Zanzibar NI Nchi-Samia Suluhu

Zanzibar NI Nchi-Samia Suluhu

Mheshimiwa Waziri wa Muungani amehalalisha uhalali za Zanzibar kuwa HAKUNA Atahri kwa Zanzibar kuwa na Bendera, Wimbo wa Taifa etc kwa kuwa Zanzibar ni Nchi Kamili

Source: Taarifa ya habari ITV saa 2.00 USIKU

Huyu mama ni snake in the grass hutumiliwa na JMT kuizamisha Zanzibar., kwanza hana sifa za kuwa Waziri zaidi ya mama wa nyumbani tu, mara ngapi nimemuona bungeni anaulizwa maswali ya muungano yeye ndio mtu wa mwisho kama waziri katika Wizara ile ya Muungano anakuwa hana majibu, anatafuna maneno yaani mpaka anaaibika.,
 
Kwa mtazamo wangu, labda vita ya wenyewe kwa wenyewe (wapemba na waunguja) lakini sidhani kama Sultani atatawala pale! Labda tu wafunge mkataba wa kuchimbwa mafuta! Si unajua wazanzibar udini unawapelekesha sana!

sultan atarudi zanzibar kwa kupitia wapemba, bado wanamawasiliano makubwa sana na watu wa pemba na ndo maana ukiangalia kwa makini wanaotaka zanzibar ni wapemba.
 
Akili za Madrasa hizi.Nenda Afrika ya Kati ukawasaidie Mujahideen,Wenzako wanahamishwa na Malori kutoka Mjini Bangui baada ya Jihad waliyoianzisha kuwageukia.

Issue imegeuka mbaya mpaka inadaiwa kuna uwezekano wa kuwepo genocide!
 
Zanzibar kama ni nchi mbona haina kiti maalum AU. nyie wazenji acheni kutudanganya kisa mmegundua mafuta basi mnajiona wajajanja kweli tukiwaacha mmarekani anakuja kuyakomba yote hatowaachia hata tone LA mafuta

Mkuu ukiitazama zanzibar katika jicho la Kisheria De Facto Zanzibar ni nchi lakini De jure ni sehemu ya Tanzania yaani haina tofauti kama kisiwa cha Ukara au ukerewe.Kwa sababu hiyo unaweza ukakuta ikawa na mahusiano na nchi za nje au dunia ya Kimataifa kwa mipaka fulanifulani katika baadhi ya Masuala.Kule UN kiti chao hakipo kwasababu DE JURE wao ni sehemu ya Tanzania.

Kizungumkuti hapa ni kwamba Rais Kiwete akiwa Zanzibar nikama Raia wa kawaida tu hana Cheo chochote .Amiri jeshi mkuu kule ni DK Ali Mohamed Shein na ndomaake huwa anakagua gwaride na kupigiwa mizinga pamoja na saluti na Rais Kikwete anakuwa mtazamaji au kama waalikwa wengine (VIP).

Hawa wana Katiba yao, na Bunge lao kwa hiyo kimsingi kwa kingereza tungesema labda ni Free state but Not sovereign.Jambo lingine ni kwamba ukiwa Tanzania bara (hapa soma Tanganyika) kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na ukataka kwenda Zanzibar jua unakwenda nchi za nje.
 
halafu soma Ibara ya Kwanza ya Katiba ya JMT

Je umesoma IBARA YA KWANZA YA KATIBA YA ZNZ inayosema wazi KUWA ZNZ NI NCHI.

Pitia katiba ya Znz utaliona utalitambua hilo.

Pole sana , japo inakukera lakin ukweli ndio huo

Akili za Madrasa hizi.Nenda Afrika ya Kati ukawasaidie Mdaktaujahideen,Wenzako wanahamishwa na Malori kutoka Mjini Bangui baada ya Jihad waliyoianzisha kuwageukia.

Swadakta Farudume.

Hayo ndio yanayotarajia kutokea TAnganyika nje ya muungano. Kwani waislam huko waislam ni second citizen wana madai kibao na nchi inaendeshwa kwa mfumo KRISTO.

je hujui hilo?
 
Ndugu yangu,Tanganyika tulibadili jina na Kujiita Tanzania baada ya kujiongezea himaya ya Zanzibar,Zanzibar ni Koloni letu ndio maana hakuna hata Siku Moja Mkutano au Kikao kinachohusu Tanzania kikafanyika Zanzibar na wala Zanzibar haiwezi kugharimia kwa Sababu ipo Chini ya Himaya ya Tanganyika(hutamkwa Tanzania).

Si uweke wazi kuwa mlibadili jina BAADA YA KUOLEWA kama wanavyofanya ndugu zetu wa upande wa pili.
 
Je umesoma IBARA YA KWANZA YA KATIBA YA ZNZ inayosema wazi KUWA ZNZ NI NCHI.

Pitia katiba ya Znz utaliona utalitambua hilo.

Pole sana , japo inakukera lakin ukweli ndio huo

Acha kujidanganya na Hadithi za Vijiweni.Zanzibar iwe Nchi halafu kila Siku mnadai muachwe mpumue?.Kura mlizopiga Kumchagua Kikwete zilikuwa za nini?Kwa nini Mgombea wa Urais Zanzibar kupitia CCM lazima apitishwe Dodoma?
Zanzibar ni Sehemu ya Tanzania na Tanzania ni Tanganyika,Kimahesabu Zanzibar ni Sehemu ya Tanganyika.Baada ya Tanganyika kujiongezea Himaya yake(Zanzibar)ilibadili jina na kujiita Tanzania.Tanganyika ikaiachia Zanzibar Mamlaka yake ya Ndani mfano kuwa na Wimbo wa Taifa,Bendera,Rais,Umiliki wa Ardhi nk.Maamuzi yote ya Kisera hutoka Tanganyika(hutamkwa Tanzania).Huu ndio Ukweli wa Mambo na Wajuvi wote wanaelewa hili.
 
Kwa mtazamo wangu, labda vita ya wenyewe kwa wenyewe (wapemba na waunguja) lakini sidhani kama Sultani atatawala pale! Labda tu wafunge mkataba wa kuchimbwa mafuta! Si unajua wazanzibar udini unawapelekesha sana!

Mmh una uhakika na unalonena?

Udini upo Tanganyika, Znz 99.9% ni waislam udini utatokea wapi tena?

Je umeshawahi kusikia znz wanashindaniana kuchinja yaani ni imani gani ina haki zaidi ya kuchinja? fanya utafiti kidigo kabla kunena

Acha kujidanganya na Hadithi za Vijiweni.Zanzibar iwe Nchi halafu kila Siku mnadai muachwe mpumue?.Kura mlizopiga Kumchagua Kikwete zilikuwa za nini?Kwa nini Mgombea wa Urais Zanzibar kupitia CCM lazima apitishwe Dodoma?
Zanzibar ni Sehemu ya Tanzania na Tanzania ni Tanganyika,Kimahesabu Zanzibar ni Sehemu ya Tanganyika.Baada ya Tanganyika kujiongezea Himaya yake(Zanzibar)ilibadili jina na kujiita Tanzania.Tanganyika ikaiachia Zanzibar Mamlaka yake ya Ndani mfano kuwa na Wimbo wa Taifa,Bendera,Rais,Umiliki wa Ardhi nk.Maamuzi yote ya Kisera hutoka Tanganyika(hutamkwa Tanzania).Huu ndio Ukweli wa Mambo na Wajuvi wote wanaelewa hili.

Pole sana ahali yangu,

Kwa kukusaidia kidogo ni kuwa mamlaka ya nchi kisheria yapo katika mihimili mikuu mitatu YAANI SERIKALI, BUNGE NA MAHAKAMA.

Jiulize ZNZ IMEKOSA KIPI HAPO?

Pole sana

Si uweke wazi kuwa mlibadili jina BAADA YA KUOLEWA kama wanavyofanya ndugu zetu wa upande wa pili.

Siamini kama Mfano wa kuolewa ni wa Kiungwana sana lakini kama ni lazima utumiwe nafikiri Zanzibar ndio imeolewa.Ninavyojua Mume ndie hugharimia Gharama za Familia.Angalia zanzibar wanapewa umeme na Tanganyika,Gharama za ulinzi zinalipiwa na Tanganyika na hata Kesi ya Uhaini iliyokuwa inawakabili akina Maalim Seif iliamuliwa Uhaini hauwezi kufanyika Zanzibar.Zanzibar hupewa 4% ya Pato kutoka Serikali ya Tanzania(Tanganyika)
Kwa Ufupi Tanganyika ndio inayoihudumia Zanzibar na hili ndili Jukumu la Mume kwa Mkewe.
 
Mheshimiwa Waziri wa Muungani amehalalisha uhalali za Zanzibar kuwa HAKUNA Atahri kwa Zanzibar kuwa na Bendera, Wimbo wa Taifa etc kwa kuwa Zanzibar ni Nchi Kamili

Source: Taarifa ya habari ITV saa 2.00 USIKU

Nchi zote au karibu zina kiti UN na AU kwa Africa. Je Zanzibar wanavyo?
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Hilo halihitaji ubishi.
Kuwa na bendera au wimbo si hoja hata vilabu vya mpira vina nyimbo na bendera zake.
Serikali tatu ndio jibu
 
Kiukweli inatakiwa tuwe na serekali moja na Zanzibar itambuliwe kama mikoa mingine tu kama Mtwara, Kigoma, Dar, Dodoma au mkoa mwingine wowote.

Uzalendo katikati ya Udini ni sawa na uwandawazimu usio na tiba.

Pole sana
 
Ni serikali 3 itawaokoa wanzanzibar tatizo ni waunguja kuwahofia wapemba
 
Znz ni nchi,Tanganyika ilikufa

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Baada ya Sief Khatibu kushindwa?

Back
Top Bottom