Ziara ya Obama; Kenya wazidi kuitenga Tanzania, waishawishi Burundi kujiunga G4

Tanzania tuna nafasi kubwa sana ya kuendelea kama tutaondokana na ubinafsi na kuchagua viongozi makini wenye nia thabiti ya kuiendeleza hii nchi na kuondokana na mikataba yote laghai, Sio tu EAC bali Afica kwa ujumla na Dunia itatambua.
 
Mimi nawafagilia sana wakenya maana wazungu walipofika hapo kwa ajili ya kuwekeza, waliambiwa hamna haja ya kufanya uchunguzi wa madini tutawaonyesha yalipo ila shea ni pasu pasu, wazungu wakaimbia, hapa bongo walipofika wazungu kwanza walijifanya kama hawana taarifa kuwa nchi hii imetapakaa madini basi wakawaambia viongozi wetu tunaomba muda wa miaka mitano kufanya uchunguzi, wakachimba madini mpaka wanakaribia kumaliza ndio wanaiambia serikali njooni tujadiliane sasa tutalipana vipi, Wakenya wanatuhurumia kwa matatizo tunayojiongezea
 
wakenya wana roho mbaya sana nimepata bahati ya kukutana nao katika mambo mengi kama masomo,michezo nilipokuwa chuoni huko kwao na nchini uganda na hapa nchini jamaa wanaroho mbaya na wakabila wakuu mkenya sio mwenzako najua kwa akina raila na wajaluo na ODM wamechukulia hii kama ushindi kwao ila kwa PNU ndio wanaweweseka alah

Wanaitwa UHURUTO hawa ndo wamenuna balaa.
 
Na bora East Africa Community ife tu. hii community Wakenya wanaing'ang'ania sana. Wana roho mbaya sana Kenyans
 
uyo anayewaza 'blueband' sinahakika kama anaelewa 2nakizungumzia humu ndan, ajipange. Tena nae akitaka ajitenge nas kam g3 walivyofanya
 
Mimi niko nao huku Kenya wajamaa kiukweli roho zao si nzuri ukabila bado upo just imagine hata uchaguzi wa serikali ya wanafunzi wanachagua wenzao,mtanzania alikuwa anagombea U Vice kapigwa chini mbaya eti hawawezi kuwapa Watz kuwatawala
 
Hivi tukiwekeana Vikwazo vya kibiashara kati yetu na Wakenya nani ataathirika zaidi? maana huku kuzorota kwa mahusiano kumeanza kunitisha
 
Kama ni kweli utakuwa wivu wa kijinga kwani Tanzania ni taifa lenye uhuru kamili na pi ni ruksa kuendesha mambo kwa uhuru. Pia kama kuna mtu wa kumwekea bifu ni obama na si Tanzania au JK
 
Nani anakuanganya? Hata blue band unayotumia ni made in Kenya. Nitajie watanzania watatu tu wenye investment za maana Kenya
Duh uko mbali kweli wewe unaijua TANBOND? Museveni anataka kubaki madarakani hata huyo Kony kamtengeneza mwenyewe ndio mana ile operation yao na US imesitishwa baada ya wazee kugundua ni danganya toto, Kagame mlisha msema sana humu hata kwenye Genocide yenyewe ana mkono wacha ya DRC, kuhusu Uhuru, Obama waziwazi utawala wake haukutaka ashinde uchaguzi na meseji aliituma kwa wananchi wa kenya na bado icc inamsubiri wanahisi wako vulnerable for anything, wanajilinda, bado kuwaita wajinga sidhani kama ni sahihi si wana wananchi wao, wataamua, ukweli bila TZ jumuhia hiyo haitadumu hata mwaka mmesahau majeshi ya kagame na museveni yalivyochapana kule kongo? ilikua ni nini? almasi?
 
Siyo ivo tu! Nimetazama BBC Mfanyabiashara wa kenya anasema alialikwa na Obama na hajaja kwa kuwa Wakenya wamefedheheshwa na Wao sio ombaomba.

Intake
Wakenya wameanza kuiogopa tz? Wakenya fakunana sana.
waigope tz kwa lip.......
 
Mkuu Albedo umemjibu huyo jamaa vizuri na kwa mfano mfupi tu,nilichojifunza watu wanapenda kuropoka tu,pasipo kuwa na ufahamu wa mambo,wakenya kwetu ni potential sana katika mstakabali wa bidhaa zinahitajika ktk maisha yetu ya kila siku,tuna vitu vingi sana pia tunategemea kutoka kwao
Shilingi 1000 ya KENYA ni Shilingi 19200 ya Tanzania.wako mbali sana.Tatizo wezetu wana aina ya Viongozi wa kuiendeleza nchi yao sisi tuna Viongozi wanaoididimiza nchi yetu.ndiyo maana tunarasili mali nyingi kuliko wakenya lakini wakenya wanatumia vizuri kidogo chao,Ndiyo maana wanatuzidi.
 
Nawakubali sana Wakenya
Tulishambwambia Kikwete hatuwataki MANYANG'AU kwani walishatuliza sana sasa yanatukuta
Kenyatta wakati anagombea kakanyaga sana, kuomba msaada leo anataka tumsaidie asishtakiwe the HAGUE
Museveni kakulia na kusomea Tanzania lakini hafai kwani anataka kuwa Rais wa Jumuia ya Afrika Mashariki
Kagame ndio kabisa hafai hata kushirikiana naye
leo ndio waichukue na Burundi kweli KUVUJA KWA PAKACHA nafuu kwa TANZANIA
Jinsi walivyovamia ardhi yetu na nafasi za kazi (mf Mahotelini, vyombo vya habari nk)
View attachment 100485 View attachment 100485View attachment 100485View attachment 100485View attachment 100485
watatukana saaaana
 
Hayo ya kwao ni ccm ndiyo waliokuwa wanampigia debe Kenyatta ashinde, kasoro Magufuli aliyejibambanua wazi kuwa upande wa Odinga, watavuna walichokipanda


Hili suala ni zaidi ya vyama, jaribu kuongeza upeo wa kufikiria kidogo.
 
Mkuu Riwa asichokijua Albedo ni kwamba soko la bidhaa za Kenya Tanzania ni kubwa sana siku tukiamka tukazizuia bidhaa za Kenya watafunga viwanda vingi.Marekani inatoa heshima kubwa kwa nchi ya China kwasababu ya soko kubwa walilonalo China.Tanzania ni nchi ya pili kwa kununua bidhaa nyingi Kenya ya kwanza ni UK ipo Ulaya,viongozi wetu wakitumia nguvu ya soko,ukubwa wa ardhi na rasilimali kibao zinazowaleta viongozi wa mataifa makubwa Tanzania kila wakati ni wazi kabisa Tanzania ni super power within EAC.


Wakenya wanasahau kua consumption ya bidhaa zao hapa nchini ni kubwa hata ukijumlisha burundi.rwanda na uganda. Tukifunga mipaka viwanda vingi vitafungwa hata zile ajira zao nyingi zilizopo hapa nchini zitakua hatarini.
 
tungekua hatuna direct gateway kama bandari wangetutesa sana lakini kwa sasa hata tukiwa na ushirikiano mzuri nao , je undhani kuna chochote cha kufaidi?, bora wajitenge watapunguza kutuibia, waende zao
 
Back
Top Bottom