Ngekewa,
Mkuu wangu wewe unazungumza kwa lugha ya Kibaguzi pasipo kuelewa kwamba hapa tunazungumza kama ndugu jamaa na hakika mimi nawapenda sana ndugu zangu/zetu WaZanzibar isipokuwa hukereka mnaposhindwa kuelewa kwamba viongozi wote wa Zanzibar ni wanafiki na washenzi.
Zanzibar na mustakabali wake haunihusu ila nazungumzia mtazamo wangu kutokana na historia ya nchi hiyo hivyo hata siku moja Zanzibar haijawahi na haitawahi kuitoza chafya Bara isipokuwa huruma ya bara ndio inatuponza, tupo kama beach safe guards wenu tu.
Kweli, ni Nyerere ndiye alimwambia Karume kuhusu Muungano kutokana na kwamba waliyachukua Mapinduzi toka kwa kina Abrahman Babu na unajua fika kwamba Wakomunsit walikuwa tayari kumwondoa Karume. Karunew had no option hata kufikiri akili iliganda akijua hafiki popote na unyakuzi wake.
Nenda kazungumze na Nassor Moyo sii alikuwa mshikaji wa marehemu Kassim Hanga akueleze vizuri historia ya Zanzibar. Hawa wote walijiunga na Babu na walikuwa tayari kuiendesha nchi isipokuwa huo Muungano ndio ulowaponza na wakahamishiwa Bara kumpa pumzi Karume.
Kwa hiyo huu muafaka ni kanyanga tu. Ni marudio ya miafaka kibao iliyowahi kutokea zanzibar mwisho wa yote hutoana damu.. Ebu nambie kilichomkimbiza Shamte ASP na kuunda coaliation na ZNP ili kuwashinda ASP ilitokana na kitu gani kama sii unafiki? Hali Karume aliwahi kumfuata Shamte na ZPPP waunde umoja kumshinda DSultan (ZNP) lakini akamtolea nje, ili mradi tu yeye na Sultan wachukue nchi akihahidiwa na kupewa Uwaziri Mkuu. Nasema Uongo?..Na Si ndio anayofanya leo Seif Sharrif au naongopa pia!
Hivyo Shamte aliuza nchi kwa sababu tu yeye kupewa Uwaziri mkuu ktk serikali ya Kutawaliwa tena na Sultan, na haikuwa kwa maslahi ya Wanzibar kwani kama sio wao kujiengua ASP kulikuwa hakuna nafasi ya Sulatn (ZNP) kushinda uchaguzi wowote Zanzibar. Na ndio maana unaona sifa sana kuzungumzia nywele ndefu kama ni tuzo fulani vile.
Tuache huko, Baada ya Mapinduzi Karume kamfanya nini Abrahman Babu, na hata hao kina Hanga waliokuwa chama baada tu ya Ushindi. Kawageuka na kuwa maadui zake tena kwa ushenzi mkubwa alipokufa Karume unakumbuka jinsi mlivyowaua watu wasiokuwa na hatia kabisa. Zanzibar na Pemba kulikalika au umesahau mkuu wangu! Jiulize ni kwa nini Zanzibar hawamtaki Babu hadi siku anaingizwa kaburini na kina Salim ndio wanazeeka pasipo kukubalika tena Zanzibar. Yaani viongozi wamejaa chuki na roho za kikorosho sijapata kuona.
Kwa hiyo, Salama ya Zanzibar ipo mikononi mwa Bara na hakika kila mnapotaka kufanyiza ndipo hudai sana mamlaka fulani lakini ndani ya roho za vioongozi wenu wana nia mbaya sana. Nina hakika JK akikubaliana na matakwa kama haya ipo siku mtakuja jutia na hakika kusingizia kwamba ni JK aliyesababisha hali mnasahau kwamba kwa kila ovu na matukio ya mauaji Zanzibar hupangwa na hao hao viongozi wenu. Nitakujulisha tena kwamba ni Seif Hamad Huyu huyu aliyewatonya bara kuhusu dhamira ya Aboud Jumbe kuuvunja Muungano. Sasa kama sii unafiki hivi ni vitu gani?
Mkuu wangu nawajua sana kwa ukaribu.. Unafiki ndio mila ya Wazanzibar, atakuchekea usoni huku akikuimbia Taarabu inayokuvua nguo wewe, mkeo na familia yako yote na hata siku moja hapatakuwepo na mahusiano mazuri kati ya Waunguja na WaPemba kwani kila mmoja wenu anajua zaidi wakati hajui kwamba hamjui mwenzake hajui asichokijua!