Zelenskyy ashauriwe kwa manufaa ya Ukraine

Ungekuwa raia wa Ukraine na hakuna namna kabisa unaweza kuondoka nchini mwako katika hali yoyote ungemshauri nini Zelenskyy kama Rais wako kuhusu uvamizi wa Urusi kwa maslahi mapana ya nchi yako?
Mimi namwambia baba shikilia hapo hapo tu, tulipotoka ni mbali kulipo tunapoenda!! Na jamaa anaelekea kukata pumzi!!
 
Ungekuwa raia wa Ukraine na hakuna namna kabisa unaweza kuondoka nchini mwako katika hali yoyote ungemshauri au ungemtaka Zelenskyy kama Rais wako afanye nini kuhusu uvamizi wa Urusi kwa maslahi mapana ya nchi yako?
Wale waukraine(wananchi) ni tatizo,waligomea bidhaa za Urusi , Zelensky akiwaongoza kufanya hivyo.

Halikuwatosha Hilo,wakamwondoa Kwa maandamano kiongozi wanaedai ni kibaraka wa Urusi.

Nimekupa hii mifano uone tatizo ni Zelensky au wananchi.

Sasa hao wananchi wanaotaka Shari,watamshauri Nini?
 
Tulimshauri akakaza shingo... sasa hivi hakuna haja ya kumshauri acha atiwe adabu maana nchi yake sasahiv imechakaa kama tambaka la deki....
Mlishauri ushauri gani?
 
Wanachi kugomea bidhaa za Urusi na kumuondoa kiongozi waliyedai ni kibaraka wa Urusi inawahusu vipi Urusi?!
Hayo si mambo ya ndani ya nchi yao wenyewe??
 
Zelensky wewe ni shujaa, Russia hawezi kupora Crimea umuachie kisha atake apore na nchi yote aachiwe.

Vita si lelemama, atasikia mengi na kuona mengi ila endelea kupambana kijana.
 
Kuna kosa gani wananchi wa Ukraine kugomea bidhaa za urusi na kumuondoa madarakani rais waliyemuona ni pandikizi la Urusi kwa taifa hilo?
 
Mimi namwambia baba shikilia hapo hapo tu,tulipotoka ni mbali kulipo tunapoenda!!na jamaa anaelekea kukata pumzi,!!
Russia msimamo wao ni kuwa "hakuna maana ya dunia kuwepo kama Russia haipo". Hawa ni watu wasio na cha kupoteza. Bora mfe wote na wao ili mkose wote. Ni watu waliokata tamaa. Hakuna jinsi utamsinda umdhalilishe. Atakufa na wewe.

Cha muhimu Zelensky akae chini waelewane. Hii vita hawezi kushinda. Na NATO hawatakubali kushindwa, mwishowe Ukraini itakuwa sehemu isiyofaa kuishi wanadamu. Atakuwa amefanikiwa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…