Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,589
- 1,679
Habari zimetapakaa kuwa Zanzibar inauza visiwa vingine 9 mwaka huu, baada ya mwaka jana kuuza 10 kwa thamani ya $ 261.5 milioni! Kuna utatanishi ikiwa visiwa hivyo vinauzwa au vinakodishwa, kiasi wana habari wametumia istilahi zote mbili hizo. Wakuu wanasema wanakodisha.
Kwa uzoefu wangu, napenda sana kuwaamini watu wa nje wanapozungumzia mambo nyeti ya Tanzania kuliko wakuu wa Tanzania. Wakuu wengi wa Tanzania aidha huona uongo ni 'halali' au hawaoni kuna umuhimu wa kuwaeleza Watanzania ukweli: kwa vile, anyway, sisi ni mazuzu tu! Hiyo ni ikiwa wataamua kutueleza. Mara nyingi hawaoni hata haja ya kufanya hivyo!
1- Jee, jambo hili lilijadiliwa na wananchi, kabla ya wakuu fulani tu kufanya uamuzi?
2- Pesa zinazopatikana katika mauzo hayo zimepangiwa nini? Hizo $261.5 zimetumiwa katika nini?
3- Mara nyingi mwekaji -hasa Mzungu- anaponunua kitu, hataki 'wenyeji' wafike hapo, labda kwa kazi za kukata majani na kufagia tu.
Siku hizi wamegundua njia bora zaidi ya kuwazuia 'wenyeji' : wanaweka bei za kutisha ambazo wanajua 'mwenyeji' hata akiwa nazo, hathubutu!
Mkuu wa ZIPA amewaambia Wazungu, bei ya kisiwa inaanza dola milioni moja hadi milioni 75, tegemeana na ukubwa wake. Visiwa hivyo ni Miwi, Popo (hekta 450,Sumi 3.5 ha, Kwata 6.7 ha, Njao 470 ha, Kashani 31.8ha, Jombe 76 ha, Mtambini 200 ha na Fumbo 37 ha
Bill gates, tajiri namba nne duniani mwenye fedha 136.1 b ameshanunua Kisiwa cha Mnemba, Kisiwa kikubwa zaidi ya hivyo. Anachaji dola 2,000 kwa siku na wasiokuwa wageni hawaruhusiwi kutia mguu huko! Pia sehemu inayomzunguka kwa mita 200 ni marufuku mtu kupita huko. Inaitwa 'exclusion zone'!
Kuuza ardhi au kukodisha kumeenea sana nchi za Ghuba kama UAE (Dubai). Pengine wakuu wetu wanataka kuiga huko. Lakini wenzetu huko huuza jangwa tena kwa masharti magumu. Pia kwa vile wananchi wao wana uwezo mkubwa utakuta nao wamenunua bega kwa bega na wageni. Hapa kwetu si hivyo. Twawauzia visiwa nusu ya Pepo! Tena hakuna namna yeyote mwenyeji ataweza ku enjoy huko. Sehemu hizi zinazouzwa ni za urithi wa mazingira na hawa wanakwenda kuchafua (wakuu watakwambia tumewaambia wasichafue!).
Swali ni hili: Hivi akili zenu zote hamkuweza kupata vyanzo vingine vya fedha isipokuwa kuuza urithi wetu? Lini watoto wetu watakuja kuviona visiwa hivi katika hali ile ile walioviacha babu zetu?
Na mnataka kufanya nini na pesa hizo? Nasikia wanataka kujenga hoteli moja iitwayo DOMINO itakayokuwa ya pili kwa urefu katika Afrika!
==
Baraka Shamte akielezea suala la kukodisha visiwa