Zao gani linastahili kulimwa kipindi hiki?

Zao gani linastahili kulimwa kipindi hiki?

MwanawaMUNGU41

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
1,052
Reaction score
749
Wakuu habari za leo,bila shaka wazima na mnaendelea namihangaiko yenu ya kila leo. Naomba msaada wa kujua ni zao gani nilime kipindi hiki huko ili na mimi nijitose mzima mzima kwa mara ya kwanza,nataka kulima maeneo ya RUVU au kama kuna mtu anajua ni eneo gani zuri tofauti na huko,tafadhali naomba msaada wenu! Asanteni muwe nasiku njema.
 
Nionavyo mimi kama unaenda kulima Ruvu ambapo wanafanya kilimo cha umwagiliaji usilime kipindi hiki cha masika, maana magonjwa na wadudu yanakuwa mengi, mafuriko yanaweza kuharibu mazao, na hata ukivuna sokoni yanakuwa mengi na hivyo yatadoda, subiri kipindi cha kiangazi ulime kwa umwagiliaji utalima kwa urahisi zaidi
au mkuu kilimomaarifa.tajiri aje hapa kwa maelezo zaidi
 
Nucky Thompson
Nimefika kiongozi, ni kweli kilimo cha mazao ya mboga mboga na matunda , wakati wa masika huwa na changamoto nyingi sana. Miundombinu (barabara), mafuriko, magonjwa hasa blights/Kinyaushi, na baadhi ya wadudu hushamili sana wakati huo. Lakini kama unaweza kupambana na hayo yote basi ukivuna na kuuza ndani ya masika utapata pesa nzuri sana, maana wakati madaraja yanabomoka, barabara hazipitiki, mito inatanua njia zake n.k walaji hawajali hayo wanahitaji, mboga za majani na matunda mezani katika milo yao ya kila siku, hivyo kwa kuwa Demand ni kubwa/Costant lakini supply ni ndogo, automatic bei itakwenda juu mkuu

Kilimo cha kiangazi ni kizuri, lakini wengi hulima pia wakati huo, na gharama ya kuhudumia shamba huwa kubwa zaidi hasa kwa sababu ya mafuta/Kilimo cha umwagiliji kama unatumia pump n.k

Ni jukumu la mkulima mwenyewe kujipima na kufanya analysis nzuri , hasa aina ya zao analotaka kulima na gharama zake zikoje, ndani yake uncertaninties na risks ziwe calculated. Mwisho kabisa kabla ya kuzalisha sharti ujue soko lako/wateja wako ni wakina nani, na utawafikiaje.

asante
 
Back
Top Bottom