Zanzibar kumekucha - Abdallah Issa

Mimi nasubiri 2010. Nasema tu nisisikie watu wanajiliza hapa kuwa wameibiwa, mnasikia enyi jinius na wenzenu toka zenji? damu ya wapemba itadaiwa mikononi mwenu na Seif!
 
Haya makubaliano ya muafaka bila kuwa na maandishi yanatia mashaka.
 
makoko mbona hueleweki----una maanisha nini
Kabuche,
Yakhe ni kiswahili sasa sieleweki vipii? Si unajua tena wanasema ni rahisi kwa Mwizi kumtambua mwizi au Mchawi kumtambua Mchawi n.k nayo hutokana na hulka ya Matendo na Tabia. Sasa ikiwa fulani atadai oh Fulani hivi au vile, basi kuna namna ...................au vipi? (Narudia Ashakum si Matusi). Naamini nimeeleweka.
 
Haya makubaliano ya muafaka bila kuwa na maandishi yanatia mashaka.
Maverick has said it all!

Mara ngapi CCM na CUF wamekaa vikao vya muafaka na maamuzi ya vikao kukanwa kweupe? Lengo la Karume ni kutaka "utambuzi wa Kimataifa", kusafisha maisha yake ya kisiasa baada ya Urais wa Zanzibar! Kesho ataingia kichaa mwenye "mipasho" zaidi ya Karume, na atawakana kweupee!
 
Kila la kheri Mola awe nanyi.
Mola anawasaidia wale wanaojisaidia, hawezi kusaidia kwenye makubaliano kama yale ya "Mangungo wa Msovelo" katika karne ya 21.

Siasa za visiwani ni kigeugeu, hayo makubaliano yalipaswa kuwekwa kwenye maandishi ili yaheshimiwe hata na uongozi unaokuja. Anachofanya Karume ni kama alivyofanya Pilato (soma Biblia)
 
kwani tatizo liko wapi jamani kwani hata week bado haijamalizika leo imekuwa maneno mengi ya uzushi tu inabidi kwanza tusubiri nini kitaendelea huwezi tu mkutane leo na mumalize kila kitu hata dem ukimtongoza lazima atakujibu nimekubali lakini subiri sasa leo mnamlaumu seif bure yeye si keshaseme subirini angalau miezi 6 muone sasa leoleo mnataka mambo yote yamalizwe kwa muda mfupi hiyo haiwezekani jamani lazima mujue kuna kitu kinakuja si bure huo sio uamuzi wa karume wala seif na wala si waccm kuna nguvu fulani ndio ilotumika hawa kukutana naamini mtakuja ona mbona john garangi alikubali kuacha vita vya sudan yakusini alikubali hivihivi tu si kulikuwa kuna nguvu fulani ndio ilosukuma kupatikana maelewano msiwe na pupa mtakosa vingi vinono
 
Sura na Aya Tafadhali. Biblia ni kubwa toka Mwanzo hadi Ufunuo.
 
Jamaa wanataka za Dr Remmy WAJA LEO WAPATA LEO!! Wakumbuke Roma haikujengwa kwa siku moja.
 
Mimi nasubiri 2010. Nasema tu nisisikie watu wanajiliza hapa kuwa wameibiwa, mnasikia enyi jinius na wenzenu toka zenji? damu ya wapemba itadaiwa mikononi mwenu na Seif!
Hebu subiri tu wewe mbona unaharaka, SMZ weshafungulia mbwa zamani...na kabla ya uchaguzi wa 2010 kuna suprise ya nguvu,itawaacha hoi wale wooote,kama nyinyi wenye mashaka mashaka, tulia wewe endelea tu na operesheni sangara
 


Mkuu asante sana
 
Kweli kumekucha lol. Lakini hawa wote walikuwa CCM.
 
Mipasho imeanza..., yetu macho!
 
jamani tafadhalini kwa yeyote anojua wapi nitaweza kudownload taarab to my ipod naomba nijulisheni......this guy, he's my idol I'm dying to get his songs,pleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeease
 
Wazenj jamani... Nyerere alipokubaliana na Karume kuhusu Muungano waliimba sana kuusifia, mara haikupita muda walianza kuuliza uhalali wa Muungano huo kusainiwa na baadhi ya viongozi wachache....Leo watu wawili wamekaa na kukubaliana, tunazisikia sifa na hongera nyingi wasiulize maswali yale yale ya Muungano..
Kaazi kweli kweli!
 


Mkandara, basically unachosema ni kuwa the stage huko mbeleni wakati Seif na Karume hawapo imeshakuwa set kwani wengine watakuja na kuhoji uhalali wa makubaliano hayo. Angalau ya Nyerere na Karume yalifanywa hadharani na tukaona wanatia saini makaratasi! haya mengine .... ila tunaambiwa ni halali. Labda kwa sababu yanawahusisha Wazanzibari... well.. Karume ni Mzanzibari?
 
Tumekusikia mkulu.
wambileee haoooo!
 
siye hatuna shida na huo wimbo,je october imekubalika?
usije rudi hapa na kibao kingine oooh wametunyonga oooh mara vileee!
Mungu wasimamie Wazanzibar.
 
Kusema ukweli makubaliano ya Karume na Seif yangekuwa na maana kama yangewekwa kwenye kumbukumbu za kimaandishi. Vinginevyo ni uzushi mtupu! Hii ni kwa sababu binadamu wanabadilika kama kinyonga kutegemeana na mazingira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…