vizuri.

  Taarifa zote za serikali ni lazima zihakikiwe kabla ya kuwa taarifa rasmi. hii ni pamoja na taarifa za utekelezaji za mawizara na wakala mbalimbali.

  Bahati mbaya sana Auditing yetu inalenga kwenye matumizi ya fedha tu. Utaratibu umefuatwa na kuna risiti basi, mtu anapewa hati safi. Auditing inabidi iende mbali zaidi ikiwa ni kuangalia thamani ya pesa na kazi halisi pamoja na ubora wa kati au product. Pia ni lazima iangalie pia kama lengo la kazi hiyo limefikiwa au la. Tukifanya hivyo tutakuwa katika nafasi nzuri ya kuleta maendeleo ya kweli. lakini hizi kelele za JK anapoenda ziarani ni kama kelele za mbwa tu asiye na meno. akiondoka tu watu wanaendeleza libeneke lao kama kama kawa
  .

  Kuhusu madai ya walimu kama ilivyo kwa madai ya wafanyakazi wa iliyokuwa Jumuiya ya Africa Mashariki, kuna mchezo ndani yake unafanywa.
   
 9. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kama ni Rais tuu awamu hii tumepata.
   
 10. K

  Kigoma Member

  #10
  Oct 27, 2008
  Joined: Jul 10, 2006
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hiyo ziara haijaisha.....kwa mujibu wa ratiba ya ziara yake....anaelekea Sauzi kesho kuhutubia bunge la huko halafu atarudi Tabora kumalizia ziara.

  HabariLeo: Gwiji la habari Tanzania | Kikwete aanza ziara Tabora
   
 11. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Busy for nothing at all
   
 12. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #12
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heheeee! Amekuwa kama Zumbukuku! Yaani hajui hata aanzie wapi, naona sasa amemuiga Pinda kupiga mikwara.
   
 13. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Has Kikwete gone insane or has early stages of Dimentia?

  Maana he sounds like he is talking to himself and addressing himself. Anasema Viongozi wawajibike, waajiri wasilipe mishahara midogo, sounds like the problem with his leadership and management!

  Ustaadh MegaPyne, shukranimkubwa na pole kwa safari na mengineyo!
   
 14. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Si ndio hapo Rev, yaani kama nchi ingekuwa ni kampuni na Chief Mwankupili angekuwa CEO ingekuwa imeshafilisika, yaani na yeye anauliza? sasa sijui wakuu wa mikoa, wilaya na viongozi wengine wanafanya nini? jamaa kawa hopeless. kazi kuongea tuu.
   
 15. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #15
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kandoro astukia taarifa nzuri za ujenzi wa shule Kinondoni

  2008-10-25 20:23:33
  Na Sharon Sauwa, Mbezi Beach

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bwana Abbas Kandoro, amesema amebaini kuwa taarifa alizo nazo juu ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa shule kwenye Manispaa ya Kinondoni si za kweli kwani vuguvugu la ujenzi wa madarasa liko katika shule chache huku nyingine zikikosa mwamko huo.

  ``Nimebaini kuwa ni shule mbili tu zilizo na vuguvugu, lakini katika shule nyinginezo, kama lipo basi ni la siku hiyo hiyo moja,`` akasema.

  ``Nina uhakika kuwa kama nikienda hivi sasa, siwezi kuwakuta wakiendelea na vuguvugu hilo la ujenzi,`` akasema Bw. Kandoro wakati wa majumuisho ya ziara yake ya siku tatu ndani ya manispaa hiyo.

  Mkuu huyo wa Mkoa akasema amesikitishwa na ushiriki wa wananchi katika kuchangia ujenzi wa shule na kuwataka washiriki kwa ukamilifu katika ujenzi huo.

  Akasema Wilaya ya Kinondoni ina wanafunzi wengi ambao wanatakiwa kuingia katika shule za sekondari na hivyo njia pekee ya kuepuka tatizo la kukosa nafasi kwa wanafunzi ni kujengwa kwa shule hizo.

  Kuhusiana na ujenzi wa zahanati, Bw. Kandoro akaipongeza manispaa hiyo kwa wazo la kujenga nyumba za waganga katika zahanati mpya zinazojengwa.

  Akasema mpango huo utasaidia wananchi kupata huduma kwa saa 24 badala ya kuzisubiri wakati wa mchana pekee.

  ``Pale Msumi na Wazo, Kwembe Mpakani nimefurahishwa sana na ushiriki wa wananchi katika suala la uchangiaji,`` akasema Bw. Kandoro.

  Akaongeza kuwa uchangiaji wa wananchi utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukamilisha miradi hiyo.

  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF, unachangia asilimia 80 ya gharama zote za miradi ya zahanati iliyoibuliwa na wananchi huku asilimia 20 huchangiwa na wananchi.

  Hata hivyo, kamati za ujenzi wa miradi hiyo zimekuwa zikilalamika juu ya kupanda kila mara kwa gharama kunakotokana na kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi.

  Akielezea juu ya malalamiko ya kamati za ujenzi wa miradi kuhusiana na gharama zinazopaa kila kukicha, Bw. Kandoro akawataka wananchi kushirikiana na manispaa katika kuwezesha kupatikana kwa kiasi cha ziada cha kumudu gharama hizo.

  Aidha, Bw. Kandoro akachangia mifuko 20 ya saruji kwa kila zahanati ambayo aliridhishwa na utekelezaji wa mradi wake.

  * SOURCE: Alasiri
  Haya ndo nilikuwa nasema, Taarifa nyingi wanazopewa viongozi wa ngazi za juu, siyo za kweli. Na hili ni tatizo kubwa
   
 16. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Hivi hana kazi za kufanya ofisini kwake? Maana haya masafari yasiyokwisha kama kuna IN TRAY yenye mafaili basi yanakaribia kufikia urefu wa PPF tower!!!!!
   
 17. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Ni vyema nikueleweshe kuwa maafisa elimu huzisikia tuu fedha hizo.malipo yote ya waalimu pamoja na mishahara hupitia halmashauri za wilaya huko ndiko kwenye matatizo maana madiwani wanaweza kubadilisha matumizi ya fedha hizo au kulipa waalimu bila kuweka kumbukumbu kwenye files za waalimu ambazo ziko idara ya elimu.Ndipo hapo tatizo lilipoanza wengine wamelipwa lakini idara ya elimu haina kumbukumbu.kinachofanyika sasa ni kupitia orodha ya kila mlipwaji kutoka kwenye fungu hilo il kuoanisha na kumbukumbu za idara ya elimu na chama cha waalimu
   
 18. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tatizo kubwa hapa ni ufuatiliaji wa karibu katika utendaji.
  Serikali kama ilitoa pesa sh bil saba kwa ajili ya malipo ya waalimu kwa wilaya husiika je ilifuatilia kuona kwamba waalimu husika wamelipwa kabla ya kutoa tena sh bil 12 kwa kitu kile kile?. Wahusika na upokeaji na ugawaji wa hizo pesa ni akina nani na wana elimu husika na pesa ama ni vihiyo?.

  Kwanini viongozi wasiige utendaji wa marehemu Edward Moringe Sokoine katika ufuatiliaji wa masuala wanayoyatolea amri?
   
 19. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2008
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
   
 20. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nafikiri lengo lake ni kuimaliza mikoa yote aweke historia ya kipekee kwa kuwalaghai wananchi wa vijijini.This is another way of kampeni si mwaka huu mawaziri hawajafafanua bajeti?
   
Loading...