Mwiba,
Tatizo kubwa ambalo linautikisa Muungano ni hili la ufisadi mkubwa sana ambao haujawahi kutokea unaofanywa ndani ya serikali ya Muungano ukiwahusisha wabara watupu na hakuna sheria zinazochukuliwa ?!!? Zanzibar kama nchi inayofanya muungano huu kidamu kabisa inaona hali hii haiwezi kuendelea ikiwa nayo ni sehemu ya Muungano maana hasara inayopatikana pia inaathiri Zanzibar kwa upande fulani kimaendeleo.Wizi wa matrilioni ya shilingi unafanyika waziwazi ,huku hazina za Taifa zikipotea ,sasa kama Zanzibar wana mafuta na yananyemelewa na Muungano ,hamuoni kama faida haitapatikana na hawa wezi waliomo ndani ya serikali ya Muungano ambao sheria haziwagusi wataweza kuifikia kirahisi hazina ya Zanzibar na kuitafuna bila ya woga kama wanavyoitafuna hazina ya Tanganyika ? Hivi kutakuwa na Muungano au kutakuwa na wezi waliojificha ndani ya Muungano huu ?
Mkuu wangu acha kutuzuga. Viongozi wa serikali ya Muungano ndio MAFISADI wenyewe halijalishi nafasi ya mtu katoka sehemu gani ya Muungano.. hawa wote kwa pamoja wanachelewesha maendeleo ya sehemu zote mbili. Hivyo kama kweli kungekuwa na mwamko huo Wazanzibar tungewasikia Bungeni wakilaani Ufisadi na hata wangetaka mabadiliko ya Katiba ya Muungano kuhusiana na miiko na maadili ambayo Yalivunjwa na Mh. Mwinyi rais wa jamhuri na mwakilishi wa
Zanzibar.
Ukisema ati Zanzibar wanaona Ufisadi ulivyo bara, hali uongozi wake unawashirikisha viongozi toka Zanzibar ktk kila nafasi ndani ya serikali ya Muungano ni kutafuta uongo unaokubalika ili mradi mnakipaka tu... Nenda wizarani, mashirika ya Umma, taasisi za serikali wamejaa Wazanzibar wengi tu na Mafisadi pia tena ktk miradi ya Bara na sijawahi sikia Wabara tukizungumzia watu hao kuwa Mafisadi kutokana na Uzanzibar wao.
Na unapofikiria kwamba kuwepo kwa Mafuta huko visiwani ndio kunapelekea Zanzibar kufikiria maslahi yake ni jambo ambalo linanipa wasiwasi na mtazamo wako ktk mahusiano ya Muungano wetu.. Yaani unanikumbusha kisa cha mshiakaji wangu hapa aliyekwenda kuoa mke Bongo miaka kibao tukidhania wakipendana ajabu.. Na MaashaLlah Mnyazi Mungu kawajaalia watoto baada ya kuishi ktk ndoa miaka 10 pamoja, wakati huo huo wa ndoa mke alichukua masomo ya U nurse na muda wote huyu mshikaji akiingia gharama zote.
Siku mkewe alipomaliza masomo na kuanza kazi ndipo siku tuloanza kusikia mke akidai Talaka yake kwa madai kwamba hakuwa akimpenda jamaa toka zamani. Ndipo tuliposikia hadithi zote za jinsi alivyokuja poswa na kulazimika kuolewa kutokana na mazingira alokuwa nayo wakati ule lakini hakuwa na mapenzi na huyu jamaa. yaani mke aliolewa kwa sababu ya kuvuta karatasi za kuishi Ulaya lakini hapakuwa na mapenzi..eeeh ngoma nzito hiyo baabu!
Sasa kwetu sisi tunajiuliza hivi, kama huyu mke angeomba talaka yake na kudai hana mapenzi naye tena na amechoka kuishi ktk ndoa hiyo. Bila shaka ingeeleweka vizuri na kwa uzito mkubwa zaidi kuliko kusiribia kinyesi kwa karatasi unayotawadhia..
Tatizo kubwa ni pale huyu mwanamke anapoweka madai ya kumshusha hadhi jamaa, abuse za maneno sijui ya kwamba hakuwa na mapenzi naye kwa miaka yote 10 isipokuwa ilibidi tu.. Na zaidi ya hapo tulisikia hadi mambo ya ndani chumbani yaani ilikuwa mwanamke anasiriba sio kupaka tena..
Mkuu wangu siku zote tujaribu sana kuepusha maamuzi yatokanayo na vitu viwili:-
1.Ushawishi wa fedha au mali na 2. Ushawishi utokanao na Ulimbukeni.
Kauli zozote zinazoweza tafsirika kutokana na hayo hapo juu ndizo huondoa ladha na uzito wa hoja ya mtu kama huyu binti yetu kufikia sisi kumwona yeye ndiye asokuwa na akili. Hakuwa na sababu ya kuzungmza yoote haya ya toka ampigie mahesabu jamaa Bongo hadi maswala ya ndani ya unyumba ili kuleta uhalali wa kuomba Talaka tu. Unapotaka talaka hulazimishwi kutaja sababu kubwa au kuonyuesha ujanja wa akili kumzunguka alolala ili kuhalalisha madai yako,kwani - Haihusu!
Ukisema umechoka kuishi maisha ya ndoa inatosha kabisa kupata sheria ya kuachika -No means NO!.
Sasa kichekesho ni kwamba mshikaji pia kwa miaka mingi alikuwa akitafuta njia ya kumtoka mkewe isipokuwa alishindwa kutokana na wajibu aloji commit kuingia ktk ndoa kulingana na imani yake ya dini kisha tayari walikuwa wamezaa watoto. Kifupi kila mmoja wao alikuwa akitafuta njia ya kumtoka mwenzake kumbe hawa jamaa kwa miaka yote waliyoishi ndani ya ndoa hawakuwa na mapenzi ya haki. Kwa upungufu kila mmoja wao aliingiza tu asilimi 50 ya nguvu ya kimapenzi hivyo kila mmoja wao alimuona mwenza kuwa mchovu wa Mapenzi.
Hatuwahitaji Zanzibar hata kidogo zaidi ya kiapo, but for sure najua fika Zanzibar inawahitaji Bara..ndio inachofanya tunahitajiana.. Hiyo Greencard waliyokuwa nayo Zanzibar haitoshi kuweka guarantee usalama wa visiwa hivyo. I 'm 100 sure baada ya kujitenga tu basi Pemba watatumia sababu hizi hizi za leo Zanzibar nao kujitenga. wataanza na kuomba madaraka zaidi, ku share leadership na mwsiho ya yote hawautaki Muungano wa visiwa vya Zanzibar. Uhasama wa Kiutawala Zanzibar upo baina ya Wazanzibar wenyewe toka enzi za kutawaliwa. Hawa jamaa wamejificha ktk makundi ya vyama hivi lakini Uadui wao upo palepale na Bara inatumiwa tu kuamsha cheche za upinzani wao.
Hakuna Mzamzibar kiongozi asiyependa Muungano (ndio baba zenu hawa) na kama mmeozeshwa pasipo mapenzi wekeni maombi ya talaka mtapewa na sio kutukandya Bara mkifikiria ndio mnajenga hoja zenu.. Tumebebana vya kutosha mkuu wangu na nadhani ni vizuri sana mkiweka wazi ombi la kuvunja Muungano..sii lazima kututukana kana vile sisi ni Washenzi, Mashetani watu wasiokuwa na ustaarabu hali mmekuwa ktk ushirika huu kwa zaidi ya miaka 40 inawafanya nyie kuonekana wapumbavu au vichaa.. Na kibaya zaidi ni kwamba mnazugumzia sana hisia zenu nyie katika Muungano huu pasipo kuelewa kwamba hata sisi Bara tulishachoka isipokuwa tumebakia ktk Muungano huu kutokana na kiapo na watoto tulokwisha zaa ndani ya Muungano huu.