Zao la Kahawa kuwapatia utajiri Vijana

Zao la Kahawa kuwapatia utajiri Vijana

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Zao la kahawa limekuwepo nchini Tanzania kwa miaka mingi ni zao ambalo kwa sasa lonachagozwa na uwepo wa vijana. Ni zao ambalo likiwa linapata changamoto kwamba ukiliangalia wamiliki wa mashamba na wenye kahawa walikuwa ni watu wazima na wazee

"Na miaka inavyokwenda tunaona ni Bora kuwahusisha vijana na Serikali imefanya jambo kubwa sana ya kwamba vijana na wenyewe wanatambulishwa kwa kupewa mashamba block farming katika maeneo mbalimbali

"Mfano Kagera tumeanza vijana wanapewa hekari moja Moja ili waweze kutunza kahawa na kuweza kuuza na kupata utajiri kupitia kahawa. Ni maeneo ambayo ni nadra sana kukuta vijana wanamiliki mashamba, Na wamepata mashamba kupitia mradi huu wa BBT"- Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Primus Kimaryo

Amezungumza hayo katika kipindi cha Clouds 360 kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya mali shambani, Dodoma




Chanzo: Clouds Tv​
 
Back
Top Bottom