Zengwe la madaktari bingwa na serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zengwe la madaktari bingwa na serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mayoscissors, Mar 4, 2012.

 1. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Pamoja na haya yanayoendelea, kuna waraka umetoka utumishi hivi majuzi kuzitaka hospitali
  na taasisi kutokuwatambua madaktari kama maspeshalisti mara baada ya kugraduate
  hadi pale ambapo serikali itaamua kuwatambua.Lengo la waraka huu ni kukwepa kulipa mshahara wa daktari bingwa.

  Pia haijulikani serikali itakutambua lini hata kama ni baada ya miaka kadhaa, hawajali. Mfano halisi ni kuwa wale waliomaliza postgraduate mwaka jana hawajatambuliwa hadi leo na wanafanya kazi kwa mshahara wa registral!

  Halafu baada ya kutambuliwa hakuna areas!!

  Naandika hili nikitumia mfano halisi wa Muhimbili!  Chanzo MAT
   
 2. B

  Bwanamdogo Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi naona hapo cha kufanya ni kutafuta kule watakako kutambua kuliko kuendelea kuhangaika na serikali ambayo kila kukicha inaonekana haina dhamira ya kuleta mabadiliko bali ni kudidimiza. Maana kama ni kugoma mtagoma mpaka mtachoka
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Sijui hawa viongozi wetu watasemaje, siku tukiwakamata na kuwafikisha mahakamani kwa kosa la kutumia vibaya madaraka na ofisi za umma! If I will be the head of the state, nikuwafunga tu pamoja na kuwafilisi. Mtanisamehe wanaJF, haiji akilini watu wanasota kutafuta hizi profession, harafu mtu anakuja from no where tena anishuledi anabwabwaja kana kwamba hii nchi ni ya wanasiasa peke yao.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tumejiruhusu wenyewe tuburuzwe na wanasiasa
   
 5. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Itafika kipindi fani ya udaktari itakimbiwa ss sijui tunaenda mbele au tunarudi nyuma mi siielewi hii serikali isiyo sikivu
   
 6. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Serikali legelege kila kitu inafanya usanii! Bila mashinikizo hakuna miujiza.
   
 7. MZEE WA ROCK

  MZEE WA ROCK JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 623
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  simshauli ndugu yangu yeyote aingie katik fani ya udactari waliopo wanatosha na shida zao
   
 8. N

  Njaare JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu si kwa madaktari tu ila kwa watumishi wote. Kuna waraka unaagiza maCEO kupunguza ajira na promotions. Pia anagalia hata standing order mpya inayotumika sasa jinsi inavyominya haki za wafanyakazi.
   
 9. m

  motonsebu Member

  #9
  Mar 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matunda ya kuwa na mzee wa kaya kilaza,na hili kulitolea maamuzi anataka akadese mahali.
   
 10. m

  mzizi dawa Senior Member

  #10
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  2na raic jina.
   
 11. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Unajua watu wanaona maDaktari hospitalini au mitaani wamevaa nadhifu au wanaendesha 'mikweche' yao wa 2nd and 3rd hand, basi watu wanadhani maDaktari wana maisha mazuri au ahueni kulinganisha na fani nyingine...ukweli ni kwamba, kwa Daktari ili aweze kuishi maisha hayo ya ahueni inabidi afanye kazi hospitali mpaka 3....mimi nilikuwa nafanya kazi Muhimbili, Tumaini na Regency ili kuweza kuwa na maisha ya angalau kwa familia yangu! Mtu mzima naacha mke na mtoto nyumbani nalala zamu za usiku kwa waHindi ili niweze kulipa kodi kwa decent house, nilishe familia yangu decent food, na angalau tuwe na kagari kafamilia (1996 Honda CRV)....Jamani daktari kweli mwenye Masters ya Surgery!?

  sasa mtu umesoma..umeongeza ujuzi kwa kusota miaka mi3 au mi4 kupata Masters ya specialization na serikali haitaki kukutambua for years na kukulipa stahiki zako, wakati majukumu yako yanachange immediately toka general practitioner to specialist pindi tu baada ya kumaliza Masters...na watakapokutambua waraka unatoka usilipwe arrears zako stahiki kwa kazi ambayo umeifanya katika capacity ya specialist! hapo hapo unasoma katika magazeti list za majina na lako likiwepo eti unahamishiwa kijijini huko kwenye hospitali isiyo hata na facilities za wewe kufanya kazi kama specilist (hata barua hupewi), na usipoenda unashitakiwa kwa wananchi kuwa 'eti hutaki kwenda vijijini kuwatibu'! Nyambaff...

  Wacha tu tugome bana...hata kama waTanzania mtatuchukia, lakini kama mnatuthamini mtatuunga mkono!
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwanini ni serikali inahitaji kuwatambua kuwa ni maspecialist? je MAT wanawatambua?
   
 13. S

  Silent Burner Member

  #13
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumechaoka, kila kukicha ni issues za maslahi ya madaktari.... kwani wao tu ndio muhimu jamani??

  Hawa wanataaluma wamegeuka wauaji, wanashabikia watu kufa. Wameshapoteza maisha ya wengi kwenye mgomo wao wa mwanzo lakini bado wana hamu ya kuondoa roho zingine. Wamenogewa kuua.

  Laana iko juu yenu, kwa kutanguliza ulafi wenu wa pesa na kupigania kushibisha matumbo yenu ....kwa kutoa kafara roho za binaadam wenzenu.
   
 14. m

  mariavictima Senior Member

  #14
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu ingilia kati. hali kwa kweli ni mbaya. Wape MOYO wa huruma serikali ishughulikie haya matatizo la sivyo itakuwa gharika kwetu.
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280

  Ukitaka kufurahia utumishi serikalini lazima ujiunge na zile idara au taasisi au wizara wanazosema ni nyeti ndo utachukuliwa unafanya kazi ya maana. Huo udaktari bingwa nani anautambua kama wagonjwa wetu wanatibiwa Apollo?
   
 16. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #16
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kwani MAT kazi yao kubwa ni nini sasa? ni vigezo vipi serikali itatumia kuwatambua madaktari hao? tatizo ni nini haswa? mishahara kuwa mikubwa nini? kwa hiyo hawahitaji mabingwa ili wawe wanaenda APOLLO?
   
 17. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimeshangaa kidogo....
  Common sense ilikua inanituma kuamini kuwa kama wahandisi wantambuliwa na ERB (T), wahasimu wanatambuliwa na NBAA, Wasanifu majengo na AQRB, wanna manunuzi wana bodi yao...madaktari wangetambuliwa na kitu kifananacho na hivyo. Serikali in wataalamu wa kutosha kuweza kuwatanbua na kuwa-approve madaktari huko wizarani du!

   
 18. d

  digodigo Senior Member

  #18
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wakati huo huo jamaa wa TRA kamaliza juzi tu chuo na hana muda mrefu kazini anakuwa na maisha mazuri kupindukia na hakustruggle kama wanavyohangaika madaktari je hapo kuna usawa? tutafika kweli?
   
 19. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Uko sahihi, lkn kwa kukumbusha; sikwamba wanaosoma fani nyingine tofauti na Udaktari wanakuwa hawajastruggle, kitendo cha ku-specialize kwenye fani fulani na akafiti kisawasawa ni juhudi za hali ya juu: na kila mtu anakuwa na interest zake hivyo tusiwabeze ambao hawakusoma udaktari, cha msingi tuangalie nini cha kufanya kuishinikiza serikali kutambua umuhimu wa watumishi wake kwa ujumla.
   
 20. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Sio tu ni kazi ngumu jamani hii kazi ina torture physical and pyschological aspects za wahudumu wa afya

  1. Pricks na zama hizi za HIV (Hata kama prophylaxis zipo)
  2. Kuona mgonjwa anakufa kwa kukosa dawa au vifaa tiba na ujuzi unao
  3. Sometimes unatoa pesa yako mfukoni kuokoa jahazi lisizame mgonjwa apate dawa
  4. Imagine in a night shift unawitness binadamu wenzako say watatu wanakata roho....hapo hata ukirudi nyumbani asubuhi unakuwa psychologically disturbed sana tu
  5. Mentioning just a few (ethics)

  I once experienced and attended a patient with a "third degree tear" kijijini, ambulance haina mafuta.....Tazara hiyo ndo mpaka itoke Zambia na express ishapita zake....cutgut zikaisha usiku wa manane in a midst of the procedure I had kuendeshwa kwa bicycle na mume wa mzazi kufuata nyingine ili kumalizia kushona. Will neva forget that night.... halafu mtu ukaongeze ujuzi kweli usitambulike (kama kweli waraka umetoka)

  Jamani mlio responsible please please hebu na mtende yaliyo muhimu ili kuwafanya wanaostahili kupata haki zao ili kuepuka kupoteza roho kama wakati wa mgomo wa kwanza...Chonde chonde
   
Loading...