Zanzibar kunyimwa 'Change ya RADA' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar kunyimwa 'Change ya RADA'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sr. Magdalena, Jun 30, 2012.

 1. Sr. Magdalena

  Sr. Magdalena JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Wakuu heshima mbele sana,

  Kumekuwa na sintofahamu nyingi sana mara baada ya Serikali kwa bahati mbaya au makusudi kugawa fedha ya change ya Rada Tanzania bara pekee na Tanzania visiwani kutokupata hata centi moja, Wabunge wengi wa Zanzibar wameonekana kutokupendezwa na swala hili, Je ni sahihi kwa mgawo wa Rada kugawanywa bara pekee na si visiwani..?
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Change ya Rada si suala la muungano.
   
 3. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni sahihi kwa kuwa rada haikuwa ya muungano.
   
 4. Sr. Magdalena

  Sr. Magdalena JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Kaka Ngongo na Mangaline heshima zenu sana.

  Naona umejibu kwa kifupi sana, unamaanisha nini unaposema Rada si suala la muungano, ninavyofahamu mimi ni kuwa ulinzi na usalama ni suala la muungano, correct me if im wrong.
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Sr. Magdalena

  Kumbu kumbu zangu kama hazijachoka zinaniambia rada ililetwa kwaajili kuimarisha usafiri wa anga [ndege za kiraia] ingawa ingeweza kutumiwa katika masuala ya ulinzi.Mawasiliano si miongoni mwa masuala ya muungano ndiyo maana unasikia Zanzibar wametoa kibali meli za mafuta za Iran kutumia bendera ya Tanzania.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 819
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Rada ilinunuliwa na fedha ya tanganyika kwa ajiri ya tanganyika hivyo zanzibar haiwahusu maana hiyo change sio msaada ni fedha iliyotoka tanganyika bila kuwahusisha zanzibar sasa iweje inaporudishwa wanataka nao wahusishwe?
   
 7. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hela ya rushwa ya rada haiwahusu hao jamaa wasituzengee hapo watakula kwa macho
   
 8. Sr. Magdalena

  Sr. Magdalena JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Nimekuelewa kaka, nilidhani ilikuwa ni kwa ajili ya ulinzi na usalama, lakini kama iko Mawasiliano si muungano.

  Hapa kwenye nyekundu naona umechomekea, wa amerikani na waingereza wamechukizwa sana na hii kitu, hope JK atawaelewesha na watamwelewa kuwa ile barua iliyokua addressed magogoni imekosewa inabidi wa TRY Zanziba kwa Mr. Shein.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  Sr.Magdalena,

  ..Ulinzi ni suala la muungano, lakini kwa kawaida ZNZ huwa haichangii chochote ktk masuala ya muungano.

  ..kabla ya kulalamika, wabunge wa ZNZ wangeeleza wakati rada inanunuliwa ZNZ walitoa kiasi gani toka hazina yao. inajulikana kwamba makusanyo yote ya TRA Zanzibar hubakia hukohuko.

  ..mbona hatujasikia ZNZ wakililia kushirikishwa ktk kulipa madeni ya nje, kila siku ni kelele za kudai misaada na mgao??

  ..LET ZANZIBAR GO!!!
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hela iliyorudishwa ilitakiwa kwenda kusaidia maswala ya elimu ya msingi ambayo pia sio mambo ya muungano!
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Umeniwahi kiongozi. Wabunge toka Zanzibar wanaweza kutuambia kwa mwaka wanachangia kiasi gani kwenye mambo ya Ulinzi na usalama?
   
 12. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  wazenji wanataka vya bure, kama mnataka vya bure, njooni tuwape chenji, pia tutawanunulia na vyakula na chochote mtakachotaka tutawafanyia shopping...lakini malipo yake muwe tayari kwa lolote.....si mnataka vya bure!
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mbona hela wanzopata kutoka Al-queda kwa kutumia bendera yetu kwenye meli zao hatuulizii?
   
 14. Sr. Magdalena

  Sr. Magdalena JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  JokaKuu, Hi!

  Hapa ndipo watu wengi huchanganyikiwa, kwani mfuko mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano na mgawanyo wake wa fedha kwa serikali hizi mbili umekaaje?..na kuna uhusiano gani kati ya wizara ya fedha Bara na Visiwani, na Je wabunge kutoka Zanzibar wana maeneo maalumu ya kuchangia kwenye bunge la bajeti au wanachangia kila wizara?..
   
 15. p

  philipoz Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  bora hio change wamekula wenyewe, tukivunja muungano si tuna waachia mideni yao tu
   
 16. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Zanzibar si nchi nje ya mipaka yetu. Hivyo wamarekani hawawezi kui-address barua yao kwa Shein (mkuu wa mkoa wa zanzibar), bali kwa rais wa Tanzania JK
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Rada ni ya Serikali ya Muungano na ilipoanza kusifiwa ,ilisemwa kuwa itaweza kuweka ulinzi kwa mipaka yote ya Tanzania ,sasa jiulize mipaka ya Tz ni ipi ? Ila Zanzibar muelewe kuwa haina haja ya vihela hivyo wala haviwababaishi ,tatizo ni kwa hao wabunge wawili watatu waliojikaza kuutetea Muungano juzi ,ila wataelewa tu ,na hiyo ni chachu ya kuwajulisha kuwa kwao ni Zanzibar ,nchi yao ni Zanzibar na sio Tanganyika. Chondechonde.
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hadi hela za rada zinadaiwa na Zanzibar? Duh!
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  Sr.Magdalena,

  ..unajua ule uoga wa kuimeza ZNZ ndiyo umetufikisha hapa.

  ..kwa kuogopa kuimeza ZNZ, serikali ya muungano ilifumbia macho mambo mengi mabaya ikiwemo mauaji yaliyokuwa yakifanywa na SMZ na baraza la mapinduzi.

  ..serikali ya muungano inapaswa kuisimamia na hata kuirudisha kwenye mstari SMZ.

  ..Wizara ya fedha ya Zanzibar ina majukumu na mamlaka ambayo yana mipaka. Kuna vyombo ambavyo viko chini ya mamlaka ya wizara ya fedha ZNZ, na pia kuna vyombo kama TRA vinafanya kazi ZNZ lakini viko chini ya mamlaka ya serikali ya muungano.

  ..Wabunge wa ZNZ wana maeneo maalum ambayo wanapaswa kuchangia. Kuna wizara ambazo ni za muungano na hizo ndizo wabunge wa ZNZ wanazopaswa kuzisimamia na kuchangia ktk mijadala inayozihusu.

  ..Mbunge wa ZNZ anapoingilia masuala ya Tanganyika anakuwa amekiuka hata ile imani ya wananchi waliomchagua. Sidhani kama wa-Zanzibar waliwapigia kura wabunge wao waje kuzisimamia wizara kama ya Afya ambayo si ya muungano. Hata kile kitendo cha Raisi kumteua mbunge wa Zanzibar kuwa Waziri ktk wizara ya Afya ni ukiukwaji mkubwa wa katiba na mkataba ya muungano.

  ..Kuhusu "mfuko wa muungano" mimi nadhani Tanganyika na Zanzibar zote zinakusanya mapato ktk upande wake. Sasa kwanini wasitumie kodi hizo kugharamia vyombo vya muungano vinavyotoa huduma ktk maeneo yao? Kwa mfano: kwanini ZNZ haiwalipi wajumbe wake ktk tume ya katiba? Zaidi kwanini hailipi posho za wabunge toka Znz walioko ktk bunge la muungano, au mishahara ya polisi, na wanajeshi, au madeni yake kwa Tanesco??
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wanabodi,
  Msipokuwa na majibu sahihi ni bora kabisa kukaa kimya kuliko kukisia ama kuleta Ubishi usiokuwa na maana. Chenji ya Rada ni UFISADI mkubwa ulofanyika na hata kama zimegawiwa bara sielewi zimegawiwa vipi kiasi kwamba haya madai yawe na ukweli wowote. Rada ilinunuliwa kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni swala la Kitaifa na tumelipwa kwa jina la mfuko wa Taifa hivyo hata matumizi yake ni ya serikali ya Muungano.

  Tatizo linalowakumba Wazanzibar wengi ni pale wanaposikia serikali ya Muungano basi lazima hiyo iwe inazungumzia bara tu, lakini wasichokifahamu ni kwamba Bunge la Taifa Dodoma linawashirikisha Wazanzibar, Utawala wa serikali yetu wamo Wazanzibar kwa manufaa ya pande zote mbili na hata ukitazama Kamati kuu ya chama tawala imejaa Wazanzibar - Huo mseto walounda Zanzibar majuzi unatumika Bara toka mwaka 1964 ktk serikali yetu ya muungano. Matumizi yote yanalipwa na kodi za wananchi wa pande mbili, Bara ikichangia zaidi kwa kila kitu. Sasa iweje fedha hizi zipelekwe ktk serikali ya (mseto) Mapinduzi wakati ni fedha za Muungano?..
   
Loading...