Ni chuki zao ndo zinawafanya wahc 2nawanyonya,umeshawah kuona wabara wanavyonyanyaswa Z enji? Baa zao zinachomwa,je umewah kuckia duka la mpemba limechomwa moto Dar au Mby?
Kwa mtazamo wangu hizi chokochoko hazitaisha, hata kama wakipiga kura, na wanaotaka muungano kuvunjika wakawa wachache, siku itafika watadai kwa nguvu tu.Hii ni hatari kwani hao wachache wataendelea kumwaga sumu kwa wengine.Ni kama ilivyokuwa madai ya mfumo wa vyama vingi mwaka 1992....wale wachache (20%) waliotaka vyama vingi wangelikataliwa...hali isingetulia mpaka wangekuja dai haki yao kwa nguvu.Hii hata kwa zanzibar inaweza ku-apply....nafikiri tuwaache waamue hatma ya nchi yao...mimi nimekaa na wazanzibari wa kawaida karibu wote walionesha kutoutaka muungano, wamekuwa ni watu wa kulalamika kila wakati...wanaona tunawanyonya...hata katika masomo wakifeli wanaona wanaonewa...juhudi hawana, hawapendi kufanya kazi kwa kujituma...jamani tuwaache waondoke kwa amani...dar si mbali watakuwa wanakuja kutusalimia...bara hatutapoteza kitu...tuna natural resouses kibao, virgin ardhi kubwa, misitu, mito, madini, mafuta,gesi, wanyama. Kama tutaacha ufisadi..na kulitumikia taifa kwa moyo wote huku serikali ikilipa watumishi malipo bora...tutapiga hatua kubwa sana kimaendeleo ndani ya muda mfupi tu.
Hao wanaosema hawautaki muungano ni wale vikaragosi vya sultan Jamshid anaetaka kurudu kwa mlango wa nyuma ; kwani mwanae wa nje amepata madaraka sasa huko Zenj!!
Mkuu unakuwa kama mgeni na issue zinazohusu muungano? Zingatia haya;
Mimi naupenda Muungano but wanzanzibar wanakera mno,chokochoko nyingi wakati kiuchumi bado wako hoi....kama tunataka kuendelea nao tufanye mchakato wa kuwa na serikali tatu...FULL STOP...
- Mara ngapi ile kamati iliyochini ya Makamu wa Rais na waziri kiongozi(kabla ya marekebisho ya katiba zenji) walikaa na kutudanganya kuwa mapungufu yanafanyiwa kazi na hatuoni mabadiliko?
- kwanini bado watanzania mnapenda kuendelea kudanganywa kwa mambo yaliyowazi?
- Kwa hakika mapungufu ya Muungano HAYAZUNGUMZIKI tusidanganywe na viongozi wasio waadilifu na wasio litakia mema taifa hili..
- Kama bado tunaupenda Muungano hatuna budi kubadilisha mfumo wake hasa katika serikali...
Umoja ni nguvu ikiwa wote mnajenga kitu kimoja. Lakini kama mmoja anajenga kitu chake kwa kutumia fito za wote inakuwaje? Zenj hawatumii tu fito za wote ila wanachomoa fito zilizojengwa kwenye nyumba. Kwa mfano walidai wapeperushe bendera yao - wakapata; wakataka wimbo wao - wakapata. Walipobadili katiba ili wajitenge zaidi wakasema Znz ni nchi. Hapa wakavunja katiba ya muungano kwa waziwazi ila mkuu wa nchi amawanyamazia. Hapo kuna muungano?
Nonda at work, plz usipotoshe Nonda uchumi wa zanzibar ulikuwa mzuri sio kabla ya union bali sema kabla ya Mapinduzi, ni mapinduzi ambayo yaliwafukuza masettlers wengi wa kiarab na kupunguza imani ya wafanyabiashara hao kuwekeza zanzibar,kama ilivyokuwa huku bara na azimio la arusha-achana historia ya maskani. Karume akakuta pesa akatumia bila kuwekeza ktk return endelevu ili kuwa na revenue endelevu-zilipoisha kwisney. Kwanini kila falure yenu nyie zenj mnadai ni bcz Tanzania?(eh sory ni Darnyika)!
Hivi ulishakaa ukafikiria kuwa labda makubaliano ya kuungana yalikuwa yamefikiwa kabla ya mapinduzi? I.e. Tanganyika itoe msaada kwa kina Karume in return tuungane?Hapo nilipoweka red naomba utafakari yafuatayo: Mapinduzi ya Zanzibar yametokea January 12 1964, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulifanyika tarehe 22 April 1964 (siku rasmi uliposainiwa mkataba wa Muungano) - jee ni siku ngapi? Jibu 112!. Sasa kama umewahi kusoma historia ya Zanzibar utajua kabisa kwamba kwa kipindi hicho hata Zanzibar yenyewe ilikuwa haijakaa sawa. Na hata huku Tanganyika hakukuwa sawa baada ya mutiny iliyotokea January 19 (wiki moja baada ya mapinduzi). Kama kila kitu kilikuwa poa haraka zilikuwa za nini?
Hamtokaa salama!! luv this one please watch it all! its' amazing stuff!!
Nonda at work?
Nonda mpotoshaji?
Nonda ana historia ya Maskani?
Nonda mzenj?
Tanzania....Darnnyika?
Mkuu.
Ningependa sana kuchangia juu ya mchango wako lakini naona umejaa jazba.
La msingi bila ya kuweka wazi ni kuwa umekubali kuwa tatizo ni viongozi, inatosha. Viongozi wa Tanzania, Tanganyika na Zanzibar. Wa Zanzibar siwalaumu sana kwani wamebanwa sana na Muungano.
Nimefurahi kusikia maoni yenu watanzania bara. Sisi wazanzibari tunataka nchi yetu. Sivo kamwe hivo munavofikiria kuwa ulimwengu wa ulaya wanakuwa kitu kimoja. East africa wanakuwa kitu kimoja. Huwezi kufananisha mapatano/ makubaliano na kutawaliwa. Sisi wazanzibari tumetawaliwa kikoloni. Na mtu akisoma nakala zenu, zinaonyesha wazi dharau mulionayo dhidi ya wazanziabri. "tukiwaachia nchi yao watauawana wao kwa wao". Kauli kama hizo ni za kejeli na wengi wenu hamujuwi athari ya muungano dhidi ya Zanzibar. Ikiwa mutakuwa na subira mukataka kujua kinachowafanya wazanzibari wakaukataa muungano pengine munge faidika katika kujua matatizo ya utawala wenu.Sisi ni wazanzibari popote pale tulipo duniani wala hatujitambulishi kama watanzania/ wabongo. Hilo ni lazima mulikubali katika akili zenu. Tuliweza kushirikiana kabla muungano na yunaweza kushirikiana baada ya muungano lakini mambo ya kuburuzwa na nchi yetu basi. Wala musifikiri tunaogopa, la hasha waliosababisha midahalo ya katiba Tanzania ni sisi wazanzibari na ukitaka kujua zaidi, tembelea blogi za kizenj uone kama ni waoga wakusema. Miezi miwili sasa hivi inaendelea mijadala na kongamano za katiba na wanaozungumza ni wananchi wa Zanzibari kwa mapenzi ya nchi yao Zanzibar. Tunawataka na nyinyi mulio bara muwe na kongamano kama zetu mujadili mustakbali wa nchi yenu.
Unajuwa hii kauli ya mmoja kujenga kitu chake kwa kutumia fito za wote. Unaonaje hii tabia ya Tanganyika kujijenga kwa fito za Muungano hujaiona bado? Hebu nitafautilishie Bunge la Muungano na lile la Tanganyika? Bajeti ya Muungano na ya Tanganyika. Rais wa Muungano na Rais wa Tanganyika? Nafikiri hutoweza kutafautisha na huku ndio kutumia fito za Muungano kuijenga Tanganyika. Mfano mmoja ni ni umeme kwani ule umeme ni wa nani wa Muungano au wa Tanganyika?
Kwa upande mwengine Zanzibar inajengea fito zake mwenyewe na iwapo Muungano ukivunjika basi walichofanya kitabaki Zanzibar na kwa upande wa Bara kitabaki bara lakini kilifanywa kwa jina la Muungano.
Upupu mtupu, tena unawasha!
Sikilizeni,watanganyika/watanzania nyinyi hamuuelewi maanga ya muungano na vipi munafaidika na vipi munapata hasara,wazanzbari ni watu ambao wasomi,wafanya biashara,na wenyewe uwezo kwa silimia kubwa ukipiga hesabu ya wananchi wa zanzibar.
Muungano unakuja kiuchumi,na uchumi ni kkifedha,wazanzibari ni wafanya biashara,ipo katika damu yao hasa,kwa hiyo katika huu muungano wao wanaufahamu zaidi kuliko watanganyika,kutokana wao ni wafanyaji biashara,kiuchumi hauwasaidiii,nyie ndio munao faidika muungano,kiufupi ni kwamba baadhi ya watu hawafahamu vitu gani ambavyo vinafanya nchi ukiwe kiuchumi ukiwacha hizo rasilimali mulizonazo.
Muna ropoka maneno tu ,,oh vunja waache wandee kwaoo,ah nini wewe,nyie ndio mutakao athirika,sisi wazanzibar tutabaki kama wazanzbari,jee nyinyi ? Kuna makabila kibao,na sasa kumeingia na udini,kutakuwa hakuna mtanganyika,na nyerere ameshawaleza,.musije kuiyacha zanzibar,kwani anafahamu fika kuwa zanzibar itabakia kuwa zanzibar.
Muungano huu hauna maana kwa wazanzbari kiuchumi,kwa maslahi yao kinchi,,hakuna mtu anaetaka kuuza utaifa wake,katika muungano kulikuwa na mataifa mawili,tanganyika na zanzibar,jeee leo hii mmoja afute utaifa avae koti la muungano huoni kuwa ni ulakini na usanii ?
Kura ya maoni sio wauliza wananchi kuvunja muungano au serikali tatu au moja...hapanaa
KURA IWAULIZE HIVI,Munataka muungano au hamutaki ?
muungano huo ukiwa unautaka uwe vipi ? Serikali tatu au wa kibiashara tu kama EAC.
Amueni juu ya nchi yenu. Kwa maoni yangu sisi hatuna tatizo.Tutatoa baraka zote.Mkisha ondoka mtakuja gundua mchawi wala si muungano....matatizo mliyonayo ni mengi sana tu.Kwa mtazamo wako haki ya Zanzibar ni chokochoko navuguvugu za kudai haki huko kwenu ni kitu takatifu? Kuhusu maisha ya Wazanzibari ni bora ukanyamaza kwani Zanzibar haikuwa hivi kabla ya kuingia CCM na halafu si nyie mnaolalamika kuwa Wapemba wametajirika? Sasa mvivu nani wewe unaililia umasikini na yule alitajirika? Mnapochangia bora muangalie dharau zenu zisije zikakurudieni.
Amueni juu ya nchi yenu. Kwa maoni yangu sisi hatuna tatizo.Tutatoa baraka zote.Mkisha ondoka mtakuja gundua mchawi wala si muungano....matatizo mliyonayo ni mengi sana tu.