Zanzibar kunyimwa 'Change ya RADA'

Zanzibar kunyimwa 'Change ya RADA'

Membe hapo vipi wazenji wanahusika wakati wanna baraza lao la elimu. Au kwa kuwa tuliibiwa wote kabla ya Zanzibar kuitwa nchi kwa utawala huu. Maana wakati wa mkapa Zanzibar haikuwa nchi Bali integral part of Tanzania.
 
Wanabodi,
Msipokuwa na majibu sahihi ni bora kabisa kukaa kimya kuliko kukisia ama kuleta Ubishi usiokuwa na maana. Chenji ya Rada ni UFISADI mkubwa ulofanyika na hata kama zimegawiwa bara sielewi zimegawiwa vipi kiasi kwamba haya madai yawe na ukweli wowote. Rada ilinunuliwa kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni swala la Kitaifa na tumelipwa kwa jina la mfuko wa Taifa hivyo hata matumizi yake ni ya serikali ya Muungano.

Tatizo linalowakumba Wazanzibar wengi ni pale wanaposikia serikali ya Muungano basi lazima hiyo iwe inazungumzia bara tu, lakini wasichokifahamu ni kwamba Bunge la Taifa Dodoma linawashirikisha Wazanzibar, Utawala wa serikali yetu wamo Wazanzibar kwa manufaa ya pande zote mbili na hata ukitazama Kamati kuu ya chama tawala imejaa Wazanzibar - Huo mseto walounda Zanzibar majuzi unatumika Bara toka mwaka 1964 ktk serikali yetu ya muungano. Matumizi yote yanalipwa na kodi za wananchi wa pande mbili, Bara ikichangia zaidi kwa kila kitu. Sasa iweje fedha hizi zipelekwe ktk serikali ya (mseto) Mapinduzi wakati ni fedha za Muungano?..

Ndugu wana jamvi uzuri kusema ile hela ni ya Tanganyika kumbe Tanganyika ipo ki maslahi wakati wa hela hela hiyo ni ya Tanganyika kwa mengine ni muungano, kama ile hela ya Tanganyika ilitoka katika mfuko gani kwani Tanganyika inayo account yake nijuavyo mimi usafiri wa anga uko chini ya muungano, mimi nahisi wacha tuendelee kula hela za watanganyika mpaka itakapo kuwa tayari kuvua koti la muungano, kwanini ijivalishe koti kwenye maslahi ghafla hufufuka Tanganyia
 
[QUOTE=Mkandara;4151684

SikuTanganika itakapo vua koti la muungano basi huu ulalamishi wote utaondoka, lakini chenji ki mantik ni ya Tanganyika aliye preset ni Tanzania na pia lazima kuwe nyenzoambazo zuitatofautisha ki utendaji wa Tangayika na Tanzania
 
Tupa kuleee....pambaf....yanapenda kuvuna yasipopanda...
 
Wakuu heshima mbele sana,

Kumekuwa na sintofahamu nyingi sana mara baada ya Serikali kwa bahati mbaya au makusudi kugawa fedha ya change ya Rada Tanzania bara pekee na Tanzania visiwani kutokupata hata centi moja, Wabunge wengi wa Zanzibar wameonekana kutokupendezwa na swala hili, Je ni sahihi kwa mgawo wa Rada kugawanywa bara pekee na si visiwani..?
serikali ya muungano ndio Tanganyika kwa maana nyingine serikali ya muungano haipo ndio maana tunataka serikali Tatu,maana serikali ya Tanganyika ndio imevaa koti la muungano, hamjaelewa tu?
 
Wakuu heshima mbele sana,

Kumekuwa na sintofahamu nyingi sana mara baada ya Serikali kwa bahati mbaya au makusudi kugawa fedha ya change ya Rada Tanzania bara pekee na Tanzania visiwani kutokupata hata centi moja, Wabunge wengi wa Zanzibar wameonekana kutokupendezwa na swala hili, Je ni sahihi kwa mgawo wa Rada kugawanywa bara pekee na si visiwani..?

Haya ni miongoni mwa madhara ya kuwa na serikali mbili!
 
Back
Top Bottom