Zanzibar wanatupa kampani ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ?

Mtanganyika1

Member
Sep 13, 2011
56
5
Habari zenu wana JF: Ndugu zangu mimi bado natatizwa na suala zima la muundo wa serikali yetu, mwaka huu tunasheherekea miaka 50 wa Tanganyika na siyo tanzania tena ambayo nayo huwa tuna sema miaka kazaa ya Muungano wa tanzania,vivyo hivyo kwa zanzibar huwatunasheherekea miaka kazaa ya mapinduzi ya Zanzibar.

Tukija katika suala zima la tukio la mwaka huu, tungesema wazi tu kwamba Miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika na siyo Tanzania, hili limekaa kama watu walio funga ndoa kila mtu atatambulika kwa mwaka wake wa kuzaliwa, tarehe na mwezi binafisi ,ikija kwenye birth day kila mtu anatmbulika kwa namna yake, suala la ndoa nalo miaka yake inaazimishwa kwa kuitambua tarehe mwezi na mwaka waliofungia ndoa, hata kama mmoja atakuwa amebadilisha jina, siku ya birth day ya mwenzake anaitambua kama ya mwenzake na siyo yake.

Kumbe basi , ni bora tuka sema wazi ni miaka hamsini ya Tanganyika na siyo Tanzania ambayo ilimbandilisha jina mmoja wawanandoa hao wawili.na Tuirudishie Tanganyika heshima yake ndani ya katiba mpya ijayo.

nawakirisha.
 
Back
Top Bottom