Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Serikali visiwani Zanzibar imeyafungukia maduka matatu makubwa wilayani Wete ambayo yalibainika kufanya ubaguzi kwa kutowahudumia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mkuu wa Wilaya ya Wete, Rashid Hadid Rashid amewaambiwa waandishi wa habari kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kina, walibaini kuwa wafanyabiashara Said Juma Seif, Titi Juma Othman na Hamad Haji wanaomiliki maduka makubwa hukataa kuwahudumia wanaCCM.
“Tumelazimika kuyafungia maduka hayo matatu baadaya Serikali ya Walaya kujiridhisha kuwa yanawabagua wanachama wa CCM,” Rashid anakaririwa.
Mh.Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa Cuf.
Maalim seif alinukuliwa akinena katika moja ya mikutano yake akisema ''Tukikazana serikali hii itaondoka madarakani.Ikiwa mnangoja Maalim Seif au Marekani kuiondoa haitawezekana kwani Sheria ya kimataifa hairuhusu Marekani kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar.
Kwa Upande wa CCM Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Vuai Ally Vuali alisema kuwa hivi sasa hawana muda wa kujibizana na CUF kwani uchaguzi umekwisha na kwamba watakutana tena majukwaani mwaka 2020.
Je ''Raisi wa mioyo ya Wazinzibar'' atafanikiwa? Kwanini Pemba wabague wenzao wa CCM?