Ziara kisiwandui: Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Daniel Chongolo azungumza na Wazee

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
668
836
Kisiwandui Zanzibar

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo Leo Julai 5, 2021 amekutana na Kufanya Mazungumzo na Wazee pamoja na Waasisi wa Chama Cha Mapinduzi katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, Kisiwandui.

Akizungumza na Wazee hao Ndg Daniel Chongolo ametoa Salamu za Shukrani toka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Samia Suluhu Hassan kuwashukuru wazee kwa Kuendelea kuisimamia Maadili katika jamii na kuwa mstari wa mbele kutoa Ushauri mbalimbali ndani ya Chama na Serikali.

Pia, ndg Chongolo amewaomba wazee hao kuendelea kuwa washauri kwa nyakati zote kwa Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee kusimamia dira ya Kuanzishwa kwake.

Aidha, akizungumza kwa Niaba ya Wazee hao Mwenyekiti Mwenyekiti wa Wazee wa CCM, Bi Khadija Jabir ameipongeza Sekretarieti ya CCM inayoongozwa na Katibu Mkuu Ndg Chongolo kwa kuanza kazi vizuri na ufanisi mkubwa wa Kuhakikisha Chama kinaendelea kuwa imara.

Chama Imara
Kazi Iendelee

IMG_20210705_210751_621.jpg


IMG_20210705_210751_625.jpg


IMG_20210705_210751_623.jpg


IMG_20210705_210751_622.jpg
 
Back
Top Bottom