Zanzibar yakabidhiwa takwimu za uchimbaji mafuta, gesi

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,826
21,436
1660159562386.png


Unguja, Serikali ya Zanzibar imekabidhiwa rasmi takwimu (data) za utafutaji wa mafuta na gesi kutoka Serikali ya Tanzania. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo Jumatano Agosti 10, 2022 Ikulu ya Zanzibar kwa kutiliana saini kati ya Waziri wa Nishati wa Tanzania, January Makamba na Waziri wa uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Zanzibar, Suleiman Masoud Makame.

Awali takwimu hizo zilikuwa zikihifadhiwa na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu (Pura), ambapo sasa imekabidhi takwimu hizo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA). Hatua hiyo inatoa fursa kwa sasa Zanzazibar kuanza kujisimamia katika suala hilo na kuliondoa kwenye Muungano.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema kuna kila dalili inayoonyesha Zanzibar ina rasilimali ya kutosha ya mafuta na gesi. “Mungu atatuwezesha Zanzibar sasa ianze kuchimba mafuta na gesi, kila dalili zipo za kuwa na rasirimali ya kutosha kilichobaki ni kukamilisha kutoka hapa kwenda hatua nyingine. Hizi data nyingi zipo katika hatua ya 2D tunatakiwa twende hatua ya pili ya 3D na ya tatu ni kuanza kuchimba.”

Dk Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji katika sekta hiyo ili kuendelee kufanya utafiti na kuchimba rasilimali hiyo itakayoleta mabadiliko makubwa katika uchumi wa Zanzibar. Amesema iwapo Zanzibar ikifanikiwa kupata mafuta na gesi asilia, uchumi utabadilika kwa kiasi kikubwa na tayari kitalu cha Zanzibar-Pemba wameshapata takwimu za awali zinazoonyesha kuwa na kiasi cha trilioni 3.8 za gesi asilia.

Naye, Waziri Makamba amesema takwimu hizo ni muhimu katika mnyororo wa utafiti na utafutaji mafuta na gesi. Amesema vitalu vilivyokabidhiwa ni vitano; kitalu namba tisa, 10, 11, 12 na kitalu cha Zanzibar-Pemba. Amesema tangu miaka ya 1950 zilipoanza shughuli za utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi, data zimekusanywa katika maeneo ya baharini na nchi kavu zinazohusisha mitetemo ya 2D kiasi cha kilometa za mraba 139,000 na data za mitetemo za 3D kilometa za mraba 32,094 na data za miamba kutoka kwenye visima 96 vilivyochimbwa na kuchorongwa.

Kwa upande wake, Makame amesema licha ya utafutaji wa mafuta na gesi kuanza kipindi kirefu, kwa Zanzibar ilikuwa ni nadharia ila kwa kukabidhiwa takwimu hizo sasa wanaanza kazi hiyo kwa vitendo. “Wawekezaji walikuwa wakija na kuondoka kwasababu ya kukosa data hizi, sasa zitakuwa kichocheo cha utafutaji wa kukuza uchumi wa Zanzibara,” amesema.

Chanzo: Mwananchi​
 
Awali takwimu hizo zilikuwa zikihifadhiwa na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu (Pura), ambapo sasa imekabidhi takwimu hizo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA).

Hatua hiyo inatoa fursa kwa sasa Zanzazibar kuanza kujisimamia katika suala hilo na kuliondoa kwenye Muungano.
 
Mafuta na gesi yaliindolewa Lini kwenye mambo ya Muungano?
Nami nikuulize wewe, samaki waliondolewa lini katika mambo ya Muungano?
Samaki akivuliwa Zanzibar ni wa Zanzibar, na yule atakayevuliwa Tanganyika ni wa Tanzania!

Inabidi tufike mahali tuseme, Muungano umekuwa ni wa upande mmoja kufaidika na mali za mwenzie, huku zake zikiwa ni kwa faida yake mwenyewe.
 
Mafuta na gesi yaliindolewa Lini kwenye mambo ya Muungano?
Ziliondolewa wakati wa uongozi wa JK na Karume, waliondoa kinyemela kwani mafuta na gesi yalikuwa miongoni mwa mambo 8 ya muungano na taratibu za kuondoka ni kuridhiwa na theluthi mbili ya binge la jamhuri na Baraza la wawakilishi kitu ambacho hakikufanyika.
 
Yaani nyerere alijifanya mjuaji lakini kwenye huu muungano alotuingiza sisi wabara tumeonekana mbumbumbu kabisa yaani watu wasio na ujasiri wakujitetea kwa chochote wanaweza kuonewa na wanajua kabisa wanaonewa lakini watakaa kimya.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
EeenHeeeee!

yanakuwa ya chatu kummeza tembo!

Usimlaumu Nyerere bure; Muungano haukulenga kuwa hivi. Haya yanayotokea leo ni ya CCM mbovu inayodhani kwa yenyewe kuendelea kuwa kwenye madaraka ni lazima kutoa rushwa kwa wapemba.
 
Ziliondolewa wakati wa uongozi wa JK na Karume, waliondoa kinyemela kwani mafuta na gesi yalikuwa miongoni mwa mambo 8 ya muungano na taratibu za kuondoka ni kuridhiwa na theluthi mbili ya binge la jamhuri na Baraza la wawakilishi kitu ambacho hakikufanyika.
Sema kwa sauti usikike vizuri mkuu 'rodrick alexander', na sasa Samia ndio anatekeleza kwa kasi yote.

Na bado!
 
Huu muungano ni michosho kweli. Kitu chochote cha Tanzania, Zanzibar anahusika kwasababu Tanzania ni muunganiko wa Zanzibar na Tanganyika. Lakini kitu cha Zanzibar sio lazima kiwe cha Tanzania na Tanganyika haihusiki kabisa. Yaani kifupi Zanzibar wanahaki ya vitu vyote vya Tanganyika lakini Tanganyika(Tanzania bara)haina haki na vitu vya Zanzibar, yaani sielewi maana ya huu muungano.
 
Huu muungano ni michosho kweli. Kitu chochote cha Tanzania, Zanzibar anahusika kwasababu Tanzania ni muunganiko wa Zanzibar na Tanganyika. Lakini kitu cha Zanzibar sio lazima kiwe cha Tanzania na Tanganyika haihusiki kabisa. Yaani kifupi Zanzibar wanahaki ya vitu vyote vya Tanganyika lakini Tanganyika(Tanzania bara)haina haki na vitu vya Zanzibar, yaani sielewi maana ya huu muungano
Kwahiyo ndio mana wazanbr wakija na biashara Tanzania bara wanalipa kodi ila Tanzania bara wakipeleka biashara zanbr free
Ndio mana zanzibar mtu akija na gari lake kutembea nalo Tanzania bara wanalipa kodi kubwa ila mkenya,Zambia na nch jirani wanaingia kwa kodi ndogo Kama kwao
 
Wazanzibari kuweki makini na gesi yenu sisi yetu Kikwete aliitumia kama dhamana kwa mchina kwa miaka 99 alisikika mjinga mmoja akisema!
 
Kwahiyo ndio mana wazanbr wakija na biashara Tanzania bara wanalipa kodi ila Tanzania bara wakipeleka biashara zanbr free
Ndio mana zanzibar mtu akija na gari lake kutembea nalo Tanzania bara wanalipa kodi kubwa ila mkenya,Zambia na nch jirani wanaingia kwa kodi ndogo Kama kwao
Umesema uwongo@
 
Mafuta na gesi yaliindolewa Lini kwenye mambo ya Muungano?
Hili swali wanatakiwa watujibu watu wa CCM maana mambo ya kitaifa wanayageuza ya kichama. Sijui wanahisi Watanganyika ni wapumbavu.

CCM ndio wanaohujumu na kuuvunja huu muungano sababu ya kufeli kuusimamia.
 
Wazanzibari kuweki makini na gesi yenu sisi yetu Kikwete aliitumia kama dhamana kwa mchina kwa miaka 99 alisikika mjinga mmoja akisema!
Si ujinga bali ni kweli ilailikuwa lazima iwe hivyo hata Raisi ungekuwa wewe. Hatuna pesa za kufanya utafiti(exploration) na hatuna pesa za uchimbaji/uzalishaji(extraction). Wawekezaji wametumia matrillion ya pesa kufanya hiyo kazi na lazima warudishe pesa yao na faida hata hiyo miaka 99 ni michache
 
Back
Top Bottom