Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 988
Kuifananisha Zanzibar na mkoa wowote wa Tanzania Bara imekuwa ni dhana ikikataliwa hasa na wazanzibar. Tunakumbuka Julai 2008, Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliingia matatani aliposema Zanzibar siyo nchi.
Leo tena Bungeni kumeibuka hoja hiyo. Mheshimiwa Zitto Kabwe aliuliza swali zuri tu, swali alilomuuliza Waziri Shamsa Vuai Nahodha. Swali lenyewe ni kwamba siku haijawahi kutokea tangu tujitawale Mkuu wa Majeshi (Chief of Defence forces/TPDF) akatoka Zanzibar. Wakuu wote wamekuwa wakitoka Bara.
Swali likaendelea kuuliza je, Waziri anaweza kutamka kuwa sasa inawezekana akapendekezwa mkuu kutoka Zanzibar?
Kila mmoja hata mimi nikajawa na shauku kujua jibu la swali hili. Binafsi nilijisiki vizuri mbele ya TV yangu kwanza nikijua kwamba swali linajibiwa na mzanzibar na aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar.
Kwa kweli alijibu vizuri kwa kusema kuna wanzanzibar kadhaa kwenye ngazi za juu ya jeshi letu (TPDF) katika ngazi ya Brigedier-General na wengine. Hivyo upo uwezekano japo hawezi kutamka rasmi kama itakuwa hivyo. Hadi hapo kwa hakika swali likawa limeisha.
Lakini Nahodha akaongezea kauli nyingine ambayo sidhani kama alipima matokeo yake. Akasema hata hivyo na yeye kama Nahodha anajua historia ya CHADEMA ambako hajawahi kusikia Mwenyekiti wa CHADEMA akitokea mkoa wa KIGOMA. Bunge zima likabaki linacheka. Kwani muuliza swali aliyekuwa anajibiwa ni Zitto kabwe na anatokea Kigoma.
Athari za jibu hili ni nini? Zitto aliipa Zanzibar uzito unaostahili katika uwiano wa mambo ya muungano. Kwa namna moja Zitto anaonyesha kwamba kuna usawa wa eneo wa iliyokuwa Tanganyika na usawa kwa eneo la Zanzibar. Hivi viwili ndivyo vinavyobidi kulinganishwa.
Sasa, Nahodha anapojibu swali kwa kulinganisha Zanzibar na Kigoma basi hii ni hoja yake na wala haikuwa mlinganisho wa Zitto Kabwe.
Maadam mlinganisho huu umetajwa na mzanzibar basi wazanzibar waache kulalamika wanapolinganishwa Zanzibar yote kama mkoa wowote wa bara. Maana ni ukweli kwamba Zanzibar inaingia zaidi ya mara tatu kwenye mkoa wa Mwanza kieneo na population.
Binafsi ninamshukuru sana mzanzibar huyu Shamsa Vuai Nahodha kwa ulinganisho huu, maana ingekuwa leo amesema mbara yaani m-tanganyika sijui upepo ungekuwaje mle bungeni na siajabu dakika hii ingekuwa ni mfululizo wa kuomba miongozo kwa spika kwa kitendo cha kuilinganisha Zanzibar na mkoa.
Shukurani sana Shamsa Vuai Nahodha.