Nadhani watu waache ushabiki usio na maana kwanza. Tujadili issues kuhusu hili.
Sheria za milki ubunifu zinaeleza wazi kwamba mtu anayetengeneza kitu kutokana na ubunifu wake ndiye mmiliki! Mara nyingi huwa mbunifu napoteza haki ya kutambulika kama mwenye 'mali' hiyo inayotokana na ubunifu kama ni mwajiri kwa maana kwamba kubuni vitu kama hivyo ni kazi yake na analipwa mshahara na mafao kwa kutenda kazi hiyo. Yatakiwa lakini kuwepo na mkataba wa ajira baina ya pande mbili. Hii kitaalamu inatokana na dhana kwamba mwajiriwa anakuwa anafanya kazi ile ili kutekeleza majukumu yake na kukidhi matakwa ya mwajiri kwa maana kwamba asingefanya hivyo basi asingekuwa na manufaa kwa mwajiri wake.
Kwa kuwa hakuna mtu awaye yote kati yetu anayejua kama hawa watu kwa mujibu wa makubaliano yao na EATV walikuwa waajiriwa au hapana, tuache ku-pass judgment kuhusu EATV. Yawezekana kabisa hawa vijana wamedanganywa wakadhani wanaweza kuondoka na kila kitu wakati mkataba wao unasema vingine.
Iwapo ,kwa mfano, EATV ndiyo walikuwa waanzilishi wa kipindi kwa ku-conceive idea na kui-translate na hawa vijana wakawa walitafutwa kufanya kazi tu kwa kuingiza kipaji chao tu, uwezekano ni mkubwa kwa EATV kuwa mmiliki halali.
Kwa upande mwingine, pamoja na kuwa ndugu hawa waweza kwa mujibu wa sheria kuwa wao ndiyo waandishi na watengenezaji wa scripts na kipindi chenyewe cha Ze comedy, wakati EATV wakiwapa airtime, studio na vifaa vya kurushia na kurekodia, inawezekana kabisa walikubali kwamba kwa vile wanatumia mali za EATV kutengeneza vipindi vyao then, EATV wapewe haki miliki wakati wao wakilipwa fees tu. Kama makubaliano yapo hivyo basi haki zote zinakuwa mali ya EATV by virtue of the transfer in lieu of the fees and other things.
Kwa hiyo , ni muhimu sana kufahamu makubaliano baina ya pande mbili kabla ya kurukia issue.
Hili ni suala la kitaalamu zaidi badala ya kiushabiki. Na si kila mwanasheria anajua sheria juu ya milki ubunifu, kwa Tanzania bado wapo wachache sana ukilinganisha na mahitaji.
nafahamu kuna bush lawyers wengi sana wanaojifanya wanajua hii sehemu ya sheria, ila hawajui, na kwa kuwapa dondoo kidogo tu, advocate SWAI atachemka na vijana wanaweza kujuta kwa nini walimchukua kama wakili wao.